Nivea
JF-Expert Member
- May 21, 2012
- 7,460
- 4,771
Mtambuzi nielewe hivi im incharge of my own life sio dini ,sio mchungaji ,sio shekhe ,sio jamii .mimi binafsi niko incharge ,nikipigwa ndani nakuumizwa na mume wa ndoa ,ninae umia ni mimi wao watanipa pole ,hakuna atakayeweza kuniambia ondoka never ever sasa basi mimi huwa sijali kabisa eti dini itanionaje ???nimefunga ndoa kanisani lakini siamini kama ni kitu kinaweza tie freedom ya maisha na amani ya moyo wangu ,n\ikinishinda naacha Mtambuzi.eti nina watoto ndio nife,jamii itanionaje ndio niteseke hizo jamii,dini,wazazi nk nimewajua nikiwa na akili timamu na nimewajua ukubwani mimi hawanipi shida .nasimamia kile ninachokiamini mpaka nife nikicheka sio roho kukakamaa.nakubaliana na wewe kuwa maisha ya ndoa ni kama bahari labda niseme, maji kupwa maji kujaa, mawimbi na wakati mwingine shwari... Sawa?
Lakini hebu tuseme ndoa imekushinda, yaani ni kwamba bahari imechafuka kiasi cha kuleta gharika, imeacha majeraha makubwa moyoni na hata mwilini na pia imeharibu mazingira yenyewe ya ndoa kiasi kwamba kurekebisha hali hiyo ni ngumu kumeza.
Hapo nakubaliana na wewe juu ya kauli yako hii:
"itakapotokea ndoa imekushinda give up.mimi nasema kuwa sintaupa moyo wangu hata sekunde kusikitika juu ya maamuzi ntakayofanya .nilizaliwa mwenyewe,ntazikwa mwenyewe,iam incharge of my own life ,nikifa ndoa imeishia hapo so ya nini kuitesekea..."
lakini je dini zinasemaje kukusu kuachana?
Je jamii inamchukuliaje mwanamke anayeitelekeza ndoa yake na kujitoa?
Je ndugu na marafiki wana mtazamo gani kuhusu jambo hilo?
Je mwanamke yuko tajari kukabiliana na hali hiyo? Yaani mashinikizo kutoka katika dini, jamii na labda ndugu na marafiki....
Hebu nipe uzoefu wako dada yangu kabla ya kikao chetu cha kahawa leo kujadili business proposal.... Lol
Last edited by a moderator: