Mwanamke: Hata kama huzai kinakuuma nini..?

katika majaribu yoote duniani, omba Mungu wako jaribu hili lisikupitie.....

yaan hapo umenena! Wengi wetu hapa tunaongea tu weeee ila kama likikutokea binafsi,pengine haya mnayoongea hapa hutatenda hata mojawapo hasa kwa mwanaume! external pressure ni kubwa sna kias yaweza usihimili.nyie acheni tu!
 
Usemayo ni kweli Mtambuzi wanandoa wanatakiwa kufurahia maisha ya ndoa yao hata kama hawakujaliwa kupata mtoto pasipo kunyanyapaana. Lakini hili huwa gumu kubebeka pale ndugu, jamaa, na marafiki watakapoazisha maswali ya ni mwaka wa tatu sasa ndoa haijajibu mna tatizo gani. Itategemea na msimamo au uelewa wa mume kwani wengi wao husukuma tatizo kwa mke bila kufikiri kwamba hata yeye aweza kuwa tatizo.

Tunatakiwa tujikubali na kujidhamini hata kama hatukujaliwa watoto ambao huwa ni zawadi toka MUNGU na si matokeo mazuri ya muungano wenu.
 
Last edited by a moderator:
Mtambuzi unachokisema kina matinki sana lakini bana asikudanganye mtu, hata kama ndugu hawatasema kukosa mtoto kunasononesha sana, hasa kwa mama. jamani kila mwanamke anatamani abebe mimba na ndio maana hata wazungu wanafikia stage wanaasili watoto. kuna raha kuiskia kauli ya mwanzo ya mtt wako mwenye miezii sita akisema mmamam jamani hii ipo tu kimaumbile. wapendwa kuzaa kuzuri sana na nikutam sana hasa pale unapomtaka mtoto kusudiwa.

ila kwa wale wasioweza nawatia moyo, Mungu yupo pamoja nao atawapa kwa nama nyingine.
 
Last edited by a moderator:
Wanaume wana faida moja kubwa katika hili, hata wakibambikwa yawezekana wasijue milele. Ni rahisi kumfichia mume 'aibu'.

Kinachowasikitisha zaidi wanawake ni ile hali ya kuhisiwa kwamba kutokuzaa kwake kumesababishwa na sababu zisizo za asili kama utoaji mimba.

Ni vema wanandoa wakubali na kuamua kwamba maisha sio lazima watoto wawe wa kuzaa wenyewe.
 
hizi extended family zetu hizi...
ukichelewa kupata mtoto wanaweka midomo juu utafikiri uliolewa na ukoo mzima...

uombe upate mume mwenye msimamo, kama mumeo bendera fuata upepo.....lazima uwe stressed!!!!!!!!!!!
Sure.
Ukipata mume asiye na msimamo kwenye shida ya namna hiyo basi ndoa huwa mashakani.
 
Kweli ni tatizo,
si unaona hata watu wenye vijisenti vyao kama hawana watoto hawana amani kabisa.

Kwani wewe unasemaje kuhusu hili tatizo.
 
Rachel NA DADA YAKE Leah WALIOLEWA NA na Jacob , RACHEL akawa kipenzi cha mume miaka yote but kukosa mtoto kulimkosesha sana raha hata alipomzaa Yusuf ndipo furaha yake ilipotimia!

Sisi kwetu watoto ni baraka na ni utajiri sasa ukiwa kosa mh



Tatizo unakosa mtoto na pesa pia unakosa LOL!
 
wanaume hawaumii sana sababu wenyewe wameumbwa kwanza na mioyo mizito mie huwaga siamini physically sie wanawake na wanaume tuna uwezo sawa wa kuhandle jambo/stress ingawa wale wanaopigania haki za wanawake wanatueleza hivyo,lol jaribu kwenda msibani wanawake ndio wanaolia zaidi......wanaguswa zaidi......


second mwanaume mie kwangu naona saa yoyote hio hali ya kutokuwa na mtoto anaweza kuibadilisha kwa siri,hivyo anakuwa hana wasi wasi tofauti na mwanamke......

mwisho utamaduni wa ku adopt hatunao sana,i wish hawa ustawi wa jamii waanza kupiga kampeni adoption as one of the ways ya kuwasaidia child-less families...huku ughaibuni wameanza kitambo na hadi leo bado wanatangaza maredion kuhusu fostering....
 
hizi extended family zetu hizi...
ukichelewa kupata mtoto wanaweka midomo juu utafikiri uliolewa na ukoo mzima...

uombe upate mume mwenye msimamo, kama mumeo bendera fuata upepo.....lazima uwe stressed!!!!!!!!!!!

kuna rafiki yangu alioa wakachelewa kupata mtoto basi mama wa yule kijana akija kuwatembelea anafunga mdoli mgongoni wakati anamsaidia mkwee kufanya kazi ndogondogo. usiku anakaa nae seblen kama mjuu hebu niambie katika mazingira hayo inakuwaje kwa msichana?? si ataenda hata kwa mganga.
 
