Mwanamke hebu funguka uko upande upi...?

Mwanamke hebu funguka uko upande upi...?

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,438
couple.jpg

Mara nyingi nimekuwa nikikutana na wanawake walio katika ndoa ambao hujuta sana na kusema kwamba wanajuta kuolewa na laiti wangejua kwamba maisha ya ndoa yako namna hiyo, katu wasingeolewa na wakati mwingine hukumbuka maisha yao kabla ya kuolewa jinsi yalivyokuwa mazuri na ya amani kuliko ilivyo sasa baada ya kuolewa

pretty-woman-hair.png

Lakini pia nimekuwa nikikutana na wadada walio single ambao wanayatamani sana maisha ya ndoa. Umri umekwenda na wamekata tamaa na wanatamani hata ajitokeze mwanaume yeyote yule amtamkie kumuoa ili mradi tu na yeye aingie katika orodha ya wanandoa.

18.jpg

Jambo hili limekuwa likinitatiza sana.
Walio ndani wanatamani kutoka na walio nje wanatamani kuingia. Je hii taasisi ya ndoa mbona imekuwa kizungumkuti hivi?

Naomba wanawake mnipe uzoefu wenu katika jambo hili....
 
mkuu wangu Mtambuzi

mi nadhan hawa wanaume waulizwe tu....!kiukweli mim binafsi hufika mahali ninajilaumu sana kwa uamuzi mgumu nilioufanya
 
Last edited by a moderator:
mkuu wangu Mtambuzi

mi nadhan hawa wanaume waulizwe tu....!kiukweli mim binafsi hufika mahali ninajilaumu sana kwa uamuzi mgumu nilioufanya
Teamo sasa waulizwe wanaume au wanawake..?
Mtenda kamwe hawezi kukumbuka madhila ya mwenzie isipokuwa mtendewa...
Naamini wanawake ndio wako kwenye nafasi nzuri katika kulielezea jambo hili na kwa uzoefu wao utatusaidia sisi wanaume kujitambua na kujua wajibu wetu katika ndoa na huenda ikasaidia kuokoa ndoa nyingi na kurudisha mioyo ya wanawake wanaojuta kuingia katika taasisi ya ndoa na kufurahia maisha yao ya ndoa, hivyo kuleta amani na upendo katika ndoa
 
kuna tofauti kubwa kati ya uhalisia na ndoto Mtambuzi inabakia pale pale kuwa mambo haya lazima yawepo ili dunia izunguke siku 356 na robo .kiuhalisia huwezi pata jubu sahihi wengi wanajuta kwenye ndoa wanawaza kwanini waliingia wengine wanang'ang'ania kuingia.nawashauri sana wenye ndoa zenu maisha hubadilika sana watu hawabaki constant kadri dunia inavyokucha watu wanabadilika .panua akili yako kaa katikati ya ndoto na uhalisia kwamba itakapotokea ndoa imekushinda give up.mimi nasema kuwa sintaupa moyo wangu hata sekunde kusikitika juu ya maamuzi ntakayofanya .nilizaliwa mwenyewe,ntazikwa mwenyewe,iam incharge of my own life ,nikifa ndoa imeishia hapo so ya nini kuitesekea .ISHI KWA AKILI HAPA DUNIANI UTAFIKA MBELE ZA MUNGU AKUTANDIKE MAKOFI NDIOPO AKUHUKUMU SABABU U WERE TOO IGNOGANT
 
Last edited by a moderator:
Natamani sana siku moja nioe, nami niitwe mume nami niite mke, sina matarajio makubwa kwenye ndoa yangu.......just anifulie nguo zangu, anipikie chakula, afanye usafi nyumbani, anipe pale kati, niishi kwa peace.....bhaaaaaaaaaaassssssss sihitaji kingine zaidi!!!!!
 
umetisha kaka.....!to you that is the rationale of marriage
 
@ Mtambuzi

mimi naamini kabisa kuna wanaume ambao pia hutamani sana kutoka nje
ya hii system-marriage...!ninaamini hivyo
 
Ingawaje huwa nakwazwa lakini sio kiasi cha kutaka kutoka looh ndoa ina raha yake bwana, najaribu kuwaza ningekuwa sijaolewa ingekuwaje, labda ningezaa na mume wa mtu ...halafu inakuwaje ukikaa nae anakwambia ngoja niwahi kwa wife, halafu nanuna au? Aaa hapana imekaa vibaya kwangu. Sitamani kutoka jamani.....na mnaotaka kuja njooni tu..
 
Nakubaliana na wewe kuwa maisha ya ndoa ni kama bahari labda niseme, maji kupwa maji kujaa, mawimbi na wakati mwingine shwari... sawa?
Lakini hebu tuseme ndoa imekushinda, yaani ni kwamba bahari imechafuka kiasi cha kuleta gharika, imeacha majeraha makubwa moyoni na hata mwilini na pia imeharibu mazingira yenyewe ya ndoa kiasi kwamba kurekebisha hali hiyo ni ngumu kumeza.
Hapo nakubaliana na wewe juu ya kauli yako hii:

"itakapotokea ndoa imekushinda give up.mimi nasema kuwa sintaupa moyo wangu hata sekunde kusikitika juu ya maamuzi ntakayofanya .nilizaliwa mwenyewe,ntazikwa mwenyewe,iam incharge of my own life ,nikifa ndoa imeishia hapo so ya nini kuitesekea..."

Lakini je Dini zinasemaje kukusu kuachana?
Je jamii inamchukuliaje mwanamke anayeitelekeza ndoa yake na kujitoa?
Je ndugu na marafiki wana mtazamo gani kuhusu jambo hilo?
Je mwanamke yuko tajari kukabiliana na hali hiyo? Yaani mashinikizo kutoka katika Dini, Jamii na labda ndugu na marafiki....

Hebu nipe uzoefu wako dada yangu kabla ya kikao chetu cha kahawa leo kujadili business proposal.... LOL
 
kuna tofauti kubwa kati ya uhalisia na ndoto Mtambuzi inabakia pale pale kuwa mambo haya lazima yawepo ili dunia izunguke siku 356 na robo .kiuhalisia huwezi pata jubu sahihi wengi wanajuta kwenye ndoa wanawaza kwanini waliingia wengine wanang'ang'ania kuingia.nawashauri sana wenye ndoa zenu maisha hubadilika sana watu hawabaki constant kadri dunia inavyokucha watu wanabadilika .panua akili yako kaa katikati ya ndoto na uhalisia kwamba itakapotokea ndoa imekushinda give up.mimi nasema kuwa sintaupa moyo wangu hata sekunde kusikitika juu ya maamuzi ntakayofanya .nilizaliwa mwenyewe,ntazikwa mwenyewe,iam incharge of my own life ,nikifa ndoa imeishia hapo so ya nini kuitesekea .ISHI KWA AKILI HAPA DUNIANI UTAFIKA MBELE ZA MUNGU AKUTANDIKE MAKOFI NDIOPO AKUHUKUMU SABABU U WERE TOO IGNOGANT

your advice is exclusive of christian women. Si ndo wameambiwa wang'ang'anie humo hata iweje (unless ni uzinzi).
I think Ukiingiza mungu on this, nothing will be solved. Tena dini zinavyoshikilia mfume dume. Mke akileta ubishi, all scriptures on her!

#source : my parents experience
 
Last edited by a moderator:
Natamani sana siku moja nioe, nami niitwe mume nami niite mke, sina matarajio makubwa kwenye ndoa yangu.......just anifulie nguo zangu, anipikie chakula, afanye usafi nyumbani, anipe pale kati, niishi kwa peace.....bhaaaaaaaaaaassssssss sihitaji kingine zaidi!!!!!

ndomanaana wanatamani kutoka.

Wanaume nchii hii wanalelewa na akili ya kwamba wanawake ni machine.
 
@ Mtambuzi

mimi naamini kabisa kuna wanaume ambao pia hutamani sana kutoka nje
ya hii system-marriage...!ninaamini hivyo
Mkuu kama unaweka katika mizania wanawake ndio hujuta zaidi katika jambo hilo...
Kwa kawaida wanaume walio wengi shabaha yao dhaifu kunapotokea ndoa kukumbwa na vurugu za mara kwa mara ni Ulevi kupindukia, nyumba ndogo au makahaba, tofauti na wanawake ambao huchukua muda sana kufika hapo.
Leo hii mwanaume kuikimbia nyumba yake na kutelekeza familia ya mke na watoto sio jambo la kushangaza wakati zamani enzi zetu lilikuwa ni jambo la kufedhehesha na kubezwa mtaani na hata ukoo wenu ungepewa hiyo kasoro inapotokea mwanaukoo kuposa mahali fulani.
Siku hizi hilo halipo na wengi huchukulia powa tu. Zipo nyumba nyingi siku hizi hazina baba. Unakuta mama amebaki na watoto akihangaika peke yake kulea familia. Si kwa sababu baba amefariki, bali ni kwa sababu baba kaikimbia nyumba na kutelekeza familia.

