MwanaKJJ Jumatatu: Mada 4 (kati ya nyingine) Zilizomfikisha Max Kizimbani

Binafsi sina shaka hata chembe kuwa kama kuna rafiki wa kweli katika vita dhidi ya ufisadi na ubadhirifu au dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka basi katika nchi yetu hakuna rafiki bora kama mtandao wa JamiiForums. Na hapa nasema nikiwa na maslahi kwani ni miongoni mwa waanzilishi wa mtandao huu.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com

Mzee wetu MMM kama kweli hili /hilo hapo juu ndiyo inayoweza kumweka ndani Max for a Week najua harakati ya Raisi ya majipu bado iko moto kiasi hiki na subiri kuona majipu ya maana kwa wote wanaozungukwa na kadhia hii. Nilikuwa na imani kubwa baada ya kusitishwa kwa uteuzi wa DCI. Ni kiona kuwa pengine ni maboresho lakini kuja kwa Kesi ya Max na hii hoja zako hapo juu nimebaki mdomo kufa ganzi. Kuna jambo haliko sawa.

Rais Magufuli atengua uteuzi wa DCI - Habari | Gazeti la Kiswahili ...
UrlAdvisorGoodImage.png

www.mwananchi.co.tz/.../Rais...atengua-uteuzi-wa-DCI/.../index.ht...
Translate this page
Oct 29, 2016 - Rais John Magufuli ametengua uteuzi wa Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI) Diwani Athuman.
 
Naona wengi mnaishia kusema ni polisi, polisi! Ukweli ni kuwa ni serikali yote. Labda mniambie kuwa tcra imehamishiwa wizara ya mambo ya ndani! 'roho' ileile iliyozuia mikutano ya hadhara, iliyozuia bunge kuonyeshwa live, inayofungia magazeti nk, ndiyo hiyohiyo isiyotaka kuiona Jamii Forums hewani. Ukweli ni kuwa serikali hii haitaki uhuru wa habari kwa raia wake.
[HASHTAG]#Free[/HASHTAG]MaxenceMelo.
 
Mbona sioni uhusiano hizo kesi na Ikulu, sasa wale wanaomtukana Rais, kua ndio amewatupa polisi.. Ahsante mwanakajiji
 
melo.jpg

Na. M. M. Mwanakijiji

Maxence Melo (pichani) mmoja wa waasisi wa mtandao maarufu wa kijamii wa JamiiForums amefikishwa kizimbani wiki iliyopita baada ya kukataa kufichua taarifa ambazo zingewatambuliwa waandishi wa mada kadhaa kwenye mtandao huo; mada ambazo Serikali ingependa kujua ni nani alizianzisha. Kukataa kwa Max hakukuja kwa sababu ya kiburi bali kile ambacho amekidai kuwa ni kutokuwa na uwezo wa kujua ni nani ameandika kitu gani kwenye mtandao huo kwani teknolojia inayoendesha baraza (forum) hilo la mijadala haimpi uwezo au nafasi hiyo. Asubuhi hii Max anatarajiwa kufikishwa tena kizimbani na ni matarajio yetu kuwa ataachiliwa huru na baadaye kesi zote dhidi yake kufutuliwa mbali kwani ni za kuunga unga na ambazo hazina ushahidi wa kuweza kushinda mbele ya chombo huru kama cha mahakama.

Zama Mpya iliamua kwenda kuchimba ndani zaidi kujua ni mada gani hasa ambazo zimeifanya serikali imlaze ndani kwa karibu wiki nzima Max, mume na baba wa watoto watatu. Tangu sakata hili lianze ZM imejaribu kufuatilia kwa kina kutaka kujua serikali inataka kumjua nani hasa na kwanini kutoka katika mtandao huo.

Uchunguzi wetu umeonesha kuwa kuna mada kadhaa ambazo serikali ilimtaka Bw. Melo kuwapatia taarifa za waanzilishi wake; kwanza kwa hiari yake tu lakini baadaye kwa kulazimishwa chini ya tishio la kufikishwa mahakamani chini ya Sheria ya Uhalifu wa Mitandao. Hapa chini nitazitaja ambazo zinaonekana ni kuu; kuna nyingine sijaziangalia kwa undani wake. Lengo ni kutaka watu wajue ni nini hasa kinachotafutwa na kama kweli kinastahili kutafutwa.

