Herbalist Dr MziziMkavu
Platinum Member
- Feb 3, 2009
- 43,093
- 34,909
Mwanamke aoa wanaume wawili
Jaiya Ma, 34, amewaweka kinyumba wanaume wawili ambao anaishi nao kwa kuwahudumia kila mmoja kwa zamu.
Wanaume, Jon Hanauer, 48, na Ian Ferguson, 44, wanaishi kwa amani, hawaparurani, kila mmoja anaridhika kushea na mwenzake.
Watatu hao, wanaishi kwenye nyumba ya kifahari ya Jaiya, iliyopo Topanga Canyon, kaskazini ya Malibu, California, Los Angeles, Marekani.
Katika uhusiano huo, Jaiya, amefanikiwa kujifungua mtoto mmoja anayeitwa Eamon ambaye kwa sasa ana umri wa miaka miwili.
Mtoto huyo, Jaiya amezaa na Ian ambaye yupo naye kimapenzi kwa mwaka wa nne sasa.
Wanaume hao, walianza kuishi pamoja miaka minne iliyopita, kwani Jon yupo na Jaiya kwa zaidi ya muongo (miaka 10) sasa.
Mtindo wa maisha yao ni mzuri, kasoro ni moja tu kwamba Jaiya na Jon wana vyumba vyao, wakati Ian yeye hulazimika kuegesha sehemu yoyote.
Kutokana na kukosa chumba, Ian hulazimika kulala katika chumba cha Jaiya, Eamon au kwenye ofisi yake iliyopo ndani jumba hilo lenye ghorofa moja.
Kuhusu wivu, Jaiya anasema kuwa kuna wakati dalili za mgogoro hujitokeza lakini anamshukuru Mungu kwamba kila mmoja hujitahidi kudhibiti hisia za wivu.
Si Jon wala Ian aliyefunga ndoa halali na Jaiya lakini wanaishi kwa amani.
Ian na Jon hawajawahi kugombana wala kukwaruzana, wanakubali hali halisi na kila mmoja anapata kile anachohitaji, alisema Jaiya na kuongeza:
Nimewafungulia milango, anayeweza atafute mwanamke mwingine na tutaishi wote bila wasiwasi.
Jon hajatangaza nia ya kuwa na mwanamke mwingine lakini Ian yeye ameshaweka wazi kuwa anasaka mwanamke mwingine na akishampata, atamuingiza kwenye jumba hilo la kifahari ili kuongeza familia.
KUHUSU JAIYA
Mwanamke huyo ni mtaalamu wa masuala ya mapenzi na hivi sasa ameanzisha darasa linalotoa elimu ya mambo ya ngono.
Jaiya, anaelezwa kuwa fundi wa mapenzi ndiyo maana anaweza kuwatosheleza wanaume hao na kuwapagawisha kiasi kwamba hakuna anayefikiria kumuacha.
Hii ni kali bado haijaumuliwa kabisa kama ni pombe basi itakuwa ni Gongo.