Mwanamke Dar ajifungua chatu!

Mwanamke Dar ajifungua chatu!

Amejifungulia nyumbani? Hakuna maelezo ya mkunga/daktari? Hadithi ya kijinga kabisa.Hivi haya magazeti yanasimamiwa na chombo gani kuhakikisha yanatoa habari zisizopotosha?
 
Huyo chatu yuko wapi sasa?

Nilikuwa nataka kuuliza swali hilo hilo, huyu MziziMkavu huwa anavituko visivyo na ushahidi na wala sio mara ya kwanza kuleta uzi usiokuwa na mashiko. Binaadamu hawezi kuzaa mnyama au mnyama kuzaa binaadam.

Nyani Ngabu kuwadanganya watanzania wala sio kazi ilimradi tu uwaaminishe hata kama hukutoa ushahidi wataamini, ndio tabia za watanganyika wameshazoewea kudanganywa na wanapenda kudanganywa
 
Tatizo source ya habari ilipotoka ni vigumu kuamini hata ikisema kweli...99.99% ni uongo mtupu...
 
Nyani Ngabu kuwadanganya watanzania wala sio kazi ilimradi tu uwaaminishe hata kama hukutoa ushahidi wataamini, ndio tabia za watanganyika wameshazoewea kudanganywa na wanapenda kudanganywa

Yaani ni rahisi mno.

Lakini hiyo yote ni kwa sababu tunapenda kuendekeza ujinga.

Kwa mfano tu, ukitaka kuleta kizaazaa sehemu jaribu kuchukua paka halafu shingoni mfunge matambara halafu weka na kikaratasi chenye maneno ya Kiarabu (na si lazima hayo maneno yamaanishe chochote...unaweza ukaungaunga tu herufi, basi).

Halafu kabla watu wengine hawajaamka ile alfajiri kamtupe uani kwa mtu.

Hahahaaa.....naweza kukuhakikishia kuwa watu siku hiyo hawatalala. Wanaweza wakashinda hata kwa mganga wakijaribu kujua hayo maneno yanamaanisha nini.
 
Kama ni kweli basi ni aina ya wakina mama wanaotafutia

watoto kwa wanganga wa kienyeji.

Haya ni mauzauza kuna mwingine nakumbuka mwaka 1979 alijifungua sungura na baadaye yule mama alifariki.
Weka picha ya huyo sungura,otherwise na wewe ni Shigongo tu!!!
 
Mmeuziwa mbuzi kwenye gunia kwa dadithi ya chatu aliyezikwa.
 
Unaambiwa mtoto kazaliwa hospital lakini jina hospital hakuna hivi hizi enzi za utandawazi kweli azaliwe mtoto kama huyo hata wandishi wa habari wa magazeti makini wasijue lakini sishangai ndio udaku huo
 
Huyu alizini na chatu au hiyo mimba alipewa na mganga huyu chatu aliyeyuka baada ya kuzaliwa mbona hamna picha?
 
Back
Top Bottom