Mwanajeshi wa JWTZ achezea Kipigo cha Trafic Tabata

hao KM wafungwa wakifanya fujo hawaendi na mabomu ya machozi,ni ngumi tu mpaka wafungwa wanasalimu amri!kumbuka jela kuna mpaka askari,na wahalifu waliobobea! Hawa Jw waache kuonea raia bana alaa!
 
Tanzania ni nchi inayoongozwa katika misingi ya utawala wa kiraia unaofuata sheria(Japo sometimes hii ni nadharia ngumu kuelewa hasa pale sheria zinapopindishwa kulinda wateule fulani). Hii attitude ya askari wengi wa JWTZ kuwa wao ni everything kwa kuwa tu tumewakabidhi kutuangaliazia maghala yetu ya silaha tunazonunua kwa kodi sometimes huwa inatia hasira sana. Iweje askari aliyefundishwa kuwa na nidhamu ashindwe kuheshimu kazi za watu wengine?. Sitetei Trafiic kwani sometimes nao ni kero ila anapokuwa anatekeleza majukumu yake na kutokea mtu mwingine kumdhalilisha hiyo ni njia mojawapo ya kumfanya ashindwe fanya kazi yake.

Attitude ya askari wengi wawe Polisi au JWTZ ni kuwa wao wanastahili priority kuliko mtu yeyote. Nchi nyingi duniani askari huheshimiwa sana kwa sababu wanajitolea maisha yao kulinda wengine, heshima hiyo huwafanya askari kila wakati kuweka mbele masilahi ya wasio askari kuliko yao wao. Huyu askari jeshi aliyechapwa na Traffic anastahili kichapo hicho kwani ameshindwa kufahamu nafasi yake katika jamii. Lakini pia na askari Traffic nae anastahili lawama kwa kushindwa kudetect triggers of violence kutoka kwa huyo askari jeshi mpuuzi asiyejua nafasi yake katika jamii. Wakati wa ubabe umeisha siku hizi watu hawasifiwi kwa ujuzi wa kupiga ngumi au kutukana bali ni katika kutumia akili na maarifa kuleta mabadiliko chanya kwenye jamii.

Kama askari jeshi watakuwa na attitude ya avenge kwa mwenzao kupigwa watakuwa wanaendeleza mtazamo uleule wa ubinafsi badala ya kujijengea heshima kwenye jamii. Sisi wananchi tunajua kuwa aksri jeshi wananguvu za kufanya chochote kwa kuwa tumewakabidhi silaha zetu watulindie mipaka na maadaui wa nje na hata wa ndani ikibidi. Ningeshauri JWTZ na Polisi kuangalia upya mitaala yao hasa katika kujenga ATTITUDE on new recruitments. Attitude is the basis for everything. Kama watu hawa watakuwa trained kwa kupewa kiburi cha kuwa wao ni everything na wasiheshimu wengine matokeo yake ndiyo haya. Ila kama watafundishwa kuwaheshimu na kuwathimini raia na watu wengine na kamwe iwe ni mwiko kwa askari kumpiga raia, yaani iwe ni taboo fulani, kama ilivyo kwa mtu mwenye akili kupigana na mlevi alisiyetambua chochote, tutapata askari wazuri wenye huruma na raia wa nchi yao. Pia iwe ni marufuku kwa watawala kutumia askari kuwapiga raia wema, hasa pale wanapotekeleza hazi zao za maandamano ya amani.
 
Kwani JWTZ wao wanafundishwa ubabe na kuonea raia kule mafunzoni, mimi nilipita JKT, hatukufundishwa somo la kuwa adui waumma, sasa inakuwaje hawa jamaa kuleta kashkash mitaani ?
 
wengi wakiona trafiki wanadhani pengine si askari mkakamavu,lakini matukio mawili yaliyotokea ubungo mataa la yule trafiki aliyetoa nishai majambazi ni mfano hai,pia yule aliyewazidi nguvu askari wa Jwtz mpaka wakaenda kumshambulia kwa kumchangia. askari wa majeshi yote Tanzania ukitoa wenye mafunzo maalum kama makomandoo wanauwezo sawa wa hand to hand war,tena kwa taarifa yenu hakuna kikosi kilichopikwa vizuri kwaajili ya hand to hand kama KM wa jeshi la magereza!
nimewahi kuwasikia hao jamaa wa KM, wako kule Ukongo nasikia ni kikosi hatari sana, wanapiga karate sana, ni kweli pia ukiacha wale makomandoo wa JWTZ hiki ndicho kikosi kikali kwa matumizi ya mikono, sasa natamani hawa makorofi wa JWTZ WA MITAANI WANASE KWENYE MIKONO YA KM WA MAGEREZA WAKAKIONE CHA MOOTO
 
Hii yote ni matokeo ya kutoweka kwa nidhamu, kwa wanajeshi hawapendi kutii sheria.Kwa kuvaa Gwanda unakuwa juu ya sheria na taratibu?
 
mjeda kakutana na kiboko yake....nao wamezidi saa ingine......lakini kilio kwa yangeyange....mbona ndio kumekucha......bakabaka...yangeyange....yangeyange....bakabaka....he he

Preta wewe mumeo si Mjeda halafu unafurahia shem wako kupewa za chembe!!
 
Huyo traffic police kama hatapandishwa cheo basi atakuwa ameonewa! Haya ma JWTZ yanatia aibu jamani! yanastahili vichapo!
 
Tatizo hawa wanajeshi wanajiona wao ndio wao, wako juu ya sheria. Safi sana trafiki kwa kutembeza kichapo!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom