Ndege yaanguka hifadhi ya Serengeti Tanzania, yaua wawili akiwepo mtoto wa CDF Jenerali Mabeyo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
Ndege ndogo ya Shirika la Auric Air imepata ajali leo Jumatatu asubuhi Septemba 23, 2019 katika uwanja mdogo wa ndege eneo Seronera ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.

Ajali hiyo imetokea saa 1:30 asubuhi ambapo ilikuwa ikiruka kutoka Serengeti kwenda Arusha baada ya kushusha watalii.

Katika ajali hiyo, rubani na abiria mmoja wamefariki dunia.

Kamishna Msaidizi mwandamizi wa shirika la Hifadhi za Taifa (Tanapa), Pascal Shelutete akizungumza na Mwananchi amethibitisha kutokea ajali hiyo. "Tunatoa taarifa zaidi baadaye kwani sasa kazi inayoendelea ni kuokoa vitu na kuhifadhi miili," amesema.

EFJT-BbXoAI7hEy.jpg

MAONI YA MDAU
CDF Mabeyo kapoteza kijana,bwana mdogo kabisa Captain Nelson Mabeyo.Ninadhani suala la uzoefu linahusika hapa.Huyu kijana alikuwa mdogo sana kumuachia chombo peke yake,hasa katika viwanja korofi na vyenye changamoto kama vya huko mbugani Seronera,endapo kama atakuwa alikuwa peke yake akifuata abiria

Haya mashirika madogo ya ndege,sababu ya kutaka faida za haraka wanakuwa wanaumia rubani mmoja ili kupunguza gharama na kuongeza faida,lkn ukweli ni kuwa kiutaratibu hata ndege hizi ndogo zinahitaji marubani wawili.

Unapompa kijana kama Nelson ndege arushe peke yake,tena kwenya viwanja vya mbugani ambapo unaweza kuwa umeachia kila kitu unatua,mara twiga anakatiza au unakuta simba anaota.jua la asubuhi kwenye runways unahitaji kuwa mzoefu ku-abort na kurudi hewani,hii inakuwa rahisi kama marubani wanakuwa wawili na mmoja mwenye uzoefu wa kutosha.

Ninatoa changamoto kwa TCAA,kusisitiza haya mashirika yanayomiliki hizi ndege ndogo kuhakikisha wanakuwa marubani wawili,hasa huko porini,na kama bwana mdogo itadhibitika aalikuwa rubani peke yake bila first officer,basi watu wawajibike.

Lakini pia isiwepo ile dhana kuwa huyu ni Mtoto wa shangazi dada yake IGP,hasa anapokosea kwenye nidhamu ya usafiri wa anga basi aogopwe kuadhibiwa kwasababu ya jina la mjomba wake.

Nelson Mabeyo has gone while he is too young...R.I.P young fella

Mtoto wa mkuu wa majeshi Tanzania afariki ajali ya ndege

Nelson Mabeyo, mtoto wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini Tanzania (CDF), Jenerali Venance Mabeyo ni miongoni mwa watu wawili waliofariki katika ajali ya ndege ya Kampuni ya Auric iliyotokea leo asubuhi Jumatatu Septemba 23, 2019.

Nelson ndio alikuwa rubani wa ndege hiyo iliyoanguka katika uwanja mdogo wa ndege wa Seronera uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania.

Ndege hiyo ilianguka saa 1:30 asubuhi wakati ikipaa katika uwanja huo kwenda mkoani Arusha.

Habari za uhakika kutoka mamlaka ya viwanja wa ndege imeeleza kuwa Nelson aliondoka na ndege hiyo jana katika uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Dar es Salaam.

Akizungumza na Mwananchi katika uwanja wa ndege wa Soronera, Msimamizi wa Kampuni ya Auric, Peter Kimaro amesema Nelson amefariki katika ajali hiyo akiwa na Nelson Orutu ambaye ni rubani mwanafunzi.

“Baada ya kuhakiki na kuona ndege iko sawa na kuruhusiwa kuruka kwenda Gurument kuwachukua wageni kuwapeleka KIA (Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro), walipoingia na kuondoka na mimi nikajua wako sawa,” amesema na kubainisha kuwa Nelson ni mtoto wa mkuu huyo wa majeshi.

Amesema baada ya kuona ndege imeshika mwendo kisha ikapaa kidogo, badala ya kunyooka juu ikakata kona, “na mimi nikashangaa kuona vile kisha ikagonga choo cha uwanjani na kuanguka na wote walifia ndani ya ndege.”

