Mwanamke mnyenyekevu hakosi mume.

Mwanamke mnyenyekevu hakosi mume.

Simaanishi wewe mgomvi mpendwa wangu nimetoa Hilo andiko kuonyesha kwamba mwanamke anaweza kufanya mazuri na familia ikafika mbinguni na akafanya mabaya familia yote ikateketea , hasa ulipozungumzia ufalme was mbingu
Okay nashukuru kwa neno
 
Mimi siyo mgomvi wala mchokozi ila it seems like anayetakiwa ahangaikie ndoa ni mwanamke peke yake maana sisikiagi mwanaume anatakiwa afanye nini ili aoe mke mwema au ili ndoa yake idumu kila siku ni wanawake tu na sisi tushajichokea saa hizi tunataka tuone na jitihada za wanaume
Acha tu kufikiria kuolewa kama umechoka
 
Ujumbe mzuri wafanyie kazi waachane na mambo yao ya Beijing,
 
Barikiwa sana.
habari za jumapili Wana jf
Leo nimetamani Sana kuongea na wanawake wanaotafuta kuolewa.Kumekuwa na wimbi kubwa Sana la wanawake wanaowalilia wachungaji wafanyiwe maombi ili waweze kupata wenza wa maisha.Hata wengine wamediriki kwenda kwa waganga ili waweze kuondolewa nuksi na kuolewa.
Mimi naamini kabisa mwanamke akikaa katika nafasi yake ya uanamke Kama Biblia inavyosema hawezi kukosa mume wa kumuoa.
Mwanamke mnyenyekevu Ni baraka kwa mume na familia.

Sifa za mwanamke mnyenyekevu Ni
Mtii, anasamehe, anasikiliza, anampenda Mungu, anashukrani anafundishika kirahisi, anakubali makosa na kuyarekebisha, mwaminifu na zingine unaweza kuongeza.

Hivyo basi mwanamke akiacha jeuri, kiburi, majivuno, wivu uliopitiliza, hasira, kununa nuna, ubinafsi, ubishi, uchoyo, kushindana sidhani Kama atahitaji kubadilisha makanisa kutafuta maombi Wala kwenda kwa mganga kuondoa nuksi,.

Wakolosai 3:18 Neno la Mungu linasema Ninyi wake watiini waume zenu Kama ipendezavyo katika Bwana

Mfano wa wanawake wanyenyekevu katika Biblia Takatifu Ni

SARA Tunaweza kuona jinsi Sara alivyokuwa mtiifu kwa mumewe Ibrahimu mfano walipokwenda Misri Ibrahimu alimwambia aseme kwamba wao Ni ndugu na akakubali Mwanzo 12:11

ABIGAIL Jinsi alivyomwokoa mumewe Nabali(1samwel 25:3-27)

ESTHER mwanamke mnyenyekevu aliyewaokoa Wayahudi wasiuawe

Wengine Ni Ruth, Mariam Mama wa Yesu, Elisabeth nk

Tunapozumgumzia UTII maana yake ni kufuata maelekezo uliyoagizwa bila maswali , Wala kusita kwa wajeda wanaelewa zaidi Neno kutii kwa hvyo sidhani Kama Kuna mwanamke anahitaj kubishana na Neno la Mungu kuhusu utii.
Tabia njema ya mwanamke inaweza kubadilisha tabia mbaya ya mwanamume.
Hivyo basi kuanzia Leo wewe mwanamke ambae unahangaika kutafuta ndoa , umelia vya kutosha ,umefunga ,umekwenda kwa waganga jifunze unyenyekevu kwani Ni kitu unaweza kujifunza, Kuna wanawake wamezaliwa hvyo Ni wanyenyekevu lakini Kama huko hvyo unaweza kujifunza.
Kuna vijana wengi Sana wa kiume mtaani wanaotafuta wachumba lakini wanasema hawawaoni wanawake wa kuoa, wakati huko makanisani wanawake wamejaa wanaomba maombi.
Povu ruksa kwa wale wa "Haki sawa"
Jumapili njema
 
Elimu ya bure umewapa kinadada na kinamama. Hongera sana mkuu kwa thread hii.
 
Mwanaume mnyenyekevu hakosi mke mwema.
Hizi discourse za kuwataka wanawake wanyenyekee tu sizipendi kabisa.
 
Back
Top Bottom