Mwanamke huyu ananifaa?

Judgement

JF-Expert Member
Nov 13, 2011
10,327
4,779
Ninachokisema hapa ni serious na naomba comments also seriously! Nina mpenzi wangu nampenda kw dhati, kadhalika kiasi flani nashawishika kuamini nae ananipenda kufatana na mambo flaniflani niyaonayo kwake, moja kubwa linalonifanya nizidikua nae krb ni vl ambavyo amekua si tegemezi kwangu, kwani ameajiriwa. Mimi humpa fund kama za vocha pale ninapojisikia na mara chache hutokea akaniomba pesa au kitu, hatuishi nyumba moja yeye anaishi kwao nami kwangu. TATIZO LANGU NI HILI :- Bibie huyu ni mlevi japo si mlevi (cha pombe) aliepindukia laa, lakini ieleweke kwmb yeye ni mnywaji wkt mimi situmii pombe, nilikua mnywaji lakini takriban nina miaka mitano hv tangu nimeacha pombe, hivyo ndiyo kusema mazingira yote ya ulevini nayajua! Binti huyu ana mashosti wake wawili ambao ndy mara kw mara anakunywa nao, mmoja kt ya hao rafikize tabia zake c nzuri anabadili mabwana km hana akili nzr! Nimejaribu mara kadhaa kumnasihi kwanza aachane na ulevi ambao utampelekea pia kutengana na group la marafiki wale japokua yule rafiki yake wa pili hadi hv cjafanikiwa kujua tabia zake nje ya ulevi. Kinachonikwaza ni pale napokua mi niko hom kitandani natafuta usingizi yawezakua mida ya saa 5- 6 -7 usiku nikimpigia akipokea tu nasikia sauti ama ya Tv au muziki mkubwa ambapo kwao anapoishi hakuna umeme! Nikimwuuliza uko wp? Jibu niko Bar. Kesho yake tukionana nikianza kumlamikia kwmb mimi sipendelei yeye kua klabu hadi mida hiyo na uwezekano wa kupata mwanaume kiulevi unakua mkubwa, yeye hunijibu kw kujiamini kwmb ana uhakika anai'control pombe na hawezi toka na mwanaume. Aidha sijawahi kumfumania lakini je? Mwanamke huyu ananifaa niendelee kua nae?
 
Mh! Ngoja tusubiri wenye expr za couples mmoja anakunywa mwingine hanywi espclly mwanamke ni mtumiaji, mwanaume c mtumiaji wa kilevi
 
ndugu angu hapa hamna kitu....watu kubadili tabia ni mpaka atake mwenyewe na kama wewe hupendi mnyaji basi huyu sio wakukaa nae maana itafika sehemu atana wewe unamboa tuu. mwenzio anataka toka akanywe wewe wataka kukaa ndani.
bora ujiachie mapema tuu...mna interests tofauti!!!!
 
Binafsi Siwapendi Wanawake wanaokunywa pombe, sasa huyo anayekunywa bar mpaka usiku wa manane naona anapoteza sifa za mke mwema. Inatakiwa mkae mzungumze mkubaliane kuhusu tabia unazopenda kama hamtakubaliana ni bora utafute mwingine.
 
Jiandae kumfungulia mlango evi 9t. km anakuomba hela ata bia pia akienda baa anaomba!
 
mi nafikir kaen muongee, pombe anaweza kuacha ama kupunguza km ulivyofanya ww, weken mikakat yenu pamoja mtaenda mbal na kufurahia mahusiano yenu.
 
We mwambie upunguze au asinywe tena. Maanake mtu akishalewa hata kuji-control inakuwa ngumu kidogo. Mpe ukweli kuwa hupendi hiyo tabia. Asikubali au kubadilika achana naye.
 
Ulishawai kukaa nane na kumweleza kuwa unapenda mwanamke wa aina gani? au hupendi mwanamke wa aina gani, ukiwa kama mwaname lazima uwe na msimamo wako tena ukiangalia labda unamwandaa kuja kuwa mke Badae sasa kama hujawai kumwambia msimamo wako huu ndio wkt wake na kama hawezi badilika ni bora ujiepushe mapema
 
Mapenzi ni ujinga sana...we anza kunywa pombe tena utaona ka yeye hajaanza kukushauri kua hapendi...siku zote mapenzi kama hayo ni nani anampenda mwenzie zaidi ndio ataonewa zaidi...we mpotezee jifanye kama haujali utaona anavyojirudi
 
mnh...................hebu niandae essay ya page ka 18 hivi then ntarudi kuipost hapa ukiisoma utaielwa
 
The "Law of Attraction" inasema "like attract like" kama mpenzi wako anakunywa pombe bar basi ni uhakika kiuhalisia hatokuwa na tofauti na mwanamke mwengine yoyote wa mazingira ya baa nadhani umenielewa, ingawa ataficha na kutokuonyesha mbele yako traits zozote za mwanamke wa baa lakini huo ndio unabaki ukweli.

"The birds of same feather flock together" tabia za binaadamu zinaamuliwa na kuendeshwa na subconscious mind kwa maana ya kuwa mlevi rafiki yake ni mlevi na tabia na vitendo vyake vinakuwa ni sawa na mlevi mwenzake, kwa hio usidanganyike ukasema huyu anakunywa tu baa na rafiki zake wako dizaini hii ambayo siipendi lakini yeye hayuko hivo. Hakuna kitu kama hicho.
 
Ulishawai kukaa nane na kumweleza kuwa unapenda mwanamke wa aina gani? au hupendi mwanamke wa aina gani, ukiwa kama mwaname lazima uwe na msimamo wako tena ukiangalia labda unamwandaa kuja kuwa mke Badae sasa kama hujawai kumwambia msimamo wako huu ndio wkt wake na kama hawezi badilika ni bora ujiepushe mapema
Nilikwisha mpa protocal zangu zote kama nilivyokwisha eleza na mara kadhaa jibu anipalo ni "wiki hii hii naacha pombe" akipumzika wiki 1 inayofata anarudi kwenye pitch!
 
Wadau! Mkerejea mwanzoni mwa thread nilisisitiza hii maneno ni seriously! Na mlionijali na mkatumia muda wenu, vidole vyenu kubonyeza burton kuandika, nami sitokua hayawani kutokuwapa asante kw majina nitumie style mjengoni na ninahifadhi michango yenu kwenye hansard! NDU/MAYAYA, MZABZAB, LIKWANDA, IDD, NDECHUMIA, CTV KILAZA, BADILI TABIA, KWELI, SHAMTE, RAYMOND 2500, UNDUGUKAZI, MIKATABAFEKI. Nawashukuruni sana, ningeweza kutoa shukrani za jumla, lakini kwa umuhimu wa issue husika nimetumia style hii, NAWASHUKURUNI.
 
mnh...................hebu niandae essay ya page ka 18 hivi then ntarudi kuipost hapa ukiisoma utaielwa
Naisubiri kwa hamu kiongozi, usinisahau, nikiona umepitiwa ntakusaka hata kwenye majukwaa mengine!
 
Nina Expirience Sana Ndugu yangu ngoja nikwambie huyo Mwanamke anaishi kwa kutumia Pesa za Wanaume kwa Asilimia Kubwa Jaribu Kumwingizia maneno ya Mungu zaidi yanaweza kupunguza pombe kwake na kuhusu hao Marafiki usijidanganye Kaka na wala wasikusumbue bali wewe Tumia Muda Mwingi kuwa na huyo dada na awe anajielezea muda mwingi,Tabia yako ya kuonesha unamjali mi nimeipenda Sana tena nzuri,mi naamini atabadilika.
 
Kama hatoacha pombe ki ukweli hatokufaa.Mkae nae kama kamati ili akupe jawabu lililonyooka ni lini mwisho wa pombe zake,vinginevyo muwekee dead line!aAkishindwa kuacha basi uhesabu kwamba haikuandikwa muwe pamoja.
 
Back
Top Bottom