Ni kati ya mambo magumu sana kuhandle pindi linapotokea kwenye ndoa, haijalishi mume au mke, tuzidi kumuomba Mungu atuepushe na majaribu ya hii dunia ambayo kutokana kwayo mengine huleta matatizo hayo ya kutopata watoto na kwa yale ambayo ni natural basi pia tumuombe yeye huyo aliyetuumba ili tuwe na moyo wa kuhimili yote maana wototo ni zawadi kutoka kwake na kama ni ndoa mf ya kikristu ikiisha fungwa ndio hivyo tena, ukioa mwingine unazini na uzinzi ni chukizo mbele za Mungu na imeandikwa na ndoa iheshimiwe na watu wote.
 
kwakweli ndugu zangu msiba usikie kwa jirani......maji yakatike kwa mwenzio yakikatika kwako lawama....kulala njaa alale irani na sio wewe unweza ona mwisho wa maisha,

kimsingi hili tatizo linawakumba watu wengi sana Tanzania..na record zinatisha yaani katika wanandoa 10 basi 4 wanatatizo la kupata mtoto,lakini kimsingi tatizo nini.. hayo ni mambo ya kisayansi na sababu zake.. mabadiliko ya tabia ya nchi,tutawahukumu sana wanawake tukisema kwamba wanashindwa kwa kutoa mimba.....hii sio kweli kwani sio wote,ni 1 katika 10,hivi haya matatizo ya fibroids mnayaonaje?they can mess you up watu wana surgery hadi nne,mwisho hawapati watoto
Uchungu wa kukosa mtoto ni karibu sawa na uchungu wa kumzaa mwenyewe unless mtu awe hana mapenzi au hatamani kupata mtoto,

Ndoa ni ya watu wawili hivyo inategemea ni namna gani mume unamsupport mke au mke una msupport mume katika swala zima la uzazi,au uchaguzi wenu ni upi.La msingi ni kuielimisha jamiii kuhusu maswala ya uzazi,swala la kuzaa watu wanashangilia kesho wakienda shule kila mtu anakukimbia halifai.


Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamerahisisha maswala ya uzazi

mfano Kuna IVF ambayo wanachukua mbegu za mwanaume na mwanamke then zinakuwa fertilised then zinapandikizwa kkwa mwanamke though ni very sensitive as ukimess failure rate ni kubwa

kuna inseminatio ambayo mbegu za mwanaume zinaingizwa ndani kwenye yai la mwanamke na kifuatacho ni mimba

final ni Surrogacy ambayo ni sawa na IVF ila tofauti yake ni kwamba zinapandikizwa kwa mtu mwingine ambaye mnaingia mkataba naye anawazalia mtoto and anakuwa genetically ni wakwenu na kila codes zenu.....

ila uchaguzi unabaki ni wa wanandoa na wanacho kitaka ila swala la upatikanaji wa watoto limerahisishwa kidogo.

kinachotakiwa ni elimu
 
Mtambuzi mada yako ni nzuri sana.. But kiuhalisia utekelezaji wake ni mgumu sana kutokana na mitizamo mbalimbali iliyojengeka katika jamii.

Yumkini jambo hili linaweza kuvumilika ikiwa tu mume na mke wako pamoja katika kufarijiana na kupambana na changamoto hii.

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mimi nina miaka 9 na mke wangu hatujajaliwa mtoto na alinilazimisha sana na mimi nikafanye vipimo nilikuwa nagoma si kwakuwa nilikuwa naogopa kuwa mimi ntakuwa na tatizo ila ni kwakuwa nilikuwa najua ni mzima maana kuna girl friend alishatoa mimba zangu mbili, lakini alinishawishi nikasema niende nae awe na amani, nilipimwa na nikaonekana niko vizuri.

Kukimbia kwa miaka kulinifanya nichanganyikiwe juu ya kuapata mtoto haraka matokeo yake nikaanza kudandia wanawake mtaani kwa dhumuni hilo na nilioongozwa kwa hisia zaidi ya akili au niliongozwa kwa kichwa kidogo cha chini badala ya kikubwa cha juu.

I DID GET MORE THAN I BARGAINED: Wanawake watatu wote niliokuwa nao wote walipata mimba na mke wangu pia akapata mimba sasa hivi najuta kukosa uvumilivu na kutokuwa na imani. Nafikiria ntabebaje huo mzigo jibu sana mbaya zaidi kichwa kidogo kilichonisaidia kupata huo mzigo hakina usahuri wala mawazo kilishamaliza kazi yake, Stick to your
wife na mtafanikiwa tu.
 
Back
Top Bottom