Mwanamke Dar ajifungua chatu!

Mwanamke Dar ajifungua chatu!

Yaani ni rahisi mno.

Lakini hiyo yote ni kwa sababu tunapenda kuendekeza ujinga.

Kwa mfano tu, ukitaka kuleta kizaazaa sehemu jaribu kuchukua paka halafu shingoni mfunge matambara halafu weka na kikaratasi chenye maneno ya Kiarabu (na si lazima hayo maneno yamaanishe chochote...unaweza ukaungaunga tu herufi, basi).

Halafu kabla watu wengine hawajaamka ile alfajiri kamtupe uani kwa mtu.

Hahahaaa.....naweza kukuhakikishia kuwa watu siku hiyo hawatalala. Wanaweza wakashinda hata kwa mganga wakijaribu kujua hayo maneno yanamaanisha nini.

hahaaahahaaaa!
we jamaa tumesoma wote nini?
tuliwah mfanyia hiyo kitu mwalimu wetu, alikuwa mkali hatar, vijana wakaona isiwe tabu!

huwezi amin aliumwa hadi kulazwa!!
ila from there alikuwa mpole kama karogwa tena!!!! vijana hatr sana
 
Mwanamke ajifungua simu aina ya galax s3 huko mbagala ntaleta picha.
..

Mkuuu please pleaseee....naomba contact ya huyo mama ninfanye nyumba ndogo!!! Nitakuwa nam mimba kila siku...hebu niulizie kwanza..atakuwa anazaa matoleo latest au ni s3 tuu!!?
 
Atakuwa.mtoto wa kumtafuta kwa wagangani sawa na stori ya wimbo wa bahat bukuku
 
Udaku, kama ule wa watu kunatiana sehemu za siri!
 
Oh nilidhani labda nikikubandia picha ya chatu tu utaamini.

Licha ya hivyo, huu ni mwendelezo uleule wa hadithi zisizo na vithibitisho vyovyote vile.

Tena ukizingatia kwamba tuko kwenye zama za simu za mkononi zenye kamera ndo kabisa hizi hadithi zinakosa mashiko.
Hasa ukizingatia gazeti lenyewe lililotoa habari huwa linarusha picha mpaka zisizotakiwa kurushwa kutokana na maadili kiasi kwamba leo wamekuwa waungwana wasitoe picha
 
kaburi alilofukiwa liko wap msiba ulikua wap,? hii picha kama ya kihind.mwisho wakamatwe hao waliozka kiumbe ambaye tungemtumia kama maonyesho ili kuingiza mtonyo
 

WAANDISHI WETU/Amani


MAAJABU! Ama kweli dunia ina mambo na ya Mungu mengi! Mwanamke mmoja, mkazi wa Mbezi- Maua jijini Dar aliyefahamika kwa jina moja la Neema, amelea ujauzito wake kwa miezi tisa yenye matumaini lakini siku ya kujifungua akaambulia kiumbe cha ajabu kilichofanana na nyoka aina ya chatu, Amani limeifuatilia habari hii kwa kina.


attachment.php


Neema anayedaiwa kujifungua Chatu.

Kwa mujibu wa chanzo chetu, awali Neema alikuwa akisumbuliwa na pepo wachafu hali iliyomfanya akatishe masomo ya sekondari na kuanza kwenda kanisani kila wakati kwa ajili ya maombi.


MAUZAUZA KILA MARA

Chanzo kilisema kuwa, kipindi chote hicho, Neema alikuwa akianguka na kutaja majina ya watu wa mtaani anapoishi kwamba ni wachawi, wengine wanahusika kumchukua yeye usiku na kwenda naye makaburini ambako humlisha nyama na kumnywesha damu za watu.


“Neema alikuwa akisumbuliwa na mapepo tangu akiwa mdogo na alikuwa anasumbua kwelikweli. Alipokuwa akipandisha ‘madudu’ yake hayo hakuna aliyeweza kumshika labda wanaume kama watano. Pia kuna wakati alikuwa akitaka kujiua kwa kujichoma kisu,” kilisema chanzo hicho.



attachment.php


Mama mzazi wa Neema.
MAMA MZAZI ASIMULIA
Naye mama mzazi wa Neema ambaye hakupenda kujitambulisha kwa jina, alipozungumza na gazeti hili huku majirani wakifurika nyumbani kwake, alisimulia jinsi mwanaye huyo alivyokuwa akiteseka kipindi chote tangu alipokuwa mdogo mpaka ikafika hatua amepata ujauzito huo na hatimaye kujifungua kiumbe kinachofanana na chatu.

