Mwanamke auawa kwa kupigwa risasi na polisi

Mwanamke auawa kwa kupigwa risasi na polisi

Magazetini

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2014
Posts
593
Reaction score
1,713

singida-oct18-2014.jpg

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela


Mwanamke mmoja mkazi wa Kijiji cha Iglansoni, ameuawa kwa kupigwa risasi kichwani kwa bahati mbaya na askari polisi waliokuwa katika jitihada za kumkamata mtuhumiwa wa ujambazi.

Aliyeuawa ni Joyce Maragabu (65), ambaye anadaiwa kupigwa risasi na askari hao waliokuwa wakijihami na kundi la watu waliotaka kuwavamia ili wasimkamate mhalifu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Singida, Geofrey Kamwela, alisema askari hao walikuwa wanataka kumkamata, Nkida Gwisu, anayetuhumiwa kumshambulia mtu mwingine, lakini kwa bahati mbaya risasi hiyo ikampiga kichwani mwanamke huyo aliyekuwa anafua nguo nyumbani kwake.

Kamwela alisema, tukio hilo lilitokea juzi Oktoba 16, saa 6 mchana.

Alisema askari polisi wawili ambao hakuwataja majina yao wa kituo kidogo cha polisi Ihanja, walifika katika kitongoji hicho ili kutoa ulinzi mnadani, lakini baadaye walipewa taarifa kuhusu mtuhumiwa huyo kumshambulia mmoja wa wanakijiji.

Alisema wakati wakiwa katika jitihada ya kumtafuta mhalifu huyo, alitokea mwananchi mmoja aliyedai kumfahamu mtuhumiwa huyo, hali iliyorahisisha kazi ya kumkamata na kumweka chini ya ulinzi.

Hata hivyo, alisema baadaye mtuhumiwa huyo alianza vurugu, hali iliyosababisha kundi kubwa la watu kwenda eneo hilo wakiwa na silaha za jadi ikiwamo mawe, pinde, mishale, fimbo na mapanga, na kuanza kumshambulia mmoja wa askari polisi aliyemshikilia mhalifu huyo.

Alisema kuwa katika hali ya kutaka kumwokoa mwenzake, askari aliyekuwa na bunduki alifyatua risasi moja ya moto hewani, lakini hata hivyo wakiwa kwenye purukushani, ndipo risasi moja ilifyatuka na kumpiga kichwani mwanamke huyo.

Kamwela alisema baada ya tukio hilo, wananchi waliokuwa na hasira waliichoma moto pikipiki ya askari hao, yenye namba za usajili PT 3242 –Yamaha na kuiteketeza.

Alisema kutokana na vurugu hizo, askari hao walijeruhiwa vibaya baada ya kupigwa na kundi hilo na tayari jeshi hilo linawashikilia askari hao kwa mahojiano zaidi.

CHANZO: NIPASHE
 
Habari hii haiko vizuri,
Mama anafua nguo nyumbani saa sita mchana, alihusikaje na hao polisi sasa.
Waseme mtu walimmwangosi mama wa watu.
 
Kwanini wananchi wawazuie polisi kumkamata muhalifu?
Hii habari imetoka polisi bila kupata upande wa pili wa wananchi so hatutakiwi kuiAmini moja kwa moja
 
Habari hii haiko vizuri,
Mama anafua nguo nyumbani saa sita mchana, alihusikaje na hao polisi sasa.
Waseme tu walimmwangosi mama wa watu.
Nakuunga mkono Mamndenyi, hiyo itakuwa movie ya kipolisi itakayopachikwa jina la Daudi Mwangosi part 2.
 
Hayo polisi watauaje mmama kisingizio eti vurugu wananchi nao wangewa malizia na wao
 
na mashuhuda wa tukio wanasemaje? tukusema walikodiwa kwenda kumuuwa huyo mwanamke watasemaje?????
usalama wa taifa sijui mnalipwa kuchunguza cdm
 
Jamii kwa asilimia kubwa imepoteza imani na jeshi la polisi....ikifikia hatua wananchi hawataki mtuhumiwa akamatwe na polisi kuna tatizo, la mwisho hii habari imeungwaungwa sana na kuna kitu kamanda anaficha, mara kapiga riasi hewani mara mama anafua mara bunduki ilifyatuka, ina maana mama naye alikuwa anazuia polisi wasimkamate mtuhumiwa?
 
Aisee,ni tantalising story.Nao wananchi na wachangiaji inasomeka akilini kwamba hawana imani kabisa na Police Tanzania!
 
Baada ya kulinda raia na mali zao....wanawauawa raia na kuchukua mali zao....
 
Polisi wa nchi hii walishafail muda mrefu. Wamebaki kuomba rushwa tu
 
Kwa sasa jeshi la polisi linaongoza kwa mikosi na kukosea ovyo linahitaji maombi ya kukombolewa toka kwenye laana ya damu zisizo na hatia.Nataka nikafanye toba kwenye kwenye kaburi la Mwangosi naona ile damu inasumbua sana.
 
Ina maana huyo mama alikuwa anafulia hewani au mi ndo sijaelewa?

Si waseme tu ukweli wa mambo au ni yaleyale ya Tibaigana na issue ya Ditopile eti 'alikuwa akigonga gonga ndipo risasi zikafyatuka'
 
Wananchi kuwazuia polisi kufanya kazi yao ni hatari sana. Alale salama.
 
Haya matukio ya watu kuawa kwabahati mbaya yamekua meng sana nakupelekea familia zinazo achwa nahao wanao uliwa kuishi bila matumaini nafikili umefika muda sasa serikali ichukue jukumu lakutunza familia zilizo achwa kwa kukadilia muda wa kuishi kwamaisha ya mtanzani,
 
Wananchi kuwazuia polisi kufanya kazi yao ni hatari sana. Alale salama.

kwa hivyo huyo aliye uawa wewe hujaliona ila la raia kuzuia askari kufanya kazi yao ndio lililo kugusa! Heri kuwa mavi kichwani kuliko kuwa na akili kama wafuasi wa ccm?
 
Back
Top Bottom