Mwanamke anaolewa kwa vitu vinne

Mwanamke anaolewa kwa vitu vinne

Dr criminal

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2022
Posts
2,284
Reaction score
4,338
Wakuu,

Anasema Mtume Muhammad (S.A.W) ya kwamba mwanamke anaolewa kwa vitu vinne;
1. Mali zake
2. Ukoo/familia aliyotokea
3. Dini yake
4. Uzuri wake

Kwa kifupi:

Mali zake
Mwanamke, yeye kama yeye anamiliki nini? Iwe ameaijiriwa, anafanya biashara au kama ana mali za kurithi.
Siyo kwamba wasio na kitu wasiolewe hapana, hawa kuna watu wao watakuja kuwaoa, ila unapoamua kuoa hasa mwanaume ambaye uchumi haupo vizuri, kipengele cha hali ya uchumi wa mwanamke unayetaka kumuoa ni muhim sana.

Unakuta mwanaume ukoo mzima yeye ndiyo angalau anajiweza, kwahiyo kwa kidogo anachokipata anahakikisha hadi mtoto wa mjomba kule kijijini anapata sare za shule, anaenda kuoa mwanamke ambaye kwao wana hali ngumu kama ya huyu mwanaume, mwisho wa siku unajikuta unamzigo wa kuhudumia familia kama tatu hivi, yako, kwenu na kwa mwanamke, hapo lazima tukuzike mapema.

Mifano iko mingi:
Naseeb Abdul mpenzi wake wa kwanza maarufu, Wema Sepetu kwa kipindi kile alikuwa na utajiri na umaarufu kumzidi Naseeb, kila mtu anajua mchango wa Wema kwenye safari ya Naseeb.

Huyu huyu Naseeb akawa kwenye mahusiano na Zari Hassan mpaka wakazaa watoto wawili, nadhani mlikuwa mnaona kwamba Naseeb alikuwa hatumii nguvu nyingi kwenye hili penzi kwa sababu Zari Hassan hakuwa na njaa.

Ukoo au familia aliyotokea
Hii imekaa kwa upana sana, kuanzia kibailojia mpaka kijamii, ni muhim kuchunguza asili ya familia unayoenda kuoa. Aisee kuna familia zinamatatizo sana, wengine wana mila na desturi za ajabu ajabu, wengine familia nzima ina historia ya kuachika zaidi ya mara tano, unakuta familia ina historia ya kutopata mtoto wa kiume na vitu kama hivyo.

Kibailojia kuna yale magonjwa ya kurithi, vitu kama Sickle cell anemia, Albinism, na vitu kama hivyo, ni muhimu kuangalia historia ya familia kwenye magonjwa ya kurithi. Chunguza kwa makini ujilizishe.

Dini yake
ukioa mwanamke ambaye hajashika dini, umeangamia, ielewe kama ilivyoandikwa. Ukioa mwanamke ambaye hana hofu ya Mungu we ukazingatia tu kalio wakati umeenda kuoa umejila, nakuahidi.

Uzuri wake
Mwanamke ambaye amejaaliwa uzuri anatamaniwa kuwa mke kwa wanaume wengi. Iko hivyo yaani, oa mwanamke mrembo, mwanamke mzuri, mwanamke anayekuvutia, hii itapunguza hata hizo tamaa za kuchepuka hovyo. Yaani nyumbani una bonge la kisu kiasi kwamba ule muda wa kazi unauona mwingi sana, unatamani kurudi nyumbani ukamuone.

Zingatia:
Mwanamke ndoa ni majaaliwa.
Mwanaumeu sijichanganye.



#OneDayYouWillBeGone
Dr criminal


UPDATE:
Nashangaa kwenye comments watu wanamu-attack mtume, hapa nimeleta moja ya idea yake tuijadili, sio tubishane kuhusu dini, na kama unapenda sana kutukana nitukane mtoa mada vinginevyo mteleta vita ya kidini na halikuwa lengo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wakuuu.


Anasema mtume Muhammad (S.A.W) ya kwamba mwanamke anaolewa Kwa vitu vinne.

1.mali zake
2.Ukoo/familia aliyotokea
3.Dini yake
4.Uzuri wake

In short.....

MALI ZAKE
Mwanamke, yeye kama yeye anamiliki nini? iwe ameaijiriwa, anafanya biashara au kama ana mali za kurithi.
Sio kwamba wasio na kitu wasiolewe hapana, hawa Kuna watu wao watakuja kuwaoa, ila unapoamua kuoa hasa mwanaume ambaye uchumi haupo vizuri, kipengele cha hali ya uchumi wa mwanamke unayetaka kumuoa ni muhim sana.
Unakuta mwanaume ukoo mzima yeye ndo angalau anajiweza, kwahiyo Kwa kidogo anachokipata anahakikisha hadi mtoto wa mjomba kule kijijini anapata sare za shule, anaenda kuoa mwanamke ambaye kwao wana hali ngumu kama ya huyu mwanaume, mwisho wa siku unajikuta unamzigo wa kuhudumia familia kama tatu hivi, yako, kwenu na Kwa mwanamke, hapo lazm tukuzike mapema.

Mifano iko mingi:
Naseeb Abdul mpenzi wake wa kwanza maarufu, wema sepetu Kwa kipindi kile alikuwa na utajiri na umaarufu kumzidi Naseeb,, Kila mtu anajua mchango wa wema kwenye safari ya Naseeb.

Huyu huyu Naseeb akawa kwenye mahusiano na Zari Hassan mpaka wakazaa watoto wawili, nadhan mlikuwa mnaona kwamba Naseeb alikuwa hatumii nguvu nyingi kwenye hili penzi Kwa sababu Zari Hassan hakuwa na njaa.

UKOO AU FAMILIA ALIYOTOKEA
Hii imekaa Kwa upana sana, kuanzia kibailojia mpaka kijamii,ni muhim kuchunguza nature ya familia unayoenda kuoa, aisee Kuna familia zinamatatizo sana, wengine wana mila na desturi za ajabu ajabu, wengine familia nzima ina historia ya kuachika zaidi ya mara tano, unakuta familia ina historia ya kutopata mtoto wa kiume na vitu ka hivo.
Kibailojia Kuna yale magonjwa ya kurithi, vitu kama sickle cell anemia, albinism, na vitu ka hizo ni muhimu kuangalia historia ya familia kwenye magonjwa ya kurithi.
Chunguza Kwa makini ujilizishe.

DINI YAKE
ukioa mwanamke ambaye hajashika dini, umeangamia, ielewe kama ilivyoandikwa, ukioa mwanamke ambaye hana hofu ya mungu we ukazingatia tu tako wakati umeenda kuoa umejila, nakuaidi.

UZURI WAKE
Mwanamke ambaye amejaaliwa uzuri anatamaniwa kuwa mke Kwa wanaume wengi.
Iko hivo yani, oa mwanamke mrembo, mwanamke mzuri, mwanamke anayekuvutia, hii itapunguza hata hizo tamaa za kuchepuka hovyo, yani nyumbani una bonge la kisu kiasi kwamba ule mda wa kazi unauona mwingi sanaaa, unataman kurudi nyumbani ukamuone.


Zingatia:
MWANAMKE ndoa ni majaaliwa

MWANAUME: usijichanganye.


#OneDayYouWillBeGone
Dr criminal

Sent using Jamii Forums mobile app
Lakin si huyu ndo alioa katoto la miaka 6. Sasa hapo kalikua na Mali Gani.
 
Lakin si huyu ndo alioa katoto la miaka 6. Sasa hapo kalikua na Mali Gani.
Mkuu huyo ni the great religional figure Kwa waislam, mi nimeleta mawazo yake tuyajadili, unavyomfanyia yeye attack badala ya mimi mtoa mada unaanzisha vita yakidini na hapa hatupo kujadili dini, tunajadili moja ya idea yake.kuwa makini mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mbona watu mnaendeshwa sana na hisia, mkuu husimu-attack mtume, hapa tunajadili idea yake hatubishani dini.

Sent using Jamii Forums mobile app
Kama unachagua wachangiaji na aina ya michango ungesema mapema. Hili ni jukwaa huru na hapo nimeongelea uhalisia unaohusiana na point katika mada yako.

Kinyume na hapo ungeliweka hili bandiko hapo nyumbani kwako.
 
[emoji523]
Screenshot_20221009-015346.jpg
 
Na disagree kabisa my dear .

Mwanamke ni kukuheshimu .
Kukupenda na kukujali mapenzi yake yaliyotoka moyoni nawewe ukaridhia ndio utajiri wa kutosha .

Uzuri ni sawa ila isiwe too much nayo ni kero heshima hakuna hapo anauwakika na ugali tofauti nawewe.

Kingine mwanamke anayejali na anaye onyesha upendo wa kweli .

Sasa wewe kawachanganye wenzio waislamu wengi wanajua kupenda vya buree sana tu kama hamjui .
Kumtunza wife labda awe na hela
 
Na disagree kabisa my dear .

Mwanamke ni kukuheshimu .
Kukupenda na kukujali mapenzi yake yaliyotoka moyoni nawewe ukaridhia ndio utajiri wa kutosha .

Uzuri ni sawa ila isiwe too much nayo ni kero heshima hakuna hapo anauwakika na ugali tofauti nawewe.

Kingine mwanamke anayejali na anaye onyesha upendo wa kweli .

Sasa wewe kawachanganye wenzio waislamu wengi wanajua kupenda vya buree sana tu kama hamjui .
Kumtunza wife labda awe na hela
[emoji1666][emoji1666]

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na disagree kabisa my dear .

Mwanamke ni kukuheshimu .
Kukupenda na kukujali mapenzi yake yaliyotoka moyoni nawewe ukaridhia ndio utajiri wa kutosha .

Uzuri ni sawa ila isiwe too much nayo ni kero heshima hakuna hapo anauwakika na ugali tofauti nawewe.

Kingine mwanamke anayejali na anaye onyesha upendo wa kweli .

Sasa wewe kawachanganye wenzio waislamu wengi wanajua kupenda vya buree sana tu kama hamjui .
Kumtunza wife labda awe na hela
Zikiguswa hela zenu dada zangu mnalalamika.
 
Hadithi imejikita zaidi kwa uwazi na ikamalizika kwa mtume kusema kua muoe yule mwenye DINI utabarikiwa

Nadhani hili ndilo la kuzingatia zaidi

Kama ninavyo fahamu majukumu kamili mwanaume ndiye anapaswa kumtimizia mkewe

Ila ata saidiwa na mke ikiiwa mume ana dharula ya kua labda mume hajiwezi ki mali

Lakini si kukaa na kutegemea mali ya mwanamke hapa utapata unacho kitafuta.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom