Kipenzi Changu
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 58,035
- 134,292
Wanawake na watoto waliokuwa
wakishikiliwa mateka na kikundi
cha Kiislam cha Boko Haram
kaskazini mwa Nigeria
wamesema baadhi yao waliuawa
kwa kupigwa mawe na
wapiganaji wa Boko Haram
wakati jeshi lilipokaribia
kuwaokoa.
Walikuwa wakizungumza siku
moja baada ya karibu mateka
mia tatu kuokolewa kutoka msitu
wa Sambisa na kuwapeleka
katika kambi ya serikali.
Mwanamke mmoja ambaye
alijifungua akiwa mateka
ameelezea namna wapiganaji
hao walivyomkata koo mumewe
wake mbele yake, kabla
mwanamke huyo kutenganishwa
na watoto wake wengine
watatu.
Mwandishi wa Associated Press
ambaye aliotembelea kambi hiyo
amesema wengi wa watoto
waliokolewa walikuwa
wanaugua utapiamlo mkali.
Jeshi la Nigeria limesema
limewaokoa zaidi ya watu mia
saba katika kipindi cha wiki moja
iliyopita wakati wa mapigano
makali yanayoendelea dhidi ya
Boko Haram.
Source:BBC
wakishikiliwa mateka na kikundi
cha Kiislam cha Boko Haram
kaskazini mwa Nigeria
wamesema baadhi yao waliuawa
kwa kupigwa mawe na
wapiganaji wa Boko Haram
wakati jeshi lilipokaribia
kuwaokoa.
Walikuwa wakizungumza siku
moja baada ya karibu mateka
mia tatu kuokolewa kutoka msitu
wa Sambisa na kuwapeleka
katika kambi ya serikali.
Mwanamke mmoja ambaye
alijifungua akiwa mateka
ameelezea namna wapiganaji
hao walivyomkata koo mumewe
wake mbele yake, kabla
mwanamke huyo kutenganishwa
na watoto wake wengine
watatu.
Mwandishi wa Associated Press
ambaye aliotembelea kambi hiyo
amesema wengi wa watoto
waliokolewa walikuwa
wanaugua utapiamlo mkali.
Jeshi la Nigeria limesema
limewaokoa zaidi ya watu mia
saba katika kipindi cha wiki moja
iliyopita wakati wa mapigano
makali yanayoendelea dhidi ya
Boko Haram.
Source:BBC