Mwanamke kusikilizwa

Mwanamke kusikilizwa



Natumaini mmemaliza vyema weekend.... Poleni kwa wale ambao mlipatwa na maswahibu ya hapa na pale...


ASUBUHI YA LEO KATIKA KUPITA PITA HUKU NA KULE KWENYE MITANDAO MBALIMBALI NIMEKUTANA NA HILI NAOMBA KUSHARE PAMOJA NAMI, IWAPO LITAKUWA LIMEKWISHA JADILIWA HUMU NDANI BASI NAOMBA MNIWIE RADHI....

Mashitaka mengi huwapata wanaume kutoka kwetu sisi wanawake kwamba;

"Huwa hatusilikizwi na pia hatujaliwi"


Kumsikiliza mwanamke anapoongea ni pamoja na kuachana na kile ulikuwa unafanya, concentrate kwenye kile anaongea, kusikiliza hisia zake zinaongelea kitu gani na si kile mdomo unaongea tu.

Wanaume mnahitaji kufahamu kwamba wanawake mara nyingi huongelea matatizo yao kwa maana ya kuwa karibu na ninyi na kupata ahueni (relief) kutokana na matatizo tunayoyapata, si lazima mwanaume kuanza kutoa solution ya matatizo bali hata kusikiliza tu.

Mwanamke akipata matatizo hutafuta mtu maalumu wa kuongea naye, kumshirikisha hisia zake na kile kitendo cha kuongea humpa ahueni (relief) hivyo basi mwanaume kazi kubwa ni kumsikiliza na zaidi sana kuhakikisha anafahamu kwamba unamsikiliza.

MFANO

Mariamu anarudi nyumbani akiwa hoi na kazi pamoja na kusumbuliwa na bosi wake.
Anaporudi nyumbani anajisikia ni vizuri kuongea na mumewe na kumsimulia kinachomtatiza.

Fikiria Mariam ana wanaume wawili mmoja wa kweli (James) na wa pili ni kwa ajili ya kutufanye tuelewe mfano (Kelvin). Unadhani ni mume yupi kati ya James na Kelvin atakuwa amempa ahueni kwa matatizo yake na pia atakuwa alikuwa anamsikiliza?

Mariam: Kazi yangu ni ngumu sana hadi nakosa muda wa kupumzika!
James: Kwa nini usiache hiyo kazi na tafuta kazi nyingine ambayo utakuwa na muda.
Kelvin: Ooh! Pole sana inaonekana leo ulikuwa na siku ngumu sana mke wangu!

Mariamu: Yaani siamini nimeshindwa kumpigia simu Shangazi leo!
James: Usihofu atakuelewa, si anajua upo busy.
Kelvin: Ooh Pole sana mke wangu, basi pumzika kisha utampigia muda sio mrefu.

Mariamu: Unajua shangazi ana mapito magumu sana so ananihitaji kuongea naye:
James: Una wasiwasi mno na wewe, kwa nini unajisumbua wakati upo busy na kazi yako.
Kelvin: Pole sana najua leo umechoka, sogea basi nikukumbatie nimekumis sana leo. Baadae umpigie shangazi, hakikisha unawasiliana naye ili umsikilize anaendeleaje na matatizo yake.
(Mariam na Kelvin wanakumbatiana na Mariam ana relax)

NB: Mariam anakasirika na anamwambia James siku zote hunisikilizi na hunijali.
Pia anamwambia Kelvin: "Kila siku napenda sana kuongea na wewe, unanifanya kuwa mtu wa furaha, asante sana kwa kunisikiliza, kunijali na kunishauri najisikia raha kuwa na mume kama wewe Nakupenda sana mume wangu."

Ukweli ni kwamba James alikuwa anasikiliza, lakini kwa lugha ya mwanamke alikuwa hasikilizi kwa kuwa alikuwa anajitahidi kutoa solution kwa yale alikuwa mkewe Mariam anamwambia. Pia alikuwa anaongea kwa ukali fulani na sio kwa Mapenzi.

Kwa upande mwingine, Kelvin alikuwa anasikiliza kwa sababu alikuwa anaongea lugha ambayo mwanamke anaielewa na anaitaka na pia alikuwa anaongea kwa Mapenzi "Kimahaba" alikuwa anampa kile mwanamke anahitaji.
.

Wanaume wengi huwa hawawasikilizi wenzi wao, sio kwamba wanaziba masikio la hasha bali husikiliza kama ambavyo James alikuwa akisikiliza na anakuwa kama hayuko "concerned" na kile ambacho anaambiwa.

Je, wewe ni James au Kelvin?

Wanaume mbadilike jamani..............

Muwe na week nzuri

Wasalaam

CL




Hapo penye red Ukiona mmeo anaongea lugha unayoitaka kila siku ujue kuongoza familia kumemshinda na kama siyo muumini wa ninyim ujue anajiandaa kuhamia hivi karibuni
 
yaani umenigusa sana sijui nikuulize swali japo kidogo?

ngoja nikuache tu yr great thinker
Such a useful thread.

Well,

ukisoma vizuri majibu wanayotoa hao wanaume hapo juu utagundua kitu flani kwamba kuna mmoja anajua caring, na mwingine anajua scaring!

simlaumu sana James kwa kutoa majibu horror wala kumpa sifa sana Kelvin kwa kutoa majibu marvelous,

The issue here is, how are you related to the person you are giving feedback to the question? je ulimpenda kweli ndiyo maana ukawa nae? au ulilazimishwa na circumstance ndiyo ukamuweka ndani???

Women need relief from their men, that's true indeed!.... But too much is harmful, remember that!
 
Sawa sawa twinto..mm penda wewe daima. Hakuna ktu kizur kama kusklza na kujal na pengne hata kuomba msamaha pale wanapo kosea. Lakn mijanaume mengi hayajui hayo na yanapenda ubabe wakat ata simba mpole mbele ya mahab
 
cousin nimefurahia sana topic yako imenigusa sana na imenisisimua kiaina yake


nimeamua kutapika hapa cousini

huwaga nasemaga hawa wanaume wasio caring wakoje?
hawawezi kuchukuliana na wanawake jinsi walivyo hawawasomi wake zao kiundaini
na mara nyingi wengine huwaga wanakurupuka katika mahusiano yani ndoa
au wanalazimishwa na wazazi wao kuoa yule mzazi anayemtaka wakati hamtaki
anabaki kusema kuwa ni bora kumtii na kumsikiliza mzazi, eti ndo heshima
kwa mzazi akisema kula ........ utakula cause mzazi kasema huoni kuwa
unabemendwa kiaina na hiyo ndoa itakuwa yako na si ya mzazi kwani
wao wazazi walitafutiwa wake au waume wa kuishi nao, mila na tamadun
zingine zinatuingiza penye madhara wakati humo ndani mtaishi ninyi wenyewe
na ndo maana wanaume wengine hawawajali wake zao kwani walilazimishwa
wengine ilikuwa ni fashion kuoa hakuwa ana mapenzi ya dhati na huyo mdada

cousin charminglady acha niishie hapo maana nitamaliza mtama bure.....
 
Last edited by a moderator:
Wengi wenye ndoa zao ni majames sababu wako kimaisha zaidi ila kelvin hao ni usharobaro tu,ukijifanya unasikiliza sana ushauri wa mwanamke utabaki kusifia wanaume wenzako tu kuwa wana hiki wana kile we baadae sana.
 
wanawake hawana fomula moja, so ujidanganye ku-apply moja na kusahau nyingine
 
Yaani kama kuna kitu kinaniboa ni mtu kunismulia depressing story ya mtu hata hamhusu...why uje uni depress. ? Kuna Wanawake hata akitazama a sad movie anataka alie umbembeleze...
 
Yaani kama kuna kitu kinaniboa ni mtu kunismulia depressing story ya mtu hata hamhusu...why uje uni depress. ? Kuna Wanawake hata akitazama a sad movie anataka alie umbembeleze...

That is another issue hiv nilie kisa movie ahha duh hii kali asee halaf ntake kubembelezwa
 
Nitavuka daraja nikifika kabla ya hapo eneo husika mtu husika hali husika na muda husika huamua ni aina gani ya jibu utajibu lakini kabla ya yote jua mwanaume ni binadamu pia don't expect too much from them.
 
Swali kwenu wanawake hivi mnajuwa kuna wakati wanaume tunakuwa tumedhurumiwa mapesa kibao kwenye mishemishe zetu na tumejaa madeni mwili mzima? Je mnalijuwa hilo? Then unataka attension yangu wakati mimi hata hamu ya papuchi yako sina.

Kwa style hii waume zenu sasa badala ya kurudi bar usiku wa manane watakuwa wanarudi asubuhi kabisa.
 
James is romantic in his own way, some ladies get turned on by James' way of life.

Kwa muktadha huu mimi ni James, sijazaliwa kuwa romantic.
 
kumbe ndo maana akina Kelvin (mabrazameni) wanawapangaga sana, mnapenda mno maneno!!!
 
Kusikilizwa ama kutosikilizwa mwanamke anajitakia mwenyewe, lazima mtu a mark position yake. Kumbuka enzi ambazo EL ni PM, nani alikuwa anasikilizwa zaidi? Hapo alaumiwe nani?

Lakini pia huyu mwanamme yeye hana distractions zingine za maisha? Kwamba kilichobakia maishani mwake ni kum attend mkewe tu? Kuna siku za makavu na siku za kubembeleza. Ukibembeleza deile unakuwa Bus.hoke, kila kitu kwa kiasi.

Kelvin, sounds too fake for me, especially nikiwaza iwe January to December, James naye too rude kama ni January to December. Lazima kuwe na na ka balansi.

Asante kwa mchango wako Konnie, nimepata kitu hapa..
 
Ukitaka kufanya kila anachotaka mwanamke kufanyiwa lazima ujitoe ufahamu kidogo

Mkuu hebu badilisha hapo wewe ndio uwe katika nafasi ya huyo mke, afu awe anakujibu hivyo. Je utafurahi??? Unajua sometime unatakiwa kumfanyia mkeo/mwenzi wako kile ambacho nawe utapenda kufanyiwa, kutomfanyia kile ambacho haupendi nawe kufanyiwa...
 
Yaani hayo uliyoandika ndo huwa nafanya kwa wifi yako akionekana kukerwa na jambo lolote, huwa naacha nilichokuwa nafanya na kumsikiliza kwa makini, baada ya hapo huwa namwambia......pole sana kwa hayo mke wangu, katika swala hilo mimi naona jipe muda/pumzika kwanza/twende sehemu tupate faragha ya kulitafakari vizuri.......Hii njia pia inatumika kupata michepuko, maana kuna baadhi ya wanaume wanakuwa wakiwaharass wake zao, sasa mke akipata mtu ambaye anamsikiliza na kumshauri kwa kutumia busara, kuna uwezekano wa kuchepuka naye maana anaona huo ndye mfariji wake.

Usemayo ni kweli mkuu... Mwanamke anaweza kuchepuka hata kwa caring kidogo tu.

Hivyo basi mjitahidi kuwacare wake zenu...
 
Hakuna formula ya kuongea na mwanamke.leo akizoea hivyo atataka mapya.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom