Jing chu
JF-Expert Member
- May 9, 2019
- 385
- 592
Wakuu bila shaka mnamalizia weekend vyema kabisa, kwangu haijaenda vizuri kwa sababu ya hili nalolileta kwenu tusaidiane mawazo wana nzego wenzangu!
Issue iko hivi, serious nampenda huyu binti naekaa nae (mke) lakini nachokiona kwa sasa ni mapicha picha. Siku 4 nyuma tulipata mgeni ambae kiuhalisia ni mtoto mdogo niliezaa zamani zile na mwanamke mwingine lakini wakati naanza kumtongoza huyu wa sasa nilimwambia kila kitu na kuna kipindi alikuwa anaongea nae kwa simu.
Mapema kabla hatujaanza kuishi nae nikamwambia nataka kumleta mwanangu aje asomee huku niliko, kiukweli alinishauri sana nitafute vyumba 2 au chumba na sebule nikaona ni wazo zuri, nikafanya hivo, akasema sasa mlete mtoto. Nikamuuliza bado ni bachela je nitaweza kukaa nae ? Maana mm nilitaka niweke mtu wa kulipwa awe anamhudumia wakati wa asubuhi hadi napotoka job saa 9 akasema hapana niko tayari mlete tutakaa tu.
Kabla sijamleta tumekaa nae huyu Dada miezi 5 Mara zote akidai nimlete mtoto lakini tangu mtoto afike siku 4 hadi leo kabadilika yuko kimya anapika anatenga msosi yeye anakuja kula baadae ! Nimemuuliza sana shida nini anasema hakuna tatizo hadi nimeamua kuwa cool simuulizi tena!
All in all yeye hajapata mtoto bado wala hajawahi kuzaa!
Sasa wakuu hili limekaaje,msaada please. Nifanyeje?