haszu
JF-Expert Member
- Oct 10, 2017
- 837
- 1,550
Imagine, ajari ya ndege imeua wawili ila ndege ya serikali imebeba mwili wa mtu mmoja na mwengine atabebwa na ndege nyingine kwa uchunguzi zaidi,
Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii habari sasa imebadilika kutoka ajari ya ndege haki kua Mabeyo afiwa na mwanae na viongozi wanaenda kutoa pole huko.
Watanzania tuna double standard sana. Na yeye aliekufa pia ni binadam kama uyo wa mku wa majeshi,
===================================
Vyombo vya habari na mitandao ya kijamii habari sasa imebadilika kutoka ajari ya ndege haki kua Mabeyo afiwa na mwanae na viongozi wanaenda kutoa pole huko.
Watanzania tuna double standard sana. Na yeye aliekufa pia ni binadam kama uyo wa mku wa majeshi,
===================================
Baada ya ajali kutokea ilitangazwa kuwa waliofariki ni rubani na abiria mmoja. Baadaye ikatangazwa kuwa rubani aliyefariki ni mtoto wa Mkuu wa Majeshi Gen. Mabeyo. kuanzia hapo vyombo vya habari vyote vikajaa habari na picha za mtoto wa CDF kufa ajalini.
Muda si muda tukaanza kuona viongozi mbali mbali kuanzia rais wakimininika nyumbani kwa CDF kumpa pole. Viongozi mbali mbali wa upinzani nao hawakukosekana katika msafara huo. Baadhi ya taasisi na mashirika yakaanza kutoa salamu maalumu za pole kwa CDF kwa kuchapisha magazetini na kwenye mitandao ya jamii.
Yule aliyeitwa abiria baadaye tukaambiwa alikuwa ni rubani mwanafunzi/msaidizi. Vyovyote iwavyo hakuna aliye hangaika na habari zake katika mlolongo wa nilio wataja hapo juu. Vyombo vya habari na mitandao mingi ya kijamii imejaa habari za kifo cha mtoto wa CDF tu huyu mwingine kutoka katika familia ya wanyonge ambao rais huwa anajitambulisha kuwa ni rais wao, hasikiki kabisa na unaweza weza kudhani katika ajali ile alikufa mtoto wa Mabeyo tu.
Hakika hii ni aibu. Walikufa pamoja sasa imekuwaje mmoja anaonekana ndiye marehemu zaidi ya mwenzake? Hii ni aibu kubwa kwa vyombo vyetu vyote vya habari kwa kutoa coverage kubwa kwa mtu mmoja wakati walioathirika walikuwa wawili. Viongozi nao kuanzia namba moja wajithamini namna walivyolichukulia suala hili
View attachment 1215690
View attachment 1215691
View attachment 1215693
Wakamsahau mnyonge!
Pumzika kwa AMANI mnyonge mwenzetu nasi tupo nyuma yakoo😭😭😭😭
Vigogo mtupishe kidogo nasi tumfariji mnyonge mwenzetu😭😭😭😭
RIP bro naona wanamkumbuka wa mabeyo tu kwa kuwa baba Ni mkuu wa wajeda😠
View attachment 1215683