Mwanamke kama huyu nichukue maamuzi gani?

Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
319
500
Wakuu bila shaka mnamalizia weekend vyema kabisa, kwangu haijaenda vizuri kwa sababu ya hili nalolileta kwenu tusaidiane mawazo wana nzego wenzangu!

Issue iko hivi, serious nampenda huyu binti naekaa nae (mke) lakini nachokiona kwa sasa ni mapicha picha. Siku 4 nyuma tulipata mgeni ambae kiuhalisia ni mtoto mdogo niliezaa zamani zile na mwanamke mwingine lakini wakati naanza kumtongoza huyu wa sasa nilimwambia kila kitu na kuna kipindi alikuwa anaongea nae kwa simu.

Mapema kabla hatujaanza kuishi nae nikamwambia nataka kumleta mwanangu aje asomee huku niliko, kiukweli alinishauri sana nitafute vyumba 2 au chumba na sebule nikaona ni wazo zuri, nikafanya hivo, akasema sasa mlete mtoto. Nikamuuliza bado ni bachela je nitaweza kukaa nae ? Maana mm nilitaka niweke mtu wa kulipwa awe anamhudumia wakati wa asubuhi hadi napotoka job saa 9 akasema hapana niko tayari mlete tutakaa tu.

Kabla sijamleta tumekaa nae huyu Dada miezi 5 Mara zote akidai nimlete mtoto lakini tangu mtoto afike siku 4 hadi leo kabadilika yuko kimya anapika anatenga msosi yeye anakuja kula baadae ! Nimemuuliza sana shida nini anasema hakuna tatizo hadi nimeamua kuwa cool simuulizi tena!

All in all yeye hajapata mtoto bado wala hajawahi kuzaa!

Sasa wakuu hili limekaaje,msaada please. Nifanyeje?
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,552
2,000
Una kitu gani cha maana zaidi ya kumjaza tu wazungu huyo mkeo? Sababu ya kukuambia hili ni kuwa; Elewa kuwa huyo mwanamke hatoweza kutulia bila kumpata naye mtoto wake. Alitaka tu kuhakikisha kuwa umemleta amuone ka mnafanana kweli isijekuwa umebebeshwa zigo. Muda woote umekaa naye hata mate hatemi ilikuwaje uliweza kwa huyo mwanamke mwingine kwake hujaweza? Uwe macho, asije wamalizeni weye na hicho kitoto chako
 
Duuuh hatari sana hii, kiukweli mkuu anahangaikia PID treatment na amemaliza dozi juzi tu na mm ndo nilimwambia nenda hospital ucheki mana mbona sikujazi ? Hivo kaambiwa baada ya dozi ndani ya miezi 2 anaweza pata mimba kwani kwenye uzazi hana shida.
 
Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
319
500
Mkuu, hapo minaona tatizo ni wewe.
Na huyo mkeo anakujaribu tu, maana mtoto mwenyewe ni mmoja. Sasa wangekua kama mimi (watoto wangu), sindio angefungasha na virago kabisa....
Ebu acha kulea ujinga mkuu, be like a man
Nifanyeje mkuu! Nisaidie wazo
 
Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,479
2,000
Kuwa mpolee akizaa atajua uchungu wa mwana, but pia kulea mtoto wa mwenzio n kazi na yahitaji moyo kwa kweli, lakin na wee why hukumuoa huyo uliye zaa nae? Aaaaaah
Mimi kama baba siwezi kulea manyanyaso kwa wanangu aiseeee.....
Na sio kila wanawake tunao zaa nao lazima tufike kwenye ndoa, wakati mwingine tunajikuta tumezaa tukiwa kwenye tuisheni...
Bado nasisitiza mleta mada asimame kwenye nyumba Kama mwanaume, hii issue minaona ni ndogo sana
 
mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,552
2,000
Duuuh hatari sana hii, kiukweli mkuu anahangaikia PID treatment na amemaliza dozi juzi tu na mm ndo nilimwambia nenda hospital ucheki mana mbona sikujazi ? Hivo kaambiwa baada ya dozi ndani ya miezi 2 anaweza pata mimba kwani kwenye uzazi hana shida.
Jichunge sana kwani usalama wenyu sio kamili. Hakuna mwanamke mwenye wivu ka aliyekosa mtoto wake mwenyewe
 
Hendisamu

JF-Expert Member
May 9, 2019
319
500
Mimi kama baba siwezi kulea manyanyaso kwa wanangu aiseeee.....
Na sio kila wanawake tunao zaa nao lazima tufike kwenye ndoa, wakati mwingine tunajikuta tumezaa tukiwa kwenye tuisheni...
Bado nasisitiza mleta mada asimame kwenye nyumba Kama mwanaume, hii issue minaona ni ndogo sana
Nipe pa kuanzia mkuu !
 
Ushimen

JF-Expert Member
Oct 24, 2012
28,479
2,000
Una kitu gani cha maana zaidi ya kumjaza tu wazungu huyo mkeo? Sababu ya kukuambia hili ni kuwa; Elewa kuwa huyo mwanamke hatoweza kutulia bila kumpata naye mtoto wake. Alitaka tu kuhakikisha kuwa umemleta amuone ka mnafanana kweli isijekuwa umebebeshwa zigo. Muda woote umekaa naye hata mate hatemi ilikuwaje uliweza kwa huyo mwanamke mwingine kwake hujaweza? Uwe macho, asije wamalizeni weye na hicho kitoto chako
Rubish...
You're out of the point niga...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom