Mwanamke kumtongoza mwanaume na tamaduni za Kiafrika

Mi sioni tatizo. Kwani wao mbona huwa tunawatongoza na wakati mwingine wanatukataa. Hiyo ni process ya kutafuta hata kama akikataliwa. Je wale unaowatongoza huwa una imani kwamba wanakupenda kweli ma si baada ya ushawishi wa aina mbalimbali. Labda huyu aliye kuwa na courage ya kukutamkia anaweza kuwa ndiye mwenye upendo wa kweli
Tatizo lao wakikataliwa wanajenga bifu..mi huwa siwaelewi!!
 
Hebu tusikie toka kwenu wanaume unajiskiaje mwanamke anapokutongoza labda?
Ni raha sana na hasa kama anakidhi vigezo vyangu. Ni dalili ya mwanamke anayejiamini, anayejua anataka nini. Kati ya sifa ninazopenda mwanamke awe nazo.
 
Kwa Mila na Desturi za kiafrika si sahihi kwa Mwanamke kumtongoza Mwanamume............ingawa wakati fulani fulani Mali, cheo, Mipango mahususi huwafanya wanawake kutongoza wanaume na ni mara chache sana nje ya sababu hizo hapo juu mwananke kumtongoza mwanamume na ikitokea hivyo basi juwa ya kuwa mapenzi yake yapo chini ya ''Dawati'' la moyo wake...........kwani Wanawake wakipenda wana mapenzi sana kuliko wanaume.........!!!!!!
 
Mara nyingi katika maisha ya kawaida wanawake ndiyo "hutongoza"

Kutongoza kwenyewe sio kutamka waziwazi lakini, mwanamke akimpenda mwanaume humtongoza kwa kumuonyesha ishara fulani fulani ili mwanaume huyo alianzishe.

Tatizo ni kwqmba, ni wanaume wachache sana wenye uwezo wa kusoma alama za nyakati na kufanya kweli.

Mwanamke atakuchangamkia kila wakati, atatafuta fursa ya kuonana kila wakati, atajipitisha maeneo ambayo ana uhakika unapatikana na vitu kama hivyo. Huko ndiyo kutongoza kwenyewe!!! Kinachobaki ni mwanaume kujifanya anaanza yeye!
 
Back
Top Bottom