Mwanamke kusikilizwa

Mwanamke kusikilizwa

CharmingLady

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2012
Posts
18,304
Reaction score
12,997


Natumaini mmemaliza vyema weekend.... Poleni kwa wale ambao mlipatwa na maswahibu ya hapa na pale...


ASUBUHI YA LEO KATIKA KUPITA PITA HUKU NA KULE KWENYE MITANDAO MBALIMBALI NIMEKUTANA NA HILI NAOMBA KUSHARE PAMOJA NAMI, IWAPO LITAKUWA LIMEKWISHA JADILIWA HUMU NDANI BASI NAOMBA MNIWIE RADHI....

Mashitaka mengi huwapata wanaume kutoka kwetu sisi wanawake kwamba;

"Huwa hatusilikizwi na pia hatujaliwi"


Kumsikiliza mwanamke anapoongea ni pamoja na kuachana na kile ulikuwa unafanya, concentrate kwenye kile anaongea, kusikiliza hisia zake zinaongelea kitu gani na si kile mdomo unaongea tu.

Wanaume mnahitaji kufahamu kwamba wanawake mara nyingi huongelea matatizo yao kwa maana ya kuwa karibu na ninyi na kupata ahueni (relief) kutokana na matatizo tunayoyapata, si lazima mwanaume kuanza kutoa solution ya matatizo bali hata kusikiliza tu.

Mwanamke akipata matatizo hutafuta mtu maalumu wa kuongea naye, kumshirikisha hisia zake na kile kitendo cha kuongea humpa ahueni (relief) hivyo basi mwanaume kazi kubwa ni kumsikiliza na zaidi sana kuhakikisha anafahamu kwamba unamsikiliza.

MFANO

Mariamu anarudi nyumbani akiwa hoi na kazi pamoja na kusumbuliwa na bosi wake.
Anaporudi nyumbani anajisikia ni vizuri kuongea na mumewe na kumsimulia kinachomtatiza.

Fikiria Mariam ana wanaume wawili mmoja wa kweli (James) na wa pili ni kwa ajili ya kutufanye tuelewe mfano (Kelvin). Unadhani ni mume yupi kati ya James na Kelvin atakuwa amempa ahueni kwa matatizo yake na pia atakuwa alikuwa anamsikiliza?

Mariam: Kazi yangu ni ngumu sana hadi nakosa muda wa kupumzika!
James: Kwa nini usiache hiyo kazi na tafuta kazi nyingine ambayo utakuwa na muda.
Kelvin: Ooh! Pole sana inaonekana leo ulikuwa na siku ngumu sana mke wangu!

Mariamu: Yaani siamini nimeshindwa kumpigia simu Shangazi leo!
James: Usihofu atakuelewa, si anajua upo busy.
Kelvin: Ooh Pole sana mke wangu, basi pumzika kisha utampigia muda sio mrefu.

Mariamu: Unajua shangazi ana mapito magumu sana so ananihitaji kuongea naye:
James: Una wasiwasi mno na wewe, kwa nini unajisumbua wakati upo busy na kazi yako.
Kelvin: Pole sana najua leo umechoka, sogea basi nikukumbatie nimekumis sana leo. Baadae umpigie shangazi, hakikisha unawasiliana naye ili umsikilize anaendeleaje na matatizo yake.
(Mariam na Kelvin wanakumbatiana na Mariam ana relax)

NB: Mariam anakasirika na anamwambia James siku zote hunisikilizi na hunijali.
Pia anamwambia Kelvin: "Kila siku napenda sana kuongea na wewe, unanifanya kuwa mtu wa furaha, asante sana kwa kunisikiliza, kunijali na kunishauri najisikia raha kuwa na mume kama wewe Nakupenda sana mume wangu."

Ukweli ni kwamba James alikuwa anasikiliza, lakini kwa lugha ya mwanamke alikuwa hasikilizi kwa kuwa alikuwa anajitahidi kutoa solution kwa yale alikuwa mkewe Mariam anamwambia. Pia alikuwa anaongea kwa ukali fulani na sio kwa Mapenzi.

Kwa upande mwingine, Kelvin alikuwa anasikiliza kwa sababu alikuwa anaongea lugha ambayo mwanamke anaielewa na anaitaka na pia alikuwa anaongea kwa Mapenzi "Kimahaba" alikuwa anampa kile mwanamke anahitaji.

Wanaume wengi huwa hawawasikilizi wenzi wao, sio kwamba wanaziba masikio la hasha bali husikiliza kama ambavyo James alikuwa akisikiliza na anakuwa kama hayuko "concerned" na kile ambacho anaambiwa.

Je, wewe ni James au Kelvin?

Wanaume mbadilike jamani..............

Muwe na week nzuri

Wasalaam

CL




 
Such a useful thread.

Well,

ukisoma vizuri majibu wanayotoa hao wanaume hapo juu utagundua kitu flani kwamba kuna mmoja anajua caring, na mwingine anajua scaring!

simlaumu sana James kwa kutoa majibu horror wala kumpa sifa sana Kelvin kwa kutoa majibu marvelous,

The issue here is, how are you related to the person you are giving feedback to the question? je ulimpenda kweli ndiyo maana ukawa nae? au ulilazimishwa na circumstance ndiyo ukamuweka ndani???

Women need relief from their men, that's true indeed!.... But too much is harmful, remember that!
 
hakuna utam wa hubba kama kusikilizwa na kuliwazwa , caring kwa kweli hawajui tu ila hivi ndo silaha tosha kumueka mwanamke kiganjan mwako. wanawake tunapenda sana kusikilizwa na kubembelezwa
 
mimi ni JAMES ukizidi kunichanganya nashusha windows7 naweka windows 8
 
Kusikilizwa ama kutosikilizwa mwanamke anajitakia mwenyewe, lazima mtu a mark position yake. Kumbuka enzi ambazo EL ni PM, nani alikuwa anasikilizwa zaidi? Hapo alaumiwe nani?

Lakini pia huyu mwanamme yeye hana distractions zingine za maisha? Kwamba kilichobakia maishani mwake ni kum attend mkewe tu? Kuna siku za makavu na siku za kubembeleza. Ukibembeleza deile unakuwa Bus.hoke, kila kitu kwa kiasi.

Kelvin, sounds too fake for me, especially nikiwaza iwe January to December, James naye too rude kama ni January to December. Lazima kuwe na na ka balansi.
 
Aaaah wanawake bwana akili zao wanazijua wenyewe. Ukianza kuhangaika kujifunza kuhusu hawa nguvu ni sawa na kusomea bachelor degreenyingine tu. Mimi ni james na pia ni kelvin itategemea tu na mm maruhani yangu yameamkia wapi.

We are martians and they are from venus..Period. Hamna kuhangaika
 
mimi ni JAMES ukizidi kunichanganya nashusha windows7 naweka windows 8

ukibadilisha sana window mwisho wa siku mashine inaharibika! kila siku zinakuja mpya mara window8, mara window dark light na nyingine nyingi .........

Grand PA
 
Kuweza kuwasoma wanawake wanataka nini ni kazi ngumu sana.....
 
Ukitaka kufanya kila anachotaka mwanamke kufanyiwa lazima ujitoe ufahamu kidogo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom