Mwanamke hebu funguka uko upande upi...?

Mwanamke hebu funguka uko upande upi...?

couple.jpg


Mara nyingi nimekuwa nikikutana na wanawake walio katika ndoa ambao hujuta sana na kusema kwamba wanajuta kuolewa na laiti wangejua kwamba maisha ya ndoa yako namna hiyo, katu wasingeolewa na wakati mwingine hukumbuka maisha yao kabla ya kuolewa jinsi yalivyokuwa mazuri na ya amani kuliko ilivyo sasa baada ya kuolewa

pretty-woman-hair.png


Lakini pia nimekuwa nikikutana na wadada walio single ambao wanayatamani sana maisha ya ndoa. Umri umekwenda na wamekata tamaa na wanatamani hata ajitokeze mwanaume yeyote yule amtamkie kumuoa ili mradi tu na yeye aingie katika orodha ya wanandoa.

18.jpg


Jambo hili limekuwa likinitatiza sana.
Walio ndani wanatamani kutoka na walio nje wanatamani kuingia. Je hii taasisi ya ndoa mbona imekuwa kizungumkuti hivi?

Naomba wanawake mnipe uzoefu wenu katika jambo hili....
Ndoa ni institution nzuri Kama unampenda mwenzako na ukiwa na low expectation .Ukiingia kwa high expectation Za Mumeo stress .Be happy ,smile ,life is too short .Usiogope
 
Ndoa ina umuhimu wake. Na kinachonifanya niamini hivo ni:
Kuna waliotoka, wanatamani kurudi tena, hiki nikipimo tosha kinachoonesha kuwa kuna madini yanapatikana ndani ya ndoa.
 
Neylu wacha ndoto za mchana. Huwezi kuwa na furaha wakati wewe ni kapelo. Halafu hebu ongeeni kiswahili tu humu mhona mnachafua lugha za wenzenu hivo!! Kipi kimepungua kwenu . Elimu ? Au nidhamu na adabu!?.
Mungu ameumba adam na eve. Sio mmoja! Sasa tafuta baba mmoja maridadi akuonyesha ulichokuwa hujakipata muda mrefuu. Utajuta kwa nini ulichelewa
 
Mtambuzi, natamani kuzungumza kitu, ila kwa kuwa ungependa kuwasikia wadada, haya acha niwe msomaji kwa leo!!!
 
Last edited by a moderator:
Ukitaka tamu ya ndoa tuulizeni WATANGA....
Huku waume twakoshwa na vifuu
Twasuguliwa na machicha ya nazi
Twakandwa na mafuta ya nazi
Halafu twakoshwa na maji ya hiriki
Hiyo ni kabla ya korodani kuoshwa kwenye kisosa
Kabla ya kubebwa kurudishwa chumbani
 
Haha thats true gal watazame wanawake wengi walioko kwenye ndoa ama wanaolilia hizo ndoa most of them wako average in many things
Si kweli, kuwa wanataka ndoa ni average women. Wapo wengi successful and excellent wish to enjoy marriage. What i know, once in life a woman dream marriage, once the dream disappear the cause is life experience.
 
Ingawaje huwa nakwazwa lakini sio kiasi cha kutaka kutoka looh ndoa ina raha yake bwana, najaribu kuwaza ningekuwa sijaolewa ingekuwaje, labda ningezaa na mume wa mtu ...halafu inakuwaje ukikaa nae anakwambia ngoja niwahi kwa wife, halafu nanuna au? Aaa hapana imekaa vibaya kwangu. Sitamani kutoka jamani.....na mnaotaka kuja njooni tu..
Ameen and Ameen! Walahi ndoa ina raha yake ati! Kero zipo hata kwa ma BF na Mahawara - chako ni chako.com
 
Jamani hili suala tumeshalizungumzia mara kadhaa hapa jamvini, tatizo hapa linaanzia enzi za uchumba,wachumba wengi wanakuwa na matarajio makubwa sana,mwisho wa siku akiingia kwenye ndoa anakuta mambo yapo tofauti kabisa na hili lipo zaidi kwa dada zetu ndio maana utakuta wao ndo victims wa jambo hili.
Kusema ukweli hata maisha ya kisela nayo yana changamoto zake hebu jaribuni kuvuta hisia,wahuni wanagombea mwanamke saa nane za usiku, ilhali we umejilalia na mkeo kimyaaa !!
 
Ukitaka kujua utamu wa ngoma shariti uingie uwanjani na uicheze,.
 
unajua mkanganyiko unatokana na kutokuelewana au kutokulandana kunakotokea kati ya walio ndani ya ndoa kukosa usuluhishi sahihi ambao utaruisha maelewano hayo. Pia kaka mtambuzi upweke ni dunia nzito ambayo si rahisi wala nzuri mtu kutembea, na kuna umri flan mtu huwa anahitaji mwenza, ndio inapotokea dhana ya walio nje wanataman kuingia ndan.
 
Natamani sana siku moja nioe, nami niitwe mume nami niite mke, sina matarajio makubwa kwenye ndoa yangu.......just anifulie nguo zangu, anipikie chakula, afanye usafi nyumbani, anipe pale kati, niishi kwa peace.....bhaaaaaaaaaaassssssss sihitaji kingine zaidi!!!!!
Mkuu theChance,
Kwa hayo mahitaji yako mkuu itakuwa unatafuta Housemaid na sio Mke. Usiingie gharama ya Ndoa mkuu, tafuta tu Maid tena wale wa kuja na kuondoka jioni ili kupunguza gharama zaidi. Nina uhakika anaweza kukupa pale kati na ukaishi kwa Amani kabisaa. Bhaaaaaaaaassssssssss.
 
Mkuu theChance,
Kwa hayo mahitaji yako mkuu itakuwa unatafuta Housemaid na sio Mke. Usiingie gharama ya Ndoa mkuu, tafuta tu Maid tena wale wa kuja na kuondoka jioni ili kupunguza gharama zaidi. Nina uhakika anaweza kukupa pale kati na ukaishi kwa Amani kabisaa. Bhaaaaaaaaassssssssss.

Soma tena uzi mkuu......natamani siku moja nioe, niitwe mume, nami niite mke ...................
 
Mkuu kama unaweka katika mizania wanawake ndio hujuta zaidi katika jambo hilo...
Kwa kawaida wanaume walio wengi shabaha yao dhaifu kunapotokea ndoa kukumbwa na vurugu za mara kwa mara ni Ulevi kupindukia, nyumba ndogo au makahaba, tofauti na wanawake ambao huchukua muda sana kufika hapo.
Leo hii mwanaume kuikimbia nyumba yake na kutelekeza familia ya mke na watoto sio jambo la kushangaza wakati zamani enzi zetu lilikuwa ni jambo la kufedhehesha na kubezwa mtaani na hata ukoo wenu ungepewa hiyo kasoro inapotokea mwanaukoo kuposa mahali fulani.


Siku hizi hilo halipo na wengi huchukulia powa tu. Zipo nyumba nyingi siku hizi hazina baba. Unakuta mama amebaki na watoto akihangaika peke yake kulea familia. Si kwa sababu baba amefariki, bali ni kwa sababu baba kaikimbia nyumba na kutelekeza familia.

Teamo
, Je hili unalizungumziaje?

Wakati mwingine baba hukimbizwa na kero za nyumbani, masimango,, dharau na mengine mengi... so kama ana roho fupi, hugeuka na kuangalia wapi atapata raha.....wake zetu mara nyingi hutumia watoto kama fimbo ya kutuadhibu......(waache watoto wangu), na walivyo ukiwa mpole basi vidole vitaingia kumacho....so tuangalie both side na kutafuta suluhu... sio ubabeshi....
 
ukimshirikisha Mungu kwenye ndoa yako hautatamani kutoka.....kwani kwa Mungu magumu yote huyarahisisha........
nadhani tumeikumbatia sana dunia ndo mana mambo mengi yanatuwia magumu......
 
kuna mengi saana katika ndoa,taasisi ya ndoa imechukuliwa kama ni kitu kidogo saana, vijana sasa hawajifunzi ni nini hasa maana ya kuwa na mme/mke, majukumu yao n.k lakini tuangalie ni nini hasa chanzo,kama nakumbuka vizuri MTAMBUZI uliiongelea kijiwe cha SALOON za kike kuwa moja kati ya vitu vinavosababisha kuvunjwa kwa ndoa nyiingi nadhani hiko ni moja ya chanzo kaka
 
Mshua, binafsi toka unikabidhi kwa Paw sijawahi kujuta. Ofcoz kuna wakati najiuliza what is this shitty lakini mwisho wa siku it is worth it. At least kuna mtu ambae naweza kumshushia stress zangu anytime i want hehehe. Kutofautiana nako kuna raha yake. Sana tu namuonea yeye huruma manake kuwa na mke mjeda sio mchezo. Hata ukienda kwenye small hausi unaisihi 'chonde dada, wife akijua sijui atatufanyaje manake akituua atakuwa katufadhili. Naomba ubehave na unisaidie kubehave'.
Pole yako Paw wangu na mie ndo sina hata mpango wa kukuacha. Lol

cc Kongosho

Sikjui, Sikufahahamu na wewe the same, lakini andiko lako limenifanya nicheke.

Hilo tu.
 
Ukitaka tamu ya ndoa tuulizeni WATANGA....
Huku waume twakoshwa na vifuu
Twasuguliwa na machicha ya nazi
Twakandwa na mafuta ya nazi
Halafu twakoshwa na maji ya hiriki
Hiyo ni kabla ya korodani kuoshwa kwenye kisosa
Kabla ya kubebwa kurudishwa chumbani

Kama hayo yote yangelifanywa na kila mtu pasipo hiyana hizi tunazoita majuto ya kuolewa yasingeliwepo.

Kuna haja ya Serikali kuu na serikali za mtaa kuangalia uwezekano wa kutenga bajeti ili wanawake katika mikoa mbalimbali wapelekwe Tanga wakajifunze namna bora ya ku-care wanaume na hivyo kujenga familia bora zenye upendo kwa maslahi ya nchi yetu.

Wasipofanya hivyo ndoa zitaendelea kupungua, na watoto wanaozaliwa watakuwa wengi wao hawana malezi mazuri kitu ambacho ni hatari kwa usalama wa taifa.
 
Back
Top Bottom