Labda wewe ndio kuwadi wa LOWASSA na genge lake,sie tupo hapa kuwaeleza ukweli wa nyuma ya pazia kumhusu huyu rafiki yetu said kubenea,kwa kuwa tunamjua anatujua na tumekua nae kwenye shida na raha hata alipomwagiwa tindikali alizodai kumwagiwa na hwa marafiki zake wapya ni sisi ndio tuliomsaidia,hiyo story ya june unayosema tuisome iko wapi sasa??mbona hukuiweka!Mwanahalisi tunapozungumzia limepoteza muelekeo tunaagalia heading father,siku zote msimamo wa gazeti uko kwenye heading sio makala za ndani ambazo huandikwa hata na waandishi wa nje ya gazeti husika,angeiweka mbele hiyo stori ya mzee nyaronyo tuone,mbona aliificha ndani...na tunapozungumzia mwanahalisi pengine mimi niwe wazi nazungumzia stori za kubenea ambazo ndio mara nyingi kama sio zote hukaa mbele na yeye huweka jina lake kwa kuwa anadai yeye huwa haandiki habari za maruhani a.k.a.na mwandishi wetu,hivyo kwa said tuliemjua huko nyuma ilikua hivi hata wewe kama mtu wa serikalini ukawa na kigongo unataka kuigonga serikali lakini unaogopa kupoteza kazi ikijulikana unampelekea said then yeye anachofanya ni kuweka jina lake na kukulinda wewe kama source ya habri kwa kutokutaja hata iweje,hiyo ndio kitu iliyompatia heshima saidi miongoni mwa watendaji waserikali wakajenga kumuamini sana na kumpelekea stori ambazo ndio pia zikakufanya wewe pia umjue...Lakini pia haimaanishi waandishi wote pale mwanahalisi wanakubaliana nae,kuna watu pale bado ni wazalendo wa kweli kama mzee NDIMARA ambae ndio kidogo haka kaheshima heshima kalikobaki ka mwanahalisi ni kwa ajili yake na bahati nzuri saidi hawezi kumpangia wala kumuingilia yule mzee,kwani yeye na saidi ni sawasawa na mlima kilimanjaro na kichuguu,hiyo ndio inayopelekea angalau watu kama kina Nyaronyo waweze kupeleka stori pale na zikachapishwa kama zilivyo japo sio mbele,mbele pale ni kwa ajili ya ROSTAM NA LOWASSA kuandikiwa wanachokitaka..habari ndio hiyo,mwenye kununa anune mwenye kucheka acheke!