Habari zenu nyote...! Rest In Peace
Nelson Olotu.
Napenda kuchukua nafasi hii kuwapa pole familia ya Mzee Olotu iliyopoteza kijana wao mpendwa kwenye ajali ya ndege iliyotokea hivi majuzi hapa. Poleni sana wafiwa kwa kumpoteza ndugu yetu Nelson.
Lakini pia Nelson alikuwa ni mmoja kati ya mwanajamii mwenzetu hapa JamiiForums tangu mwaka 2013, hivyo basi wanajamii tunasikitika kumpoteza member mwenzetu akiwa bado anahitajika kwa kiasi kikubwa kabisa katika jamii yetu hii.
Nikiwa kama member mwenzake nachukua nafasi hii kwa niaba ya Uongozi mzima wa JamiiForums na kwa niaba ya members wote wa JF kutoa pole kwa familia ya wafiwa na tunawaombea MUNGU awatie nguvu sana katika kipindi hiki kigumu cha msiba. AMEN.
BWANA AMETOA NA BWANA AMETWAA. JINA LA BWANA LIHIMIDIWE. MUNGU AKULAZE MAHALI PEMA NDUGU YETU NELSON OLOTU. AMEN.
Pia soma
Ndege ndogo ya Shirika la Auric Air imepata ajali leo Jumatatu asubuhi Septemba 23, 2019 katika uwanja mdogo wa ndege eneo Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania. Ajali hiyo imetokea saa 1:30 asubuhi ambapo ilikuwa ikiruka kutoka Serengeti kwenda Arusha baada ya...
Imagine, ajari ya ndege imeua wawili ila ndege ya serikali imebeba mwili wa mtu mmoja na mwengine atabebwa na ndege nyingine kwa uchunguzi zaidi, Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii habari sasa imebadilika kutoka ajari ya ndege haki kua Mabeyo afiwa na mwanae na viongozi wanaenda kutoa...