Mwanamke anapotoa kauli hizi, JIHADHARI....!

Mwanamke anapotoa kauli hizi, JIHADHARI....!

Mtambuzi

Platinum Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
8,809
Reaction score
15,438
lean-in-woman.jpg


1. Mwanamke anaposema, 'sasa hivi' au 'dakika moja tu,' maana yake ni kwamba, ni nusu saa ijayo. kwa mwanamke sasa hivi ya kujiandaa ina maana sasa hivi ya muda mrefu mara sita zaidi kuliko ule anaoutaja. kama akisema , 'nusu saa tu, naja,' unapaswa kwenda kufanya shughuli nyingine kwanza, kwa sababu huenda ukiamua kuamini kwamba ni nusu saa kweli, utasimama au kukaa mahali kumsubiri hadi miguu iingie tumboni au makalio yaote ganzi.

2. Mwanamke anaposema, 'utajua mwenyewe,' ana maana kwamba amekasirishwa na kukatishwa tamaa na tabia yako na sasa hajali tena. maana yake ni kwamba kwa upande wake haoni sababu ya kujiumiza bure na huenda atachukua uamuzi ambao nawe pia hautaufurahia. Je, anaweza kuanza kutoka nje baada ya hapo? inawezekana ingawa siyo lazima.

3. Mwanamke anapopumua kwa nguvu, yaani kushusha pumzi kwa kishindo, hiyo pia ni kauli kwa upande wake. kama anashusha pumzi kwa nguvu wakati mkijadili au kuongea jambo, ni taarifa kwamba amekudharau. yaani amekuona mjinga nambari moja. ni kauli kwamba, haoni sababu ya kuendelea kuwepo hapo kubishana nawe, kwani huna jambo la maana unalomweleza.

4. Mwanamke anaposhusha pumzi polepole, ina maana kwamba, amekubaliana na wewe. Sasa hapo usifanye kosa kwani, ukibadilika kidogo au kuleta mambo mengine kinyume na na hayo yaliyomridhisha, ndipo hapo atashusha pumzi kwa nguvu , yaani kuanza kukuona huna maana kwa wakati huo. Kumbuka kwamba, mwanamke akishusha pumzi kwa nguvu kwa maana ya kukuona huna lolote, hukuona hivyo kwa wakati ule tu au kwa hilo jambo linalohusika tu, siyo kwamba, hukuona hivyo siku au muda wote. vivyo hivyo kwenye kushusha pumzi pole pole, hukuona 'babu kubwa' kuhusiana na na jambo mnalojadili kwa wakati huo tu.

5. Mwanamke anapotumia neno, 'sawasawa,' kwa kawaida kama kuna jambo umemfanyia, ina maana kwamba, 'ninachukua muda kutafakari, halafu utaona nitakachokulipa baadaye.' Kauli hii siyo nzuri na mara nyingi ni ya hatari. Wanaume ambao wamewahi kulipiziwa visasi kwa njia mbaya na ya hatari na wapenzi wao wamekiri kuambiwa, 'sawasawa,' au 'sawa bwana,' kabla ya visasi hivyo.

6. Mwanamke anapotamka neno, 'we endelea tu,' anakuwa na maana ya kwamba, siku si nyingi zijazo, atafanya jambo ambalo hutalifurahia, kama hutaacha kufanya kitu au jambo lenye kumuudhi. hiyo ni kauli ya kukutahadharisha kwamba, usije ukashangaa pale ambapo utaona amefanya kitendo cha hatari dhidi yako kutokana na tabia yako au matendo yako mabaya dhidi yake.

7. Kuna wakati mwanamke anaweza kusema, 'sawa bwana fanya,' kama kuna jambo ambalo hamjafikia muafaka au amebaini umekuwa ukifanya jambo fulani baya au lenye kumkera. Hapa hana maana kwamba, amekuruhusu kwa moyo mmoja, hapana. Hapa anataka ubaini kwamba, hajakubaliana nawe, anakupa muda wa kujaribu kutafakari tena.