Amesema jeshi la zima moto na uokoaji waliwahi kuzima moto na miili imehifadhiwa katika Zahanati ya Soronera ikisubiri utaratibu mwingine.

-------
Helikopta ya JWTZ yatua Serengeti kuchukua mwili wa mtoto wa Jenerali Mabeyo

jwtz+pic.jpg
Helikopta ya Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) imewasili uwanja wa ndege wa Seronera uliopo ndani ya Hifadhi ya Taifa ya Serengeti nchini Tanzania kwa ajili ya kuuchukua mwili wa Nelson Mabeyo.

Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Nurdini Babu amesema helikopta hiyo imeelekezwa ichukue mwili mmoja wa mtoto huyo wa Mabeyo na mwili wa Orutu aliyekuwa naye utabaki kusubiri ndege nyingine itakayokwenda Serengeti ikiwa na wataalamu wa masuala ya anga kwa ajili ya uchunguzi wa ajali hiyo.

RAIS MAGUFULI AFIKA MSIBANI NYUMBANI KWA CDF JENERALI MABEYO
Nelly.jpg

Rais Magufuli akiwa na CDF Jenerali Mabeyo

Nelson.jpg

Rais Magufuli akimpa pole mama mzazi wa Nelson Mabeyo​
 
CDF Mabeyo kapoteza kijana,bwana mdogo kabisa Captain Nelson Mabeyo.Ninadhani suala la uzoefu linahusika hapa.Huyu kijana alikuwa mdogo sana kumuachia chombo peke yake,hasa katika viwanja korofi na vyenye changamoto kama vya huko mbugani Seronera,endapo kama atakuwa alikuwa peke yake akifuata abiria

Haya mashirika madogo ya ndege,sababu ya kutaka faida za haraka wanakuwa wanaumia rubani mmoja ili kupunguza gharama na kuongeza faida,lkn ukweli ni kuwa kiutaratibu hata ndege hizi ndogo zinahitaji marubani wawili.

Unapompa kijana kama Nelson ndege arushe peke yake,tena kwenya viwanja vya mbugani ambapo unaweza kuwa umeachia kila kitu unatua,mara twiga anakatiza au unakuta simba anaota.jua la asubuhi kwenye runways unahitaji kuwa mzoefu ku-abort na kurudi hewani,hii inakuwa rahisi kama marubani wanakuwa wawili na mmoja mwenye uzoefu wa kutosha.

Ninatoa changamoto kwa TCAA,kusisitiza haya mashirika yanayomiliki hizi ndege ndogo kuhakikisha wanakuwa marubani wawili,hasa huko porini,na kama bwana mdogo itadhibitika aalikuwa rubani peke yake bila first officer,basi watu wawajibike.

Lakini pia isiwepo ile dhana kuwa huyu ni Mtoto wa shangazi dada yake IGP,hasa anapokosea kwenye nidhamu ya usafiri wa anga basi aogopwe kuadhibiwa kwasababu ya jina la mjomba wake.

Nelson Mabeyo has gone while he is too young...R.I.P young fella
 
hapana idawa inaposemwa "Captain" kwa hapa,sio ile ya cheo cha kijeshi,bali ya "Urubani".Kwa sababu baba yake ni CDF,sio kuwa na yeye ni mwanajeshi.Sidhani hata kama alikuwa na miaka 25 ya kuzaliwa.Ndio last born wa mzee...Ukiwa mpenzi wa kunywa kwenye bar ya Mzee pale Tabata,utamfahamu bwana mdogo.Mpole na mwenye nidhamu kipenzi sana cha Mama yake
 
dah aisee pole nyingi kwa familia yake na kamanda kwa wakati huu mgumu.
 
hapana idawa inaposemwa "Captain" kwa hapa,sio ile ya cheo cha kijeshi,bali ya "Urubani".Kwa sababu baba yake ni CDF,sio kuwa na yeye ni mwanajeshi.Sidhani hata kama alikuwa na miaka 25 ya kuzaliwa.Ndio last born wa mzee...Ukiwa mpenzi wa kunywa kwenye bar ya Mzee pale Tabata,utamfahamu bwana mdogo.Mpole na mwenye nidhamu kipenzi sana cha Mama yake
Inasikitisha sana,napenda sana kuvisit kwenye hiyo bar hapo segerea,kwenye hiyo kipande korofi iliyowekwa lami maridhawa,mungu aifariji familia hii,a coolest charming for everyone family.
 
Back
Top Bottom