MwanaHALISI: Makala ya leo ya Ndimara ni 'must read' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MwanaHALISI: Makala ya leo ya Ndimara ni 'must read'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Zak Malang, Jun 8, 2011.

 1. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #1
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Ukombozi waja… kipigo chayoyoma

  Na Ndimara Tegambwage

  Njia bora ya kuharakisha mabadiliko ya kisiasa nay a kiuchumi nchini Tanzania ni kubughudhi viongozi wa upinzani kila kukicha.

  Kamata. Bambika mashitaka. Weka rumande. Peleka mahakamani… Achia kwa dhamana. Kamata. Weka rumande. Fungulia mashitaka…kama jana, kama leo, kama kesho, kila siku.

  Wasimamizi wa mradi huu – wakipenyeza amri kwa watekelezaji – wanafikiri kwa njia hii, watafaulu kudhoofisha na hata kuua upinzani dhidi ya serikali chovu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

  Polisi hawafurahii kukamata. Polisi wanafurahia kubaki na ajira yao. Kubaki na vimishahara vyao. Ni ya magwanda yao yanayoelekeza urefu wa kamba yao katika kujikimu.

  Polisi wakamataji hawana masilahi katika kukamata viongozi wa upinzani. Wanatii amri ya wakubwa zao. Wakubwa wenye uswahiba na wakubwa siasani.

  Wanaotumiwa kukamata hawana masilahi katika kufyatua risasi. Katika kulipua mabomu ya machozi. Katika kumimina maji-pilipili machono mwa wananchi. Hawana!

  Ndani ya polisi nako kumejaa “Kabwela hana kitanda” – yule wa kwetu wanaita ndala omwa fulano – mtegemea fadhila!

  Watawala wanatoa amri. Polisao wanatii amri. Watawala wanatoa amri kujilinda leo. Leo hii. Kufika au kutofika kesho so hoja kwao. Wanataka leo nay a leoleo.

  Kwa hiyo kamata! Bambikia mashitaka. Weka rumande. Peleka mahakamani. Achia kwa dhamana. Kamata. Weka ruymande. Fungulia mashitaka… kama jana, kama leo, kama kesho, kila siku.

  Chukua mfano wa Mbowe. Freeman wa Chadema. Kijana mdogo tu mwenye mdomo mpana uliojaa ushawishi.

  Mbowe, kama Dk Willibrod Slaa na viongozi wengine wa Chadema, akilia wananchi wanaomsikiliza wanalia naye. Akicheka wanacheka naye. Akinuna wananuna naye. Watawala wanaamuru: kamata. Bambika mashitaka.

  Chuykua mfano wa Chadema. Chama ambacho kimejidhihirishia kuwa na uwezo mkubwa wa kuwafikia wananchi, kuwaibua kutoka lindi la woga na ujinga.

  Chukua mfano wa Chadema. Chama ambacho kimefuta umaarufu wa bandia wa CCM, kukinyang’anya wafuasi, kukibakizia wanafunzi wanaoswagwa na walimu wanaolinda ajira zao kama polisi.

  Chukua mfano wa Chadema. Chama ambacho wengi wanasema mgombea wake wa urais alishinda na CCM inakiri nguvu yake ndani ya vikao na kwenye hadhara.

  Chukua mfano wa umati wa wananchi unaojitokeza kwenye mikutano ya Chadema; maswali yanayoulizwa na wananchi na ahadi wanazotoa ili kuing’oa CCM

  Fuatilkia kashifa lukuki zilizoizonga CCM na serikali yake; kushindwa kwa chama hicho kujibu hoja kuhusu wizi ndani ya benki kuu, kuhusu matumizi hewa; kuhusu mikataba ya kihuni nay a kinyonyaji.

  Kazi ya kisiasa iliyofanywa na upinzani, hasa Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, imewezesha wananchi kuelewa kuwa CCM siyo chama cha siasa, ni chama cha ukwapuaji.

  Kukua na hata kuimarika kwa vyama vbya upinzani, hasa Chadema hakutokani na ubora na umakini wa viongozi wake peke yake. Kunatokana pia na mazingira ya kutota kwa waliotawala kwa miaka 50.

  Chadema wamepata fursa ya kuzunguka nchi na kueleza kuwa mataifa huadhimisha miaka 50 ya uhuru wake kwa kuonyesha utawala bora – kisiasa na kiuchumi.

  Lakini katika Tanzania, hasa tunapokaribia kuadhimisha miaka 50, watawala ndio huionyesha walivyo na makucha marefu ya kupora fedha na rasilimali za taifa.

  Viongozi wa Chadema wamewafafanulia haya wananchi; na wananchi wameelewa kuwa viongozi wengi wa sasa wanashindana kuiba dhahabu, alimasi, tanzanite, mbao na rasilimali nyingine.

  Wamewafafanulia wananchi jinsi viongozi walivyoshiriki ufisadi wa kila aina; wakitoa mifano kadha wa kadha na kuoanisha nay ale wanayoona na kufahamu.

  Uongo na kutosema ukweli; kutotekeleza ahadi kubwa na nzito kama kununua meli kwa matumizi katika Ziwa Victoria; kutokamata watuhumiwa wakuu wa ufisadi na tabia ya ndumila kuwili; vyote vimeelezwa kwa wananchi.

  Katika mazingira ya kawaida, viongozi wa CCM wanahitaji ujasiri wa mwendawazimu kusimama mbele ya umati kueleza mafanikio, matarajio na kuomba umma kuunga mkono.

  Wamewekwa uchi; wao na chama chao. Wamebakia kuanza na kumaliza mikutano yao kwa kusema “sasa tunajivua gamba.” Ndizo hotuba. Ndizo ahadi. Ndizo kinga za aibu.

  Huwezi kusikia tena viongozi wa CCM wakitamba na “Ari zaidi, Nguvu zaidi na Kasi zaidi.” Wamezimika. Watani zao hutafsiri ashirio hilo kuwa ni kifupi cha “ANGUKA” na huko ndiko Chadema inahubiri kuwa wanaelekea.

  Na ndani ya CCM kwenyewe mifarakano imeota ndevu. Ni piga nikupige. Kila anayefaulu kuchomoa kizinga anamchoma mwenzake.

  Katika mazingira haya ndimo tunakuta: kamata mbowe, kamata Slaa. Kamata Zitto. Bambika masitaka. Weka rumande. Peleka mahakamani… Fungulia mashitaka… kama jana, kama leo, kama kesho, kila siku.

  Mazingira haya yanaibua chuki. Yanaibua hasira. Yanachochea ujasiri wa kiwango cha juu wa kusema, “Hapana. Hatukubali tena kunyanyaswa.”……………..
  ………………………

  ……Habari zaidi katika MwanaHALISi ya leo uk 3.

   
 2. Mpevu

  Mpevu JF-Expert Member

  #2
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 23, 2010
  Messages: 1,816
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 0
  Hivi leo ni jumatano eeeeh!
  Dah mfuko umetoboka tayari...
   
 3. J

  Jasusi JF-Expert Member

  #3
  Jun 8, 2011
  Joined: May 5, 2006
  Messages: 11,484
  Likes Received: 165
  Trophy Points: 160