Polisi walianza kudai kutoka kwa JamiiForums taarifa mbalimbali za waanzilishi wa mada mbalimbali kuanzia Januari mwaka huu kupitia Idara ya Upelelezi ya Jeshi hilo. Kuanzia wakati huo Idara hiyo imetuma barua mbalimbali za kutaka taarifa kutoka kwa JamiiForums katika kile ambacho Polisi walidai kuwa kupatiwa kwao taarifa hizo kutasaidia katika uchunguzi mbalimbali unaondelea.

Mada Kuhusiana na Kampuni ya CUSNA Investment na Madai ya Ukwepaji Kodi

Kuanzia mwishoni mwa mwaka jana jina la kampuni hii lilianza kutajwa tajwa kwenye mtandao wa JamiiForums. Kufikia Februari mwaka 2016 jina hili lilikuwa limetoka uchochoroni na kufika katikati ya jiji kwa kutajwa katika mada mojawapo kuwa ni miongoni mwa makampuni yasiyolipa kodi huko Bandarini. Mada hii kuna mtu aliyekuwa anachangia mara kwa mara ni wazi mtu huyo aliwaudhi watu fulani huko CUSNA ambao waliamua kushtaki ili mtu huyo ajulikane. Polisi wakaingilia kati. Pamoja na hilo kampuni hii na nyingine zilizotajwa ilikuwa ni miongoni mwa makampuni zaidi ya 200 ya uingizaji na utoaji mizigo bandarini ambayo yalifungiwa kwa muda na TPA kupitia tangazo lake la Februari 9 mwaka huu kwa kushindwa kuwasilisha vielelezo mbalimbali.

Mwezi mmoja hivi baadaye Serikali iliyafungulia baadhi ya makampuni haya na pia kumuagiza Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Serikali (CAG) kufanya ukaguzi kati ya Bandari na CRDB. “Kimsingi bado liko tatizo baina ya Mamlaka ya Bandari pamoja na Benki ya CRDB. Naona kila mmoja hapa anamkana mwenzake. Nitamtuma CAG ili akafanye ukaguzi wa kina ili tujue ni nani kati yao amehusika na upotevu wa fedha” Waziri Mkuu Majaliwa aliyasema hayo katika kikao chake na mawakala wa Forodha mwezi Machi jijini Dar-es-Salaam.

Tuhuma za Ufisadi Benki ya CRDB

Mada nyingine kadhaa zinazohusiana na Benki ya Ushirika na Maendeleo Vijijini (CRDB) zilivuta pia ushirika wa polisi baada ya polisi kutaka kujua watu waliojaribu kufichua kile walichokuwa wanaamini kuwa ni ufisadi. Polisi waliiandikia JF barua kutaka kupewa taarifa za watu walioibua sakata hilo ili watu hao waweze kushtakiwa chini ya kifungu cha 16 cha sheria ya uhalifu wa mitandao. Kifungu hicho kinahusiana na uchapishaji wa taarifa ambazo si za kweli, zenye kupotosha au ni za uongo. Hata hivyo, haijulikani ni kwa namna gani polisi walijua kuwa kilichochapishwa si cha kweli.

Mada hiyo iliyoanzishwa tangu 2012 imeendelea kuwa ya moto hasa kwa watu kugawanyika. Wapo ambao kwa maneno makali sana walimtaka Mkurugenzi wa CRDB Bw. Kimei ajiuzulu kwa sababu kadha wa kadha huko wengine wakimtetea. Hata hivyo, inaonekana maneno mengi hasi dhidi yake yalisababisha taarifa kutolewa polisi na kutaka hasa kuwajua ni kina nani waliokuwa wanatoa taarifa mbalimbali kuhusiana na CRDB na madai mbalimbali dhidi ya benki hiyo. Polisi wakataka JF iwapatie taarifa za watu hao.

Wizi wa Mafuta Bandari na OilCom Kudaiwa Kukwepa Ushuru

Mojawapo ya mada nyingine ambazo nazo zilisababisha faili lifunguliwe polisi ni ile iliyodai uwepo wa wizi wa mafuta bandari. Polisi nao walitaka kumjua mtu aliyeanzisha mada hizi alikiri mara moja kuwa alishapokea vitisho kwenye sanduku lake la jumbepepe. Hata hivyo alionesha kitaalamu kile alichoadia ni mchezo mchafu unaochezwa kuwezesha ukwepaji ushuru akiituhumu kampuni ya Oilcom. Kuna mada nyingine (mwanzilishi mwingine) ambayo nayo inaonesha jinsi gani pale Uwanja wa Ndege wanashirikiana kuiba mafuta ya ndege.

Kutajwa kwa Aliyekuwa Waziri Charles Kitwanga na Vicky Kamata Malipo Benki Kuu

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Bw. Charles Kitwanga alitajwa kuwa yeye alikuwa ni mmoja wa watu ambao walikuwa bado wanalipwa na Benki hiyo. Pamoja naye pia Mbunge wa Viti Maalumu Bi. Vicky Kamata naye alitajwa. Ilikuwa ni taarifa ambayo haikuwa na maelezo mengi lakini kwa vile ilimlenga mtu aliyekuwa Waziri ni wazi ilivuta hisia za watu mbalimbali hasa wakati ambao Kitwanga alikuwa anatajwa pia katika ile kashfa ya Lugumi na hivyo watu wengine nao wakaona kama hawezi kuondoka na Lugumi basi aondoke na hii kama ni kweli.

Hata hivyo, Wizara ya Mambo ya Ndani ilitoa taarifa kwa umma kukanusha habari hiyo na kuwa iliwataka watu walioisoma waipuuzie na bila ya shaka watu wengi makini waliipuzia kwani taarifa ya wizara ilijenga hoja ambayo mwanzisha mada ile hakuweza kujibu. Na suala hilo likafa. Lakini kwa vile ilikuwa inamhusisha mtu anayesimamia jeshi la polisi basi kuna uwezekano kulikuwa na kiu ya kutaka kumjua huyo mtu aliyejaribu kumchafua Waziri.

Mada hizi ni kubwa zaidi ambazo zinaonesha ni aina gani ya taarifa ambazo zinatafutwa. Ni mada ambazo Jeshi la Polisi liliandika barua kwa Max kumtaka alipatie taarifa. Ni wazi kuwa serikali kupitia jeshi la polisi halitafuti taarifa kutoka kwa Max kwa ajili ya kupambana na uhalifu bali zinatafuta taarifa za watu waliojitoa muhanga kujaribu kutoa taarifa za kile wanachokiona kuwa ni kitendo kiovu au uhalifu katika mazingira yao ama ya kazi au ya karibu yao. Ni sawa na mtu aone mtu anajaribu kuvunja mlango wa jirani na anajua siye jirani na akaita polisi. Mtu yule anayevunja alipoona hivyo anakimbia polisi kudai kuwa anadaiwa kuvunja nyumba ya jirani wa mtu na kuwa taarifa hizo ni kweli. Badala ya polisi kuangalia ukweli wa jambo hilo wanatoka kwenda kumkamata jirani aliyetoa taarifa za kitendo cha uhalifu! Na kwa vile hawamjui ni jirani gani wanamkata mwenyekiti wa mtaa kwa kushindwa kumtaja jirani aliyejaribu kufichua uovu!

Swali kubwa ambalo linahitaji kuulizwa ama na polisi au na viongozi wetu ni nani hasa atakayenufaika endapo watu wataogopa kuibua maovu kwenye ofisi za umma au hata za binafsi? Watu wakiogopa kuita polisi wakiona jambazi anapanga njama kwenda kuiba benki nani anafaidika? Au kama wanamjua mtu anayecheza mchezo na majambazi kule Benki je wawe na ujasiri wa kutoa taarifa polisi? Je, Watanzania ambao wameona kuwa kuna serikali inayojaribu kupambana na ufisadi na imedai kuwa haimuogopi mtu sasa inawafuatilia waibua maovu badala ya kufuatilia madai ya uovu yanayotolewa wafanye nini? Je, watu wakiogopa kuja tena kwenye mitandao ya kijamii, wakiogopa kabisa kuingia JamiiForums na kudokeza kitu kiovu walichokiona je Serikali itaweza vipi kujua?

Siyo kwamba mara nyingi serikali imekuwa ikitoa wito kwa watu wakiona uhalifu au kitu wanachohisi ni uhalifu watoe taarifa na wakati mwingine tena wanasema watoe taarifa hata bila ya kujulikana (anonymously)? Je, hilo linatofauti gani na mtu kuingia kwenye JamiiForums au mtandao mwingine na kusema “Ofisini Kwangu kuna Wizi wa Fedha za Umma” Je, mtu huyo sasa atakuwa salama? Je, kama ni makossa kutoa taarifa za uhalifu kwa kujificha polisi bado inataka watu ni lazima watambulikane wanapotoa taarifa za uhalifu hata kama kwa kufanya hivyo kunaweza kusababisha watu hao wafanyiziwe (retaliation)?

Je, kila atakayetajwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa anahusika au anahusiana na uovu fulani ambao umma unahitaji kujua atakimbilia polisi kujaribu kunyamazisha na polisi bila kuwa na uthibitisho wowote wanamkubalia tu kuwa anasema kweli na wanaenda kuwatafuta “waliomchafua”? Kwanini sheria yenyewe isifanyiwe mabadiliko ili mtu anayedai amechafuliwa kwenye mitandao ya kijamii au kampuni inayodai kutajwa vibaya ni lazima ioneshe upotofu kwa vidhibiti ambavyo vinaweza kutumika mahakamani badala ya kudai tu kuwa “JamiiForums wamenichafua au wamesema Uongo” bila hata kuulizwa uongo hasa ni nini na ushahidi ni upi?

Je, kama JamiiForums itaamua kufunga shughuli zake na kuufunga mtandao mzima kwa hofu kuwa watu wataposti vitu vya uongo, vyenye makosa au vinavyoweza kumchafua mtu ni nani hasa atafaidika na kutokuwepo kwa Mahalia mbapo watu wanaweza kuzungumza kwa uhuru bila hofu ya kutafutwa na polisi? Na nani atadhurika ikiondoka?

Binafsi sina shaka hata chembe kuwa kama kuna rafiki wa kweli katika vita dhidi ya ufisadi na ubadhirifu au dhidi ya matumizi mabaya ya madaraka basi katika nchi yetu hakuna rafiki bora kama mtandao wa JamiiForums. Na hapa nasema nikiwa na maslahi kwani ni miongoni mwa waanzilishi wa mtandao huu.

Niandikie: mwanakijiji@jamiiforums.com
Hawa poliCCM mimi nawaona kama wendawazimu. Ni rahisi kumpa nguruwe ushahidi wa mihogo kuliko kuwapa polisi taarifa za wanachama wasiokuwa na hatia. Kwanini wasitumie intellijensia yao kufanya uchunguzi badala ya kutaka kuwatesa watu na kuwafunga kwenye viroba? Juzi tumeshuhudia watu wakielea mtoni halafu leo tena wanatafuta taarifa za watu wengine zaidi? Tuwaeleweje? Yana mwisho haya.
 
Nakuunga I mkono maneno yako kabisa hawa polisi ndio wanalinda sheria lakin kwa bahat mbaya wao wanapewa bunduki kulinda viongozi sasa nn tutegemee hapo
 
Mwanakijiji..Hayo uliyoyaandikaa ni mojawapo.kati ya meengi.Police waliyataka hayo.Ila Tabu ilikuja zaidi MTU mmoja alipoanza kucholozwa.Sasa Kiuhalisia hawawezi.sema Tumetumwa.Wameanza na Stata.Kufichua Maovu ndani ya JF hakujaanza Leo..Why owe hivi ghafra??Think Big.

