MwanaJF mwenzetu aliyefariki kwenye ajali ya Ndege, Nelson Olotu apumzike kwa amani

Hivi ni kwanini Marubani wengi nchini Tanzania ukifuatilia ' Background ' zao utakuta 99.9% wanatoka Familia za Kitajiri ( zinazojiweza Kiuchumi ) na siyo zile tutokazo akina An Eagle a.k.a Unga Robo Families? Kuna Mtu Mmoja nimemuuliza Ada ya chini kwa mwaka katika Vyuo vya Urubani kwa Afrika kaniambia ni Tsh 45 Milioni huku vile vya Ulaya / Marekani Ada yao huwa ni kati ya Tsh 90 Milioni hadi Tsh 120 Milioni kwa mwaka. Sasa sijui hapa aliniokota ( alinidanganya ) tu au labda alikuwa sahihi.

Nadhani wapo wataalamu wa haya mambo humu wanaweza kuja kutupa ABC mkuu...!
 
Hivi ni vigezo gani vimetumika kusema hii ID ni ya marehemu ?
Hakuna kina Nelson Olotu wengine ?

Haya mambo hayapo Tanzania tu ,nani anakumbuka alivyokufa Paul Walker ? Kila mtu alikuwa R.I.P Paul wakasahau na marehemu mwingine ambaye alikuwa dereva

Tukiiga tamaduni za wenzetu kuna mambo mengine tukifanya tutaambiwa tunapotoka kimaadili, eti kwa kuwa wazungu wanafanya.

Wao wana tamaduni zao na sisi tuna tamaduni zetu mkuu...!
 
Ndugu kiongozi, pesa inachukua thamani ya utu, hii inaonesha wazi kwamba hakuna politician ambaye yuko na mwananchi mnyonge, yale maneno kusema wako na wanyonge yote ni uzandiki na unafiki, na kudhirisha hilo Mungu naye hua anawaumbua kama hivi, lakini embu ona pamoja na hayo uandikwe magazetini uwe na cheo , unaishia mavumbini.

Unachokisema ni kweli kabisa kiongozi huwa wanakosea padogo sana na kujisahau.

Kiuhalisia tabia ni kama ngozi ya mwili huwezi kuibadili.

Hatari sana mkuu...!
 
Tukiiga tamaduni za wenzetu kuna mambo mengine tukifanya tutaambiwa tunapotoka kimaadili, eti kwa kuwa wazungu wanafanya.

Wao wana tamaduni zao na sisi tuna tamaduni zetu mkuu...!
Hakuna mahali nimesema tuige ,nimetoa mfano wa tukio kama hilo kuwahi kutokea

Halafu nisaidie vimetumika vigezo vipi kujua hii ID ni ya marehemu ?

Kina Nelson wapo wengi
 
Hakuna mahali nimesema tuige ,nimetoa mfano wa tukio kama hilo kuwahi kutokea

Halafu nisaidie vimetumika vigezo vipi kujua hii ID ni ya marehemu ?

Kina Nelson wapo wengi

Wangekuwepo hao wengi wangeshakuja kuthibitisha hapa na vyeti vyao na vitambulisho pia.

Ila kwa kuwa mpendwa wetu ameshafariki ndio mana anashindwa kuthibitisha angekuwa HAI angekuja kukuthibitishia mkuu. Ahsante.
 
Kwani ni lazima wawepo hapa kuthibitisha ? Kama wamesahau password ama hawatumii Jf tena ?

Wewe uliyesema hii ID ni ya marehemu ndio ulipaswa kuthibitisha hilo pasi na shaka

Anyway ya Ngoswe haya wacha tuwaachie kina Ngoswe .
 
Niliachana na king'amuzi cha Azam baada tu ya kuutenga mwili wa dereva wa costa na kuchukua miili ya watu wao tu hata kwenye matangazo yao hawakumgusia kabisa! So sad
 
Bongo kila ki2 connection
Walichokifanya n zaidi ya dharau kwa olotu nelson kawa kama vile mzoga wakat n binadam
 
Niliachana na king'amuzi cha Azam baada tu ya kuutenga mwili wa dereva wa costa na kuchukua miili ya watu wao tu hata kwenye matangazo yao hawakumgusia kabisa! So sad

Ni hatari sana kiongozi. Acha kabisa mkuu...!
 
Naomba kuuliza kupitia uzi huu.Mwanamke wa kwanza rubani Tanzania aliitwa Betty Olotu.Je wana uhusiano na huyu rubani Nelson Olotu

Sina hakika kiongozi natumai kutakuwa na wadau wenye kufahamu hilo wanaweza wakaja kutueleza kama wana uhusiano wowote au laa mkuu.
 
Back
Top Bottom