ndoa pia ina majira km yalivyo majira ya mwaka. kuna kipupwe, masika na kiangazi. sasa inategemea wewe majira yako yamemudu kwa muda gani, wakati mwingine unaweza kuingia kwenye ndoa ukakumbana na raha, raha, raha! ukadumu ktk kipindi cha rara maybe kwa miaka mitano. kikaja kipindi cha matatizo, karaha na mengine mengi, sasa hapo ndo pagumu kwani unatakiwa kuwa na uvumilivu wa hali ya juu! kwn huwezijua utadumu kwa muda gani na hali km hii. tena inaweza kuzidi miaka ya amani. so mi nafikiri ndoa ni watu wawili, kila moja hakushauriwa kuunganisha hisia zenu ni mioyo yenu imeamua. na itakapofikia mwisho moyo wako pia ukwambie toka. ikumbukwe kuwa kuna tabia za kuvumilika na zisizo vumilika, i mean tabia za asili binadamu tunazo ambazo ni ngumu kubadilika. sasa hapo ndipo inafikia mtu ku give up. ifike mahala enough is enough.