“Ni mambo mengi ambayo tumeyapitia lakini siwezi kumkufuru Mwenyezi Mungu kwa sababu mpaka leo hii tuko wazima japo mitihani ni kipimo cha maisha na hata hili lililotokea karibuni ni mtihani pia, ila kikubwa ni kuomba sana.
“Baada ya kupata huu ujauzito kuna wakati tulikuwa hatulali, akianza kulia ni usiku kucha, anasema kuna kitu kinambana kifuani. Tulipokuwa tukienda hospitali kwa ajili ya uchunguzi, vipimo vilionesha mtoto tumboni hachezi.


attachment.php


“Mimi kama mzazi, hayo mambo yaliyokuwa yanamtokea mwanangu nilikuwa nayaona kama maajabu f’lani hivi japokuwa kipindi hicho alikuwa mzima na mimi mwenyewe nilikuwa nikimsubiri mjukuu wangu kwa hamu, kumbe tunakuja kupokea kitu cha ajabu namna ile,” alisema mama huyo.


SIKU YA KUUMWA UCHUNGU
Iliendelea kudaiwa kuwa, kipindi chote cha ujauzito, Neema alikuwa mtu wa maombi, lakini siku ya kuumwa uchungu alikimbizwa hospitali (haikutajwa jina) na kujifungua kiumbe cha ajabu. Ndipo familia ikaamua kukaa kikao na kuamua kukizika kiumbe hicho kama chatu.


Mama Neema anasema: “Mwanangu alijifungua kiumbe cha ajabu, kilikuwa kama chatu halafu kina magamba na meno mawili marefu lakini hakikuwa hai. Tulishtuka sana, tukaona ni mkosi katika familia lakini tuliamua kukizika kile kiumbe.“Sikuona sababu ya kuwaonesha majirani zangu kwa kuwa kilikuwa kinatisha. Ila naona ni bora niwape taarifa kuwa, mwanangu alijifungua kiumbe cha ajabu.”



attachment.php


ALICHOSEMA ALIYEJIFUNGUA

Naye Neema mwenyewe alipozungumza na Amani kuhusu tukio hilo la ajabu, alikuwa na haya ya kusema:“Mimi mwenyewe sikupenda kuzaa chatu jamani, nimepitia mambo mengi ya ajabu, wazazi wangu ndiyo wanajua fika hali niliyokuwanayo huko nyuma, lakini sina namna.


“Labda niwaulize mama zangu ambao tayari walishazaa kama tumbo huwa linapanda juu mpaka kifuani badala ya kushuka? Na nilikuwa nakabwa sana kuanzia kifuani mpaka kwenye koo, usiku sikuwa nalala kutokana na maumivu niliyokuwa nikiyapata mpaka nilipojifungua hicho kiumbe.


“Usione watu tunatembea, hatujijui tuna nini kwenye miili yetu. Leo hii yamenikuta mimi, kesho mtu mwingine. (huku akiwaangalia majirani) mi nawaomba ndugu zangu tukazane kumwomba Mungu kwani mimi maombi yamenisaidia sana.” chanzo.
www.globalpublishers.info

Maelezo marefu ambayo hayana maana yeyote, kama unaleta habari andika na uambatanishe vielelezo au walau picha, tunaona wakamatwe tu na maelezo ya kidaku
 
Hapo hakuna chatu wala nini bali ni kiumbe hakikukamilika ndio maana wanakiona kama huyo chatu. Naamini scientifically system ya chatu na binadamu ni tofauti kabisa hivyo hiyo kitu si rahisi kutokea. Halafu ukute hiyo ni miscarriage yaani mwili ume-reject hicho kiumbe kikiwa kwenye hatua za awali za formation!
 
mbona hakuna sehemu yoyote inayomuelezea mtu aliyempa mimba hii itakuwa maigizo fulani hivi
 
Back
Top Bottom