Mwanamke kujitolea mahari je, analazimisha ndoa?

Mwanamke kujitolea mahari je, analazimisha ndoa?

Daudi1

JF-Expert Member
Joined
Dec 14, 2013
Posts
15,838
Reaction score
26,248
Habari ya muda huu wanajamii,leo ni siku njema ya jumapili tumshukuru Mungu Jehova Shama kwa kutuamsha salama kwa walio wagonjwa tuwaombee kwa Mungu awajalie afya njema,kama ilivyodesturi ya jukwaa letu letu pendwa kupeana ushauri,kujadiliana mambo ya kimahusiano yanayotukumba. Baada ya salamu turudi kwenye maada.....

Imekuwa kawaida siku hizi mwanamke kujitolea mahari kwa maana ya kwamba anampa mwanaume pesa za mahali zinazohitajika kwao ili mchumba wake huyo akatoe kwao,inawezekana ni mapenzi na huruma kwa mpenzi wake au kutaka kutetea mahusiano yake yasivunjike eti kwa sababu ya mahari ili hali na yeye ana uwezo. Wengi mtasema mapenzi ni kusaidiana hasa kwa maisha haya ya sayansi na teke linalokujia huwa najiuliza maswali yafuatayo:-

1.Ni kweli mwanaume ambaye kwa dhati anampenda mpenzi wake anashidwa kumtolea mahari?
wengine watasema mahari ni kama mnauziana labda ni kwa mtazamo tofauti ila ninachojua mahari huchukulia kama zawadi kwa mwanamke na ni heshima kwake kwa tamaduni za kiafrika,na hakuna mwanamke asiyependa heshima hiyo labda tu anapoingiza tamaduni za nje kujifariji.

2.Mwanaume anasifika kwa majukumu juu ya mke wake na familia yake sasa endapo mwanamke atajitolea mahari hapo kutakuwa na uwajibikaji ndani ya familia?

3.Kitendo cha Mwanamke kujitolea mahari je anakuwa analazimisha ndoa au ndo mapenzi yanakuwa yamemzidia kiasi kwamba hayo mengine hayaoni? ndoa nyingi zinavunjika na katika kuvunjika kunakuwa na maneno ya maudhi ilimradi kila mmoja kumkera mwenzake,inakuwaje pale mwanamke anaachika na huku fika akijua hata mahari alijilipia?

Karibuni kwa michango, wewe suala la mwanamke kujitolea mahari unalionaje kwa mtazamo wako hoja ndiyo za msingi kuliko mengine yote.
*************************************
Karibuni
​
 
Dada yangu alijitolea mahari, alimuokota masikini fulani wa kisukuma, wakapendana hadi basi.

Dada alikuwa na kazi bomba, msukuma anakaa home tu na kupiga misheni town zisizo na kichwa wala miguu.

Waliokotana sijui wapi wakaletana home kupangiwa mahari wakaanza kupaniki, sister akajidai hataki kulipiwa mahari. Wajomba wakakomaa, mahari lazima iletwe.

Dada alikuwa na haraka ya kuolewa, akaingia benki akatoa Milioni 1 yake akampa huyo msukuma alete home.

Hata hvyo huyo msukuma sasa hivi ni kupiga misheni town tu, Dada ndo anasimamia show zote pale kwake.

MAPENZI UPOFU NAKWAMBIA
 
Nyie ndo badae mnakua mabushoke...inabidi hata kwenye kugegedana inabid wewe utangulie chin yeye juu maana kakulipia ha ha haa...loading error....
 
Mwanamke hawezi kujitolea mahari! Sasa yeye si ndio atakuwa amejioa? Na atakuwa na maamuzi ya kuiendesha ndoa atakavyo?? Usije ukakubali kutolewa mahari hata na nduguyo? Watakuingila kwny maisha yako ya ndoa na utakuwa huna nguvu
Ila kama mwanamke anajua hali yako sio nzuri na una nia ya dhati ya kumuoa yeye anatakiwa awakonvis ndugu zake wakupangie mahari iliyo ndogo! Hilo liko ndan ya uwezo wake na sio kukutolea mahari
 
Aiseee kwa hiyo Dada alikuwa na haraka ya Kuolewa
 
Nyie ndo badae mnakua mabushoke...inabidi hata kwenye kugegedana inabid wewe utangulie chin yeye juu maana kakulipia ha ha haa...loading error....
Hiyo ni moja ya staili za kugegedana na haina mahusiano yoyote na suala la mahari,wewe unafikiri ubushoke unatokana na mwanamke kujilipia mahari? aliyelipiwa hawezi kumfanya mume wake bushoke?
 
