Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,478
- 39,997
Kuna msemo wa Kiswahili kwamba Aliyeumwa na nyoka, akiona unyasi anashtuka; msemo huo unafanana maudhui yake na ule wa Kiingereza kuwa Once beaten, twice shy. Misemo yote hii miwili inatukumbusha tu kuwa mtu yeyote aliyefikwa na jambo baya; na hasa jambo ambalo hakulitegemea kabisa basi anakuwa mwoga hasa mazingira yale yale yanapotokea tena kwani anaweza kuhisi jambo lile lile baya linaweza kumtokea tena.
Hili linanikumbusha mojawapo ya michango mikubwa ya Rais Kikwete katika mijadala ya kisiasa na lugha nchini ni pale alipoelezea wakati fulani jambo ambalo lilikuwa kama kichekesho lakini hadi leo limekolea ndani ya hoja za lugha zetu. Ni pale alipowahi kuhutubia huko nyuma na kuwaasa Watanzania kuwa wawe waangalifu kama alivyokuwa Mbayuwayu ambaye alipewa ushauri na ndege Gong’ota na ushauri ule kama angeusikiliza ungekuwa mwisho wake. Kwamba, Mbayuwayu alimuuliza huyo ndege jinsi gani anaweza kutoboa miti kwa midomo yake. Gong’ota akamwambia kuwa inabidi aruke kwa kasi halafu agonge mdomo wake kwenye jiwe mara mbili ndio utakuwa na uwezo wa kutoboa miti. Mbayuwayu akakubali na akaenda kuchukua kasi alipokaribia lile jiwe akajiuliza nini kitamkuta akigonga jiwe; akaona ule ulikuwa ushauri mbaya na hivyo akajisemea “akili za kuambiwa changanya na za kwako”.
Swali langu la leo lina lengo la kujenga hoja tu kwamba huku tunakokwenda kuna watu wanaweza kabisa kutuambia kuwa jinsi ya kutoboa miti ni lazima tugonge midomo yetu kwenye mawe; na wapo ambao kati yetu wako tayari kuanza kuruka kasi na wamejipanga kura kasi kwenda kugonga jiwe ili wawe na uwezo wa kutoboa miti. Swali ni je watachanganya na za kwao?
Kuna watu ambao wanampinga Magufuli na ambao wanaamini kabisa kuwa Magufuli anaunda utawala wa kidikteta na wengine wanatumia hata neno “ufashisti”. Wapo ambao wanasema hivi wakiwa wanaongozwa na misimamo ya ndani kabisa (conviction) na hawafanyi hivi kwa sababu ya siasa. Yawezekana wengi wa hawa ni watu ambao kweli wanasema kwa sababu wanaamini katika wanachokisema. Hawa sina tatizo nao kwani wanaongozwa na imani na misimamo yao.
Kwa wale ambao hawachoki kusoma hoja ndefu UNAWEZA KUSOMA HAPA.