8. Je kama mmeshindana katika jambo au umemkera katika jambo au mambo fulani, kutokana na tabia au mwenendo fulani, halafu akakumabia, 'asante sana,' itakuwa na maana gani? Hii ina maana umemkera kupita kiasi na bado wala hajajua akufanye nini. Hii ni toafauti na 'asante' ya kawaida. Mwanamke anapoongeza neno 'sana,' ujue umemkera hasa, kuliko unavyoweza kufikiri. Halafu kama baada ya kusema, 'asante sana,' anashusha pumzi kwa nguvu, ujue hali ni mbaya zaidi, bora unyamaze kwanza, hata radhi usiombe kwa muda huo, subiri apoe kwanza.....

Ujumbe huu ni mahsusi kwa mkwe wangu Paw ili amfahamu vizuri binti yangu, King'asti......

Copy to Madame B, Paloma, amu, cacico, gfsonwin, snowhite, Fixed Point, Kipipi, Asnam, Preta, marejesho, Nyamayao, ladyfurahia, Lady doctor, BADILI TABIA, miss wa kinyaru, mdida, Nivea, Lisa, Kaunga, MadameX, Kongosho, Gaijin, sister, sweetlady, FirstLady1, Arabela, KOKUTONA, lara 1
 
Kwenye hiyo namba moja,umenikumbusha kisa kimoja,mama yangu mlezi alikua anasafiri kutoka Mwanza kwenda nyumbani Moshi,basi lilikuwa linaondoka saa 12:00 alfajiri,mimi nikawa nimefika stand asubuhi saa 11 nikamsubiri mpaka saa 11:30,simuoni!Kumpigia sim akaniambia "nafika hapo baada ya dakika 5 tu"
'
Ikabidi nijiongeze,nikachukua tax kumfuata nimkakuta ndo anamalizia kuvaa,ilibidi mafuta ajipakie kwenye tax na kidogo tuchelewe
'
Hao ndo wanawake bana!
 
Hayo mengine sina uhakika sana, ila hilo namba moja halinihusu hata kidogo


Kawaida ukinivurumua kutoka nitakwambia "huwezi safari na mimi, maana nahitaji muda wa kujitayarisha nawe huna muda huo, hivyo nenda"

Ila nikikwambia nahitaji nusu saa, ni nusu saa kweli

Na hapo ujue nishaweka na dakika za akiba, ili nisikucheleweshe
 
Hayo mengine sina uhakika sana, ila hilo namba moja halinihusu hata kidogo


Kawaida ukinivurumua kutoka nitakwambia "huwezi safari na mimi, maana nahitaji muda wa kujitayarisha nawe huna muda huo, hivyo nenda"

Ila nikikwambia nahitaji nusu saa, ni nusu saa kweli

Na hapo ujue nishaweka na dakika za akiba, ili nisikucheleweshe
kama no moja haupo basi una bahati...mimi zaidi ya kuchelewesha watu huwa najichelewesha mwenyewe.....
 
kama no moja haupo basi una bahati...mimi zaidi ya kuchelewesha watu huwa najichelewesha mwenyewe.....

Mimi nipo very time conscious hususan mtu mwengine anapohusika kwa sababu sipendi niwe chanzo cha udhia kwa mtu mwengine

Kama muda alokuwa nao kunisubiri ni mdogo nami haunitoshi, "humwambia nenda tu, nimekusameh' " kuliko kupigizana kelele na mtu mzima mwenzangu

Lakini labda kwa sababu tangu hapo mwanzo, sipendi safari zisizokuwa na ratiba, hivyo huwa natafuta sababu ili niitose
 
"Hivi kwa nini upo hivi/hivyo?"

Kuna wakati mwingine wanawake hutamka hivyo. Matamshi hayo huashiria kukereka na kukata tamaa maana pamoja na juhudi zake za kukubadilisha jambo fulani ambalo ni kero kwake, lakini mwanaume ndio kwanza walirudia jambo hilo kila uchao....
 
Hiyo namba moja mi naona ina apply kwa wote...ME na KE. Frankly speaking nimeshakwaza na nimeshakwazika sana kuhusu hilo.

Huko kwingine huwa naishiaga kulia tuuu nikilia nikinyamaza hasira zangu zimeisha...kujibishana kugombana kumshika kiuno akuu...Ukiniudhi i wont argue sana sana nitajifungia chumbani nikutafakariii na automatically machozi hunitoka...baada ya hapo life goes on

Sasa ni juu yako kujisachi na kujiuliza na kujipanga how are you going to handle me coz silence kills u know
 
mengi yana ukweli kiasi, chanzo ni kipi ili tuyapate kwa undani zaidi?
 
Back
Top Bottom