Mwanamke haridhiki

Mwanamke haridhiki

godwinleo

Member
Joined
Mar 21, 2014
Posts
35
Reaction score
6
Nina mpenzi wangu anayefanya kazi Morogoro, mwezi march alikuja kunitembelea sababu alikuwa likizo na alikaa kwangu wiki 2 na siku 3 tangu afike. Alishikwa na malaria kali ikabidi niombe ruhusa kazini ili nimuuguze.

Kiukweli nilimpa kila kitu anachotakiwa kupewa mgonjwa including dawa,vyakula vilivyopendekezwa na daktari na vyakula alivyopenda mgonjwa, pamoja na gari kumpeleka hospitali au sehemu yoyote aliyopenda ili kumliwaza mgonjwa. Mungu akasaidia akapona na amerudi morogoro.

Lakini cha ajabu juzi ananiambia sikumjali alipokuwa anaumwa sababu sikuwahi kumletea kadi ya get well soon. Ebu nisaidieni kadi tu ndio mtu akujali?
 
Ha ha ha ha pole sana mkuu, she's too selfish and demanding achana nae huyo vinginevyo jiandae kuwa mtumwa wa furaha yake.
 
Hilo ni darasa zuri kwako,wanawake hawahitaji vitu vya gharama bali wanahitaji upendo.
Nadhani hilo ni fundisho kwamba mke unaweza kumpa hata karanga za sh.100 akakuona wa maana kuliko yule anayeleta matumizi ya nyumbani mengi lakini hana muda wa kutosha kuongea na mke wake.
 
Well said...
 
mkuu unatumia maji ya mende??nidai kreti
tatizo wanaume wanahisi expenses ndo matunzo kwa mwanamke,kuspend nae muda ndo matunzo kwake,hell nooo,labda kama mchimba dhahabu

TATIZO LAKO HUJUI VITU GANI UKIACHANA NA DAWA NA SIJUI KUMZUNGUSHA NA GARI NAAMANISHA VILE VYA ROMANTIC VINAVYOMPA RAHAHASWA AKIWA KWENYE MOOD KAMA YAKE
 
Nina mpenzi wangu anayefanya kazi morogoro mwezi march alikuja kunitembelea coz alikuwa likizo na alikaa kwangu wiki 2.siku 3 tangu afike alishikwa na malaria Kali ikabidi niombe ruhusa kazini ili nimuuguze kiukweli nilimpa kila kitu anachotakiwa kupewa mgonjwa including dawa,vyakula vilivyopendekezwa na daktari na vyakula alivyopenda mgonjwa.pamoja na gari kumpeleka hospitali au sehemu yoyote aliyopenda ili kumliwaza mgonjwa.mungu akasaidia akapona na amerudi morogoro.lakini cha ajabu juzi ananiambia sikumjali alipokuwa anaumwa sababu SIKUWAHI KUMLETEA KADI YA GET WELL SOON.ebu nisaidieni kadi tu ndio mtu akujali

Nahisi bado hajapona vizuri...inawezekana hiyo malaria imepanda kichwani...
Haiwezekani mtu mwenye akili timamu akadai card ni muhimu kuliko dawa na chakula. Nakusihi, kama unampango wa kuvisha pete hapo...fikiria marambili
 
Wanawake wanapenda vitu vidogo vidogo sana mkuu,kua romantic na kujua hisia zake na kuziheshm,kuzijali. Wanaodhan wanawake wanapenda mavitu makubwa wanakosea,labda wanawake machangu.

Nishawahi kung'oa mke wa kibosile mmoja kwa kujali tu hisia zake,.
 
Ataridhikaje kama hajaridhishwa? Take a lesson man acha kulalamika....
 
Dah, mawasiliano hafifu. Km alihitaji chakula au kitu Fulani na ukampatia kwa wakati, ni kwanini hakuomba kadi? Ila kakukumbusha, akiumwa tena mnunulie + mdoli
 
Kwanni uwe mtumwa???
Nashangaa sana wanaume wa sasa kitu cha kipuuzi kama hiki unamwambia unamwambia so ulitaka nikununulie kadi badala ya dawa?
Ukweli utakusaidia achana nae kuwa huru na maisha yako.
 
Upendo gani zaidi ya kumpeleka hospital na kuacha kwenda kazin?! A card seriously! Huyo mwanamke wa kwenye tamthilia achana nae, ungemuacha na malaria yake wala usingempeleka hospital halafu ungemnunulia card. Sihitaji card nikiumwa nahitaji anipendae karibu yangu period.
 
Kwanni uwe mtumwa???
Nashangaa sana wanaume wa sasa kitu cha kipuuzi kama hiki unamwambia unamwambia so ulitaka nikununulie kadi badala ya dawa?
Ukweli utakusaidia achana nae kuwa huru na maisha yako.

Yaani Leo umenifurahisha sana Ichana! Kuna wasichana wanafikiri mapenzi ni Kama wanavyotazama kwenye tamthilia, aggggrr
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom