Mwanamke kwa asili ni Mtawala

Ramark

JF-Expert Member
May 19, 2015
1,989
1,440
Jana kwenye kipindi cha Women Matters Dr Mwaka alisema Mwanamke ni mtawala hivyo hataki haingiliwi kwenye utawala wake wa mapenzi.

Mimi najua kwa asili mwanamke ni mtawala nakubali hili ikiwa mimi ni mume na baba wa familia hivyo nakubaliana na Dr Mwaka kwa upande wa mapenzi lakini naongeza kuwa huyo mwanamke ni mtawala wa familia au nyumba kwa sababu:

1. Anajua bajeti ya familia hata kama hapewi fursa ya kuiandaa

2. Ndiye mtekelezaji wa bajeti ya familia.

3. Anajua structure ya familia na nyumba kwa ujumla(nibishe).

4. Anajua majukumu yake na muda wa kazi (rejea Mithali 30, mwanamke bora ni yule anayeamka kabla ya wote na kuandaa mahitaji.

5. Ajajua kupanga vipaumbele vya familia na yeye akiwemo isipokuwa hajui vipaumbele vya baba na ndiye maana akiandaa vipaumbele hataji mahitaji ya baba isipokuwa yeye na familia kwa ujumla ila kwa uchache kwa baba na ndiyo maana nawambia wanaume kila pesa unayoipata hakikisha 30% umekula wewe binafsi na 70%kwa familia kwani ukipeleka yote hutapata hata ya kunywa bia ila atakupa ya matumizi bila kujali inatosha au haitoshi (kwa wazoefu wa ndoa wanajua)

6. Ni watunza hazina wazuri na ndiyo maana usipompa kutunza anakuwa fisadi. Au mwizi na akitunza hakika ametunza

7. Wanajali familia na ndiyo maana bosi anajali watumishi wake.

8. Hataki kuingiliwa kwenye utawala wake ikiwemo kuingiliwa katika majukumu hayo juu na ndiyo maana akiingiliwa kinawaka ikiwa mamamkwe au wifi au kimada hakubali na ndiyo sifa ya mtawala.

Zingine karibu uongezee.

Kila kwenye mafanikio ya mwanaume kuna mwanamke pembeni ambaye ndiyo mtawala(administrator) kwani unaweza kuwa na shirika lkn yupo mtawala wa yote au tumuite CEO au DG hivyo tuwashukuru na tuwapongeze sana, hata kama hujaoa na ukawa unafanikiwa basi katibu au meneja wako ni mwanamke au ni mwanaume mwenye mke hivyo utaendelea au utafanikiwa lkn ujue aliye na mke atafanikiwa kabla yako, si lazima pesa inaweza kuwa mipango au second income.

Watu watauliza vipi mapadre? Ndiyo hawana maendeleo binafsi na ni wafujaji wa mali zao binafsi. Isipokuwa za umma kwa kuwa yeye si mwamuzi bali mtawala na hategemei hiyo kazi kuishi au kufanikiwa bali kwa mazoea na inafanikiwa hakikutana na watu wenye watawala nyumbani na ndiyo maana mkurugenzi wa fedha TEC ni mlei ila vatican ni Askofu kwakuwa si kwa manufaa ya nchi wala mtu bali kanisa! Ndiyo maana hatuwezi kuwa na Rais bachelor.

Kongole wanawake endeeleni kutawala ili dunia iwe salama. Mwanamke akishindwa kuwa mtawala mkamilifu na familia inayumba yaani akishindwa kufutata hizo sababu juu.
 
Katika familia "baba ni kichwa na mama ni shingo " One shingo inavyopeleka kichwa sehemu inayotakiwa.
 
Ni mtawala? Kenu wapi? Utakuwa Makonde wewe? Huku Mara siyo hivyo.
Nawajua wa mara pia na wamakonde. Hoja si kabila au taaboos hoja hapa ni asili yaan tangu kuumbwa ndivyo ilivyo ikikimbuka Eva ndiye alimpa tunda adamu yaan mwenye wa wajibu wa kumlisha ni mwanamke hata kisa cha Samson aliyemnywesha kinywaji n mwanamke. Tulipewa na Mungu na msaidizi yaan wewe mmliki yeye mtendaji ndiyo maana nilimuota CEO, DG na Administrator
 
Neno la Mungu linasema:

" (Mungu) Akamwambia mwanamke, hakika nitakuzidishia uchungu wako, na kuzaa kwako., kwa utungu utazaa watoto., na tamaa yako itakuwa kwa mumeo, naye atakutawala." MWANZO 3:16.

Lakini nataka mjue yaa kuwa kichwa cha kila mwanamume ni Kristo, na kichwa cha mwanamke ni mwanamume, na kichwa cha Kristo ni Mungu". 1WAKORINTHO 11:3.

MUMEO ATAKUTAWALA!

KICHWA CHA MWANAMKE NI MWANAMUME! ... these are facts from God Almighty.

Mwanamke yuko duniani kumsaidia mwanaume.

"BWANA Mungu akasema, Si vema huyo mtu (Adamu) awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye." MWANZO 2:18
 
Hapo kwenye namba 5 hapo, kwamba kuna kumpelekea huyo ‘mtawala’ huu mshahara..!!

Scratching my damn head!
 
Ceo au administrator hachukui nafasi ya owner au chairman au president ambaye ndiye founder na mtoa maono au vision ya taasisi

Tusichanganyikiwe na lugha jaman
Maagizo ya Mungu yapo vilevile na yanaheshimiwa nasi tuzingatie
 
Ni asili ipi hiyo unamaanisha bwashee.?

Kwa mujibu wa maandiko (kwa waaminio) huu ni ubatili, rejea katika kitabu cha 1Wakorintho 11:3-12
 
Tuambie pls


Sijui niiandikaje...nadhan watafiti wa mwili wa mwanamke wanawwza ielezea...! Me naamin hivyo....tuna nguvu zaidi ambazo wataalam wazielezee..sio zle za umatipapasi..hapana...!Kama sio basi naamini baadhi wanazo wanamiliki nguvu hizo!
 
Back
Top Bottom