Mwanamke mjamzito anaruhusiwa kunyonyesha mtoto?

successiful dreamer

Senior Member
Joined
Sep 10, 2019
Posts
103
Reaction score
191
Habari yenu wanajamvi?

Nawasalimia wote. Naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Hivi inakuaje mwanamke akiwa na mtoto mdogo akapata ujauzito mwingine wakati alikua bado ananyonyesha?

Je, anaruhusiwa kuendelea kunyonyesha? Au kwa bahati mbaya ujauzito huo ukiharibika anaweza kuendelea kumnyonyesha mtoto wake?
 
Mmmmm hospital wanasema unaruhusiwa endeleaa ila majumban wanasema hapana utaharibu mtt sjui nnn na nn so hiii sjuag mpaka leo imekaaje. Wacha nam ntasoma coment nijifunze.
 
Mnaambiwa mwanamke akishazaa apumzike miaka miwili ndio apate ujauzito mwingine. Sasa wewe mkeo ananyonyesha halafu unamjaza mimba tena, sasa utakula ulikopeleka mboga
 
Hutokea alaf saiz mambo ya kupumzika michosho bora upige chap chap muanze kulea tu[emoji3][emoji3][emoji3]
 
Wakati namsindikiza wife hospital kulikua na watu wa uzazi wa mpango wanatoa somo.

Mojawapo walilosema ni kwamba kunyonyesha ni njia mojawapo ya uzazi wa mpango. Ukiwa unanyonyesha una chansi ndogo ya kupata mimba.

Now tuchukulie umepata.

Darasani tuliambiwa ukipata mimba huku unanyonyesha mwili wako unafunga uzalishaji maziwa automatically. Ni unaanza kuyahifadhi kwaajili ya mtoto mtarajiwa.

So scenario yako ni ngumu kuwezekana.
 
Anaruhusiwa mkuu, na hata huyo mtoto mdogo akizaliwa anaweza kuendelea kunyonya na ndugu yake . Achana na maneno ya mtaani, mwache dogo aendelee kupata haki yake.
 
Nipo nimebana hapa kona nasubiria wajuvi na wabobezi wa haya mambo..
 
Anaruhusiwa mkuu, na hata huyo mtoto mdogo akizaliwa anaweza kuendelea kunyonya na ndugu yake . Achana na maneno ya mtaani, mwache dogo aendelee kupata haki yake.
Ni kweli kabisa hili, na watoto wanakua na afya nzuri tu
 
Inawezekana vizuri,na mtoto hapati madhara yoyote,ila Tu mara nyingi unakuta huyo mama k anakua anajiskia hovyo mimba ikiwa Changa so anashindwa.
 
Mnaambiwa mwanamke akishazaa apumzike miaka miwili ndio apate ujauzito mwingine. Sasa wewe mkeo ananyonyesha halafu unamjaza mimba tena, sasa utakula ulikopeleka mboga
Jaza nikujaze ~joti[emoji851][emoji851]
 
Inawezekana vizuri,na mtoto hapati madhara yoyote,ila Tu mara nyingi unakuta huyo mama k anakua anajiskia hovyo mimba ikiwa Changa so anashindwa.
Yeah inategemeana mwingine mimba ikiwa changa anaumwa sana ila kama yuko fresh basi watoto ananyonyesha vizuri tu
 
Ananyonya bila Shida ila ukikaa na jamii wasioamini hivyo,Mtoto akinyonya atakufa au kunyongea kwani miiko mingi na mila zake zinasimamiwa na ushirikina.

Mfano ukitembea na mdogo wa mkeo da hakuna shida ila usije thubutu gamboshi utatolewa msukule halafu wakati wa mazishi watasema alipata mkosi wa kutembea na shemejiye
 
inaruhusiwa kabisa kuendelea kunyonyesha
mi niliambiwa hivyo hospitali nikaendelea kunyonyesha nikiwa na mimba bila shida.
 
Habari yenu wanajamvi?

Nawasalimia wote. Naomba niende moja kwa moja kwenye mada. Hivi inakuaje mwanamke akiwa na mtoto mdogo akapata ujauzito mwingine wakati alikua bado ananyonyesha?

Je anaruhusiwa kuendelea kunyonyesha? Au kwa bahati mbaya ujauzito huo ukiharibika anaweza kuendelea kumnyonyesha mtoto wake?
Anaruhusiwa kunyonyesha bila shida. Ila mnatakiwa kufahamu ya kuwa maziwa ya mama hayana virutubisho vya kumtosheleza huyo mtoto. Nashauri anatakiwa kama ametimiza miezi sita aanze kumlisha vyakula vingine na juisi ya matunda asilia (yaani atengeneze mama mwenyewe juisi hii). Lakini asiache kumnyonyesha mtoto kabisa.

Mimi ilitokea ishu kama hii, nilinyonyesha hadi wiki moja kabla ya kujifungua ila pia nilimkazania sana uji wa lishe, juisi ya matunda ya kutengeneza na vyakula vyenye virutubisho lakini Mungu ni mwema alikuwa na afya na nilijifungua mtoto mwenye afya nikaendelea kunyonyesha bila ya shida yoyote. Sasa hivi nina mapacha wangu wa nje wenye afya njema sana. Mungu ni mwema!
 
Wakati namsindikiza wife hospital kulikua na watu wa uzazi wa mpango wanatoa somo.

Mojawapo walilosema ni kwamba kunyonyesha ni njia mojawapo ya uzazi wa mpango. Ukiwa unanyonyesha una chansi ndogo ya kupata mimba.

Now tuchukulie umepata.

Darasani tuliambiwa ukipata mimba huku unanyonyesha mwili wako unafunga uzalishaji maziwa automatically. Ni unaanza kuyahifadhi kwaajili ya mtoto mtarajiwa.

So scenario yako ni ngumu kuwezekana.
Inawezekana sana mkuu, imeshatokea mara nyingi sana. Mimi ni mmojawapo.
 
Ahsante kwa kunitoa ushamba. Na hata mtoto mpya alikuta maziwa ya kumtosha?
 
Ananyonya bila Shida ila ukikaa na jamii wasioamini hivyo,Mtoto akinyonya atakufa au kunyongea kwani miiko mingi na mila zake zinasimamiwa na ushirikina.

Mfano ukitembea na mdogo wa mkeo da hakuna shida ila usije thubutu gamboshi utatolewa msukule halafu wakati wa mazishi watasema alipata mkosi wa kutembea na shemejiye
"Gamboshi maana Yake Nini?"
 
Back
Top Bottom