Mwanamke kukuwekea watu wakuchunguze

Kapepo

JF-Expert Member
Aug 14, 2015
1,063
1,188
Habari jf , nina mwanamke simuelewi hata kidogo amekuwa na wivu kupitiliza imefika hatua kablock watu wote nilikuwa nao karibu kama friends tu wakawaida, akaona haitoshi kanikataza nisiwe karibu na hao wanawake wengine kwani anajisikia vibaya sana akiona hayo sasa hivi karibuni ameniwekea watu wanichunguze kila nalofanya yeye akiwa hayupo na kuwalipa wamtumie pucha ikiwa nimekaa na msichana au nacheat kumbuka huyu mwanamke nipo nae ofisi moja tunafanya kazi lkn amekuwa mkorofi mno hata sielewi kwann yupo hivi kwann anafanya haya nimekuwa mtu wa kuomba msamaha kilasiku sasa sijui haya yote anafanya yann naombeni ushauri.
 
Mwanaume huwa haliilii hovyo ,mteme huyo ni mnoko sana
 
Kwanini uishi katika mahusiano yasiyo na furaha?.. mwanaume fanya maamuzi ya kiume
 
Ukimpenda sana mtu huwezi kumpata.Huyo mwanamke anakupenda sana kwa hiyo atakukosa/hatakupata.Ukitaka kumkosa mtu mpende sana.Mimi iliwahi kunitokea mara mbili kuwapenda sana wadada nikawakosa kwa sababu kupenda sana huambatana na wivu wa kijinga ambao huwa ni kero kubwa kwa yule unaempenda na hatimae mahusiano hufa.
 
Hao wanaotumwa ukiwajua kamata piga makofi watarudisha mrejesho kwa aliyewatuma. Na uyo baby mama wako muelekeze kiume namna unataka awe kama haelewi piga chini mzee wangu... Na kama Baba yako mzazi yupo jaribu kumuuliza Mama alikuwa ivi!! Alafu jibu atalokupa mshua ndo utekeleze jamaa!! Wivu kwenye mahusiano ndo mapenzi ila ukizidi ni kero na unaweza hata kuuwa so take care brother
 
Dah

Umenikatisha tamaa kabisa,wewe ni marioo?tuanzie hapo kwanza

Maana tusigekushauri ushauri wa kiume kumbe hela yako ya kula unategemea kwa mwanamke
 
Kama anaujauzito usijali ni mimba inampelekesha ila kama hana basi kua mwanaume

tambua wivu ukizidi ni manjangaa

Sent from my ɪᴩʜᴏɴᴇ 11ᴩʀᴏ using JamiiForums.com mobile app
hapana si mjamzito
 
Dah

Umenikatisha tamaa kabisa,wewe ni marioo?tuanzie hapo kwanza

Maana tusigekushauri ushauri wa kiume kumbe hela yako ya kula unategemea kwa mwanamke
hapana sema kipato kanizidi na pia umri kanizidi ni hayo tu
 
Hao wanaotumwa ukiwajua kamata piga makofi watarudisha mrejesho kwa aliyewatuma. Na uyo baby mama wako muelekeze kiume namna unataka awe kama haelewi piga chini mzee wangu... Na kama Baba yako mzazi yupo jaribu kumuuliza Mama alikuwa ivi!! Alafu jibu atalokupa mshua ndo utekeleze jamaa!! Wivu kwenye mahusiano ndo mapenzi ila ukizidi ni kero na unaweza hata kuuwa so take care brother
shukrani man kwa ushauri
 
mkuu simtegemei chochote kwenye pesa zake sijawahi kula hela yake na sijawah fikiria fanya hayo
Shida sio kumtegemea bro, tatizo ni kwamba yeye tayari anajiona anakumiliki mkuu, na anajihisi yupo juu yako kiutawala(kwa namna ulivyosimulia hapo juu) ! Hapo ni either ukubaliane na hali au uwe mkali sana and usimame kiume ili aanze kukubali kuwa yuko chini yako! Hizo tabia za kumlinda mpenzi wako, kumcontrol e.t.c huwa ni tabia za kiume naturally, ila kama yeye ndo anafanya hayo basi yeye ndo mwanaume kwenye huo uhusiano, simama kiume umrudishe awe na haiba ya kike! Ila sikushauri uachane nae b'coz huku kitaa ni pagumu sana kupata manzi ambaye anakupenda kwa dhati....pambana na mzigo wako mpaka ukae sawa! Huyo anakupenda ila tu anajidai mwanaume kwenye hayo mahusiano yenu
 
Humuwezi huyo, amekuzidi kipato na mamlaka anataka akuzidi yaani akuongoze yeye, mpe msimamo wako Kama mwanaume asipoelewa basi humuwezi....wivu ukizidi Sana kwenye mapenzi kinachofuata ni majanga...
 
Nakupa heko mkuu kwa kupendwa namna hiyo i wish na mimi nikutane na baby kama huyo i swear nita-relax sana
Mjuba since naanza haya mavitu mi ndo napasuka kwa mfuko na kwa moyo
Hawa wanaokwambia piga chini ni wachovu wanataka na wewe uyaoge
TAKE IT mpende zaidi yake utaifurahia miaka yako hapa duniani
 
Wivu haukatazwi ila hiyo ni shida mkuu hapo ni kukimbia tu, wanasema kila kitu kwa kiasi hapo jiandae hata kuwekewa sumu kwa style hiyo.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom