Emc2
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 16,808
- 16,951
Nawasalimia wana JF
Stori ya kweli
Kuna rafiki yangu (Mimi mwanaume na yeye pia) nimesoma naye shule ya msingi tume kuwa karibu nae sana.
Sasa mambo yenyewe ni kama ifuatavyo:-
Alinieleza walikutana na msichana na akatokea kumpenda, basi akaomba no ya simu na yule msichana akampa.
Basi walianza mawasiliano ya hapa na pale. Baada ya mda alimuuliza huyo msichana kama yuko na mtu, msichana akasema yuko pekee yake (Single). Basi jamaa akatupa karata yake.
Yule msichana akasema yeye ameokoka na anapenda kuenenda katika mapenzi ya kimungu.
Basi rafiki yangu alifurahi sana kukutana na huyo binti, akauliza wapi anakosali, bila kusita msichana akaeleza anasali wapi.
Jumapili moja jamaa yangu akaibukia kanisani na kuona kweli anasali pale, akamtamburisha kwa baadhi ya ndugu zake.
Baada ya muda fulani yule binti akaaza kuwa anaomba pesa. Ok bila kusita jamaa akawa anampa hizo pesa (mara anataka kusuka, anataka kununua viatu, hela ya chakula cha mchana na mengine). "Huyu dada amesoma na ana digrii pia anafanya kazi"
Baada ya muda huyo msichana akaanza kubadilika, walikua wanawasiliana WhatsApp msichana akawa hatoi ushirikiano.
Baada ya muda fulani msichana akablock namba ya huyu rafiki yangu kwa hiyo akawa hawezi tena kuwasiliana naye kwenye simu. Ila alikuwa na simu nyingine akipiga haipokelewi.
Jamaa akawa haelewi nini tatizo, akajaribu kuongea na dada yake, dada yake akasema hatayeye hajui. Basi akajaribu kumuomba waonane waongee, yaani hakutaka kabisa kuonana nae.
Basi siku moja msichana akapiga akasema "Sitaki mawasiliano na wewe". Heee jamaa haelewi nini tatizo.
Baada ya siku moja akapigiwa na mwanaume akisema mimi ndie mpenzi wa huyu msichana mbona unamsumbua.
Kwa kufupisha stori jamaa ameamua arudishiwe pesa zake. Na kwakua msichana hataki kuonana nae, jamaa katinga kwa wazazi wa msichana(Ni wacha Mungu) wameahidi watamrudishia.
Hivi kweli ni sahihi alichofanya huyu jamaa yangu?
Nawasilisha hoja.