Mwanamke mkongwe zaidi duniani, Violet Mos Brown aaga dunia

beth

JF-Expert Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
3,881
Reaction score
6,378
Mwanamke mmoja wa Jamaica anayedhaniwa kuwa mtu mkongwe zaidi duniani, Violet Mos Brown amefariki akiwa na umri wa miaka 117.

Waziri Mkuu wa Jamaica alitangaza kufariki kwa mwanamke huyo kupitia mtandao wa Twitter.
Vyombo vya habari vya nchini humo vilisema alifariki kwa utulivu katika hospitali moja katika mji wa Montego Bay.

Violet Moss Brown, aliyekuwa mtu mkongwe zaidi mapema mwaka huu, alizaliwa mwaka 1900.
Alisema kuwa aliweza kuishi muda mrefu na kwamba aliweza kula karibu kila kitu isipokuwa nguruwe na kuku.

Alisema pia hakunywa pombe kali.
 
R.I.P...kala chumvi ya kutosha aisee
Kuishi kwingi kuona mengi
 
Apo ni nguruwe tu mnamtafuta uchokozi, na hatuachi kumla mdudu
 
Mwanamke mmoja wa Jamaica anayedhaniwa kuwa mtu mkongwe zaidi duniani, Violet Mos Brown amefariki akiwa na umri wa miaka 117.

Waziri Mkuu wa Jamaica alitangaza kufariki kwa mwanamke huyo kupitia mtandao wa Twitter.
Vyombo vya habari vya nchini humo vilisema alifariki kwa utulivu katika hospitali moja katika mji wa Montego Bay.

Violet Moss Brown, aliyekuwa mtu mkongwe zaidi mapema mwaka huu, alizaliwa mwaka 1900.
Alisema kuwa aliweza kuishi muda mrefu na kwamba aliweza kula karibu kila kitu isipokuwa nguruwe na kuku.

Alisema pia hakunywa pombe kali.
Bibi yangu Mkubwa ana Miaka 130, yupo huko Meru, Naomba niitie Guinness waende wakaweke rekodi zao!
 
Back
Top Bottom