Ni kawaida siku hizi? Mi ndo nasikia leo
 
Mwanamke hawezi kujitolea mahari! Sasa yeye si ndio atakuwa amejioa? Na atakuwa na maamuzi ya kuiendesha ndoa atakavyo?? Usije ukakubali kutolewa mahari hata na nduguyo? Watakuingila kwny maisha yako ya ndoa na utakuwa huna nguvu
Ila kama mwanamke anajua hali yako sio nzuri na una nia ya dhati ya kumuoa yeye anatakiwa awakonvis ndugu zake wakupangie mahari iliyo ndogo! Hilo liko ndan ya uwezo wake na sio kukutolea mahari
Umeongea kitu cha msingi sana kumbe anatakiwa awaombe wazazi wake wapunguze kulingana na uwezo wa mpenzi wake na si kujitolea mwenyewe.
 
yaani mimi lazima nitolewe mahari tena ngombe kazaa allaaaa

NADUMISHA MILA ILA WENGINE ISHASHINDWA MI MASAI BWANA
 
Ni kawaida siku hizi? Mi ndo nasikia leo
Siku hizi ni kawaida hasa kwa wanawake wasomi wenye kazi zao,kuna mdau hapo juu katoa ushuhuda kwa dada yake
 
yaani mimi lazima nitolewe mahari tena ngombe kazaa allaaaa

NADUMISHA MILA ILA WENGINE ISHASHINDWA MI MASAI BWANA
Je kwa wanaojitolea mahari kimtazamo unalionaje hilo?
 
Mimi nataka kujua nini maana ya mahari, nini umuhimu wake, je mahari ni lazima?
 
Mimi nataka kujua nini maana ya mahari, nini umuhimu wake, je mahari ni lazima?
Kwa ninavyojua mimi mahari ni vitu anavyotoa mwaume wakati wa kumuoa mwanamke inaweza kuwa pesa(kwa siku hizi),ng'ombe na vitu vingine vya thamani kama zawadi kwa mwanamke na familia yake,umuhimu wa mahari unaunganisha familia mbili zinakuwa na furaha na upendo juu ya ndoa hiyo,pia inaleta heshima na thamani kwa mwanamke husika,na kwa tamaduni za kiafrika ukitaka kuoa mali ni lazima
 
Wadada wa miaka hii wanajifaragua sana na wanapenda kila kitu kiende kama anavyofikilia kwenye ubongo wake nakiwe kwa haraka kama uyoga.
Akiwashawaza kuolewa tu ilimladi ana mchumba labda ajajiandaa au uwezo hana yeye mwanamke atafanya kila njia ikiwemo kumpa mahali jamaa ili wafunge ndoa. Chakustahajabisha baada ya siku kadhaa mwanamke anapotakiwa kubeba majukumu ya ndoa kama mama basi anaona jamaa anamuharasi ukizingatia mahali katoa mwenyewe hapo ndio mifarakano inapoanza au labda dume uwe bushoke.
Ila hii kiuwalisia si sawa kwasababu mwanamke ni kiumbe dhaifu na unaweza ukamkwaza kidogo tu akazungumza maneno sio toka alivyokutolea mahali kwao na anavyokutunza.
 
Vipi kwa wewe mwanaume mwanamke akikuambia kama ni mahari nitakutolea hilo unalichukuliaje?
 
anampenda sana ila kijana hana uwezo wa kulipa mahari kwaio hapo hakuna tatizo jaman au nyie mnaonaje
 
anampenda sana ila kijana hana uwezo wa kulipa mahari kwaio hapo hakuna tatizo jaman au nyie mnaonaje
Kama hana uwezo wa kumlipia mahari vipi kuhusu majukumu ya ndani amabayo ni zaidi ya hiyo mahari utaendelea kutoa kama mwanamke?
 
Umeongea kitu cha msingi sana kumbe anatakiwa awaombe wazazi wake wapunguze kulingana na uwezo wa mpenzi wake na si kujitolea mwenyewe.

Kabisa, ingawa ni ngumu lakini kwa msisitizo na msaada wa maza wake wanaweza wakonvis wazee wamuelewe na wapunguze mahari
 
Back
Top Bottom