Sent from my Solar 5 using JamiiForums mobile app
 
Ni sehemu mhimu kwa Usalama wa Taifa kupata taarifa za Mwanzo, lakini kama ndo zile serikali ovu zitaitupilia mbali JF.
 
Daaaah! Bora Rizi angeimbiwa ongea na Mshua sasa huku Jonas mwenyewe Tu kafichwa
 
Wakati tumesimama imara kuing'oa ccm madarani wenzetu kwa kujiona ni magenious mkazisaliti harakati na kuipigia debe ccm irudi madarakani na kampeni zenu zilishinda hongereni sana.

Wenye akili timamu tulijuwa vyema adui yetu si Lowasa bali ni ccm, mmeanzisha mahakama ya mafisadi leo mnatuambia mahakama haina wateja wakati fisadi Lowasa yupo hai na anadunda tu uraiani mnasubiri uchaguzi ujao muanze tena kuwalaghai wajinga kwa hoja zenu zilezile za kipuuzi.

MM tubu kwanza muombe msamaha kwa jamii ili mpate utakaso mpya kuliko kuja na hoja chanya huku ukijisahaurisha ni nyinyi ndio mmewasababishia Watanzania mateso haya kwa sababu tu ya personal interest zenu.

Hii ni laana, bila kutubu makosa yenu hamtokuwa na amani kamwe.
Umenena vyema mkuu....hawa ndumilakuwili hawatakiwi kabhisaa.....hapo anatajataja watu binafsi wkt mbaya anajulikana ni yule mfalme juha
 
This is deep kama watu wanaotoa siri zebye maslahi wanatafutwa kwa ajili ya kufanyiwa "Extinction"
 
Mzee Mwanakijiji umetumia akili sana kuhamisha goli na kwa mihemko ya watu wapo watakaoamini maneno yako. Asiyeitaka JF kuwa hivi ilivyo tunamjua na wala hao uliowataja si wahusika. Inawezekana mada za kuombea kuwajua watu ni hizo lakini hao watu wamechangia mada hizo tu?

Hoja yangu inawezekana wakiwajua kupitia mada hizo ndiyo wamewajua na kwenye "zile" mada nyingine zinazomkera yule mwenye mamlaka ya kuelekeza Kesi kufunguliwa kwa mahakimu watatu tofauti ili Maxence asipate dhamana. Huwezi kusema ni mada hizo ndiyo chanzo cha msuko suko wote huu!!

Kweli kabisa Mkuu. Rais alishasema anatamani malaika washuke waje waifute mitandao ya kijamii Mwanakijiji anataka kutuaminisha kuwa tatizo ni police na wakina Kimei. Yaliyomtokea Max yasingemtokea kama Magufuli angekuwa upande wa uhuru wa habari. Ni dhahiri yaliyomtokea Max na JF yana baraka kutoka juu. Ni vile tu Rais hajui ataifutaje mitandao ya kijamii bila kujichafua, vinginevyo angeshaifutilia mbali.
 
Tanzania letu Tanzania hatuna upande wenye nafuu, wote ni wapiga deal si CCM wala huko upinzani. Tatizo kubwa viongozi wetu walishanunuliwa na matajiri. Hata CDM wangekuwa ikulu leo hii tungekuwa tunaongelea mambo haya haya maana watu ambao wangechukua ofisi ni makada wa CCM ambao walihamia upinzani. Whether you like it or not hii ndiyo hali halisi. Kama unategemea kuna mwanasiasa anayekujali wewe na familia yako inabidi uende kwa mganga akakutibu maana utakuwa unaumwa dege dege.
Mkuu issue hapa ni balance of power
Unajua "invisible hand"?
 
Kwa Karne hii ya technologia kutaka kufungia social networks ni ujuha. Tutapashana habari kupitia mitandao ya nje ya nchi na huko tutaona kama polisi watakuja kuamua upekuzi. Polisi baada ya kushukuru, wamerahisishiwa kazi ya uchunguzi, badala yake wanawaandama watoa taarifa. Kweli tanzania ni zaidi ya ujuavyo.
 
Back
Top Bottom