Teamo
, Je hili unalizungumziaje?
 
Ingawaje huwa nakwazwa lakini sio kiasi cha kutaka kutoka looh ndoa ina raha yake bwana, najaribu kuwaza ningekuwa sijaolewa ingekuwaje, labda ningezaa na mume wa mtu ...halafu inakuwaje ukikaa nae anakwambia ngoja niwahi kwa wife, halafu nanuna au? Aaa hapana imekaa vibaya kwangu. Sitamani kutoka jamani.....na mnaotaka kuja njooni tu..
Kwa hiyo swala hapo ni kiwango cha uvumilivu alicho nacho mwanamke katika ndoa yake ama? MADAM T tafadhali hebu fafanua hapo kidogo
 
Last edited by a moderator:
Maisha ni kupanda na kushuka kama ilivyo kwa ndoa kuna raha na machungu yake ndo mana wengine wanatamani kuingia na wengine kutoka pamoja na hayo MUNGU amewapa uvumilivu na ndo mana wengine wapo mpaka leo..........kuhusu ndani ya ndoa siwezi kusemea saana coz mengi siyafahamu..
 
Yeah Chocs wanasema ukitaka kujua uhondo wa ngoma ingia ucheze...
Unajua sio kwamba mimi sijui kuwa maisha ya ndoa ni kupanda na kushuka, najua sana, ninachojaribu kuchimba hapa ni kutaka kujua ni kwa nini siku hizi kauli za wanawake wanaojuta kuingia katika ndoa zimekuwa nyingi na wanaotamani kuingia wamekuwa wengi?
Au kwa sababu zamani matatizo ya ndoa mara nyingi yalikuwa yanafichwa lakini siku hizi huwekwa bayana?
Je ni mabadiliko ya kiuchumi na utamaduni ndio chanzo cha mtanziko huo au ni kitu gani hasa...?

Da AshaDii snowhite, @FP, King'asti na BADILI TABIA popote mlipo naombeni uzoefu wako katika jambo hili....
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi kama yalivo maisha mengine yoyote nje ya ndoa kuna milima na mabonde kwa mie sitamani kutoka.
 
Ukiwa upo nje ya ndoa utatamani kuinga ndani ya ndoa na hata kama watu walioko ndani ya ndoa watakushauri usiingie katika ndoa kwa kuwa kuna mateso na manyanyaso mengi ila hawataweza kuzuia hisia zako za wewe kuolewa.

Sasa unapokuja kwenye suala la kuumizwa either kwa matendo ambayo mwenzi wako anakufanyia, ndipo mtu unakuja kuyajutia na kutamani kutoka nje ya ndoa.

Ila kwenye ndoa kunahitaji uvumilivu na ustahimilivu wa hali ya juu kwani kunachangamoto nyingi, ukiwa na moyo mwepesi hutoweza kudumu katika ndoa yako.

Chamsingi ni kujua ni nini umekifuta katika ndoa na sio unakuwa mtu wa kuhadaishwa mara kwa mara.
 
Mtambuzi wakati mwingine sababu zinazotuingiza kwenye ndoa zinaweza pia kuwa chanzo cha majuto kwa walio wengi.

Yeah Chocs wanasema ukiaka kujua uhondo wa ngoma ingia ucheze...
Unajua sio kwamba mimi sijui kuwa ndoa ni kupanda na kushuka, najua sana, ninachojaribu kuchimba hapa ni kutaka kujua ni kwa nini siku hizi kauli za wanawake wanaojuta kuingia katika ndoa zimekuwa nyingi na wanaotamani kuingia wamekuwa wengi?
Au kwa sababu zamani matatizo ya ndoa mara nyingi yalikuwa yanafichwa lakini siku hizi huwekwa bayana?
Je ni mabadiliko ya kiuchumi na utamaduni ndio chanzo cha mtanziko huo au ni kitu gani hasa...?
 
Natamani sana siku moja nioe, nami niitwe mume nami niite mke, sina matarajio makubwa kwenye ndoa yangu.......just anifulie nguo zangu, anipikie chakula, afanye usafi nyumbani, anipe pale kati, niishi kwa peace.....bhaaaaaaaaaaassssssss sihitaji kingine zaidi!!!!!

yaani wewe haya unaita matarajio madogo?
1. Kufuliwa
2. Kupikiwa
3. Kufanyiwa usafi
4. Kupewa pale kati!

Yaani kama ni job description basi appraisal yake lazma iwe kubwa mnooo! Na appraisal iwe mara mbili kwa mwaka. Muulize Teamo akuambie kwi kwi kwi
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom