Mwanamke akikupenda, ni lazima afanye mambo haya

Carlos The Jackal

JF-Expert Member
Feb 6, 2017
23,911
70,850
Leo nimeona niwakumbuke ndugu zangu wanaopenda Mwanamke kwa Dhati ya Moyo na akili yao yote na hisia zao zote kuliko Kumpenda Bwana Yesu.

Sawa, eehh ndo umempata sasa , umwekeza Muda na Pesa zako na hisia zako, kiasi kwamba Unaamini HUYO MWANAMKE akiondoka ,basi utakufa.

Kabla HUJAFA , yajue haya mambo ili yakusaidie kufanya maamuzi ya kuanza kujiondosha kwenye shimo la Dhahama Matokeo yake unaishia kulia lia humu

MWANAMKE HUWA NI MSIKIVU SANA KWAKO NA ANAKUPA ATTENTION 100%. Ndiooo katika mazingira ya kawaida kabisa, wanawake ni Watu wa kuongea nasio kusikiliza , lakini mwanamke anayekupenda kutokea Ndani yake , Hufanya kinyume, yeye huwa msikilizaji zaidi kwako, unachoongea akakishika kwa umakini, hujali vitu vidogovidogo unavyomwambia , na hata ukija kumkumbusha , utaona anakumbuka vema, lkn huu usikivu unaenda mbali sana kiasi kwamba HUKUPA WEWE UTAWALA yaan unachokisema, hakibishiii ,hukifanya, akibishia BASI UJUE ANASABABU KUBWA TENA HABISHI KWA MANENO MACHAFU,BALI KWA MAELEKEZO........ huyo ulonaye Kameza CD ya midomo ya kizaramo ????? Au ...unajua mwenyewe !!!

DAIMA HUPIGANIA PENZI LAKE KAMA WAPENZI AU WANANDOA.
Yes kataaa kubali, Unlike Nasisi wanaume. Mwanamke Mwenye moyo wakupenda aliumbwa KUMPENDA MWANAUME MMOJA TU ,Ndiooo na anapokutana na huyoja alompenda, humpenda na humpigania, hawezi kuondoka kwako kwa sbabu za KIJINGA, Daima hupigana sana kuhakikisha Penzi linasonga mbelee ... Huyu anapochoka "Humlilia. Humwaga machozi ,Why G?? Why Carlos ?? I love you mbona hivo Baba ??? ..,... Kumbe Carlos mwenyewe Muhuni .

Je Mwanamke wako anakupigania au ndo kaamua " Ukisusa mwenzio anakula????"......unajua mwenyewe .

HUJIVUNIA SANA MAFANIKIO YAKO.
asikuambie MTU, mwanamke akupendaye , kwakua upo katika maisha yake ya kila siku, Furaha yake ni kuona unachanua kimaisha, unafanikiwa, na once unapofanikiwa unajivunia mbele yako au nje ya upeo wako , haishi kukutia nguvu na hamasaa ... Je demu wako huyo..anajivunia kwako??? Au demu wako ni "Maisha yako hayanihusi, nachotaka unitumie hela " poleee.

HUKUBALIANA NA MABADILIKO YA MAISHA YAKO ..
Ndiooooo asikuambie MTU bana, Ukiona umeyumba kimaisha na demu akabadilika basi jua HAKUWAHI KUKUPENDA hata punje, hakukupokea vile ulivyo,Bali alikupokea kwa kile ulichonacho... Mwanamke akupendaye toka ndan huyapokea mabadiliko unayopokea yawe Hasi, yawe Chanya, kichumi, kijamii n.k
...... Je demu wako ukikosa au unaposhindwa kumtumia sawa na alichoomba, Hufura kama katafuna mavi??? hukubali ??? Anakusupport na kukutia nguvu??? ...au ndo imeisha hiyo

HAWEZI FANYA MATUMIZI MABAYA YA PESA ZAKO......hili lieleweke hivyohivyo.

HUWAJALI WOTE UNAOWAPENDA...
Ndiooo asikudanganye Mwanamke et "Mama mkwe wengine hawafai ,sijui mawifi hawafai, sijui nn"..... Mamakee. PIGA CHINI CHAP....MWANAMKE anayekupenda atawapenda watu wote unaowapenda wewe, awe Mama, Baba, Ndugu zako n.k, Siku zote hujihisi FURAHA kuwatreat wapendwa wako kwan kwa kufanya ivo, hijihisi anakutreat wewe ....

Je demu /Mke ulonaye, Mara ya mwisho kukuulizia Wazazi wako, Ndugu zako, ilikua lini????? .

NYIE MWANAMKE AKIKUPENDA HUJITAHIDI AJULIKANE KWA NDUGUZO,FAMILIA, MARAFIKI NAJAMII YAKO....
.. Wee una dem au mchumba au njoo tuishi, hajawahi hata kutaka kujua kwenu ,hajali chochote ,hawajibiki kwa lolote kutaka ajulikane kwenu..... .... Acha kupoteza muda, BADILIKA nawee mcheze muziki mmoja wa kupotezeana muda.

HUJITOA KWA LOLOTE KUHAKIKISHIA UNA FURAHA MZEE...
unajuaga ile wanaiita Sacrifice?? Sasa Mwanamke akikupenda kindakindaki siku zote za maisha yake atajitahidi kwalolote kuhakikisha wee ni MTU wa FURAHA..yaan km alikua na tabia zinazokuirritate , ataziachaaaa Mara moja , kama kuna jambo kwake Lilikua zuri lkn kwako linakera ,ataliachaaa yaaan ATABADILIKA KUKUFAA, ATAHAKIKISHA HAKUPI SABABU ZA KUKOSWA FURAHA...sikiliza, ukiona una demu /mke HAKUPI AMANI Kila siku anakutengenezea mazingira ya kujiuliza uliza maswali kama Fala, na kuongea kama mjinga.... Huyo HAKUFAI.

Brooooo to be honesty about True relationship ukiona DEMU WAKO KWAKE ,HUYAHONI HAYO, BROOOO SIMAMA JUST LEAVE HER AND PURSUE YOUR DREAMS, ASPIRATIONS , GOALS AND GOD WILL BLESS YOU.

Utasikia maneno ya watu dhaifu "Et ooohhooo mwanamke anaweza kukupenda nabado asijue namna gan ya kukupenda ""

NB!!! For a Good relationship, both Men and Women must be Loving, Caring and not self seeking, neglecting etc.!!.
 
Wanawake wa wapi hao unaongelea , Hawa Hawa wanaendeshwa na pesa , ukiwa na pesa watapritend mpaka basi
Hawa hawa tulonao TZ na Duniani kwako Mkuu.

Utakua mzembe sana ikiwa utashindwa kujua matendo ya tabia ya mwanamke yako, ni yamaigizo au halisi.
 
Waefeso 5:22 Wake waheshimuni waume zenu kama mnavyomtii Bwana, … 5:25 enyi Waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa nafsi yake kwa ajili yake ili atakase, …5:28 vivyo hivyo Waume wawapende Wake zao kama miili yao. Anayempenda Mkewe anajipenda mwenyewe, …

Hakuna mahali palipo sema kwamba Mwanamke akupende, bali Biblia imesema Mwanamke amuheshimu mumewe na Mume ampende mkewe kama anavyojipenda mwenyewe.

Hivyo usiatafute kupendwa na Mwanamke Utaumia kwani Mwanamke hawezi kukupenda isitoshe wewe siyo mtoto, tafuta na pigania HESHIMA, got it ?
 
Leo nimeona niwakumbuke ndugu zangu wanaopenda Mwanamke kwa Dhati ya Moyo na akili yao yote na hisia zao zote kuliko Kumpenda Bwana Yesu.



Sawa, eehh ndo umempata sasa , umwekeza Muda na Pesa zako na hisia zako, kiasi kwamba Unaamini HUYO MWANAMKE akiondoka ,basi utakufa...
100% true, nina miaka 20 katika ndoa ,nimeona kama vile unamchambua mke wangu.
 
Waefeso 5:22 Wake waheshimuni waume zenu kama mnavyomtii Bwana, … 5:25 enyi Waume, wapendeni wake zenu kama Kristo alivyolipenda Kanisa akajitoa nafsi yake kwa ajili yake ili atakase, …5:28 vivyo hivyo Waume wawapende Wake zao kama miili yao. Anayempenda Mkewe anajipenda mwenyewe, …

Hakuna mahali palipo sema kwamba Mwanamke akupende, bali Biblia imesema Mwanamke amuheshimu mumewe na Mume ampende mkewe kama anavyojipenda mwenyewe.

Hivyo usiatafute kupendwa na Mwanamke Utaumia kwani Mwanamke hawezi kukupenda isitoshe wewe siyo mtoto, tafuta na pigania HESHIMA, got it ?
Mkuuu maandiko nayajua kwa kiasi chake, hata hayo uloandika pia niliwah yaandika.

UKWELI NIKWAMBA, SISI WANAUME TUNATAFASIRI HAYO YOTE +HESHIMA KAMA NDIO "MWANAMKE MWENYE UPENDO YAAN ANAYETUPENDA ".

ndio maana utasikia.." daah dem ananipenda kinyamaaaa........ Huwa hatusemi....Demu ananiheshimu kinyamaaa.
 
35 Reactions
Reply
Back
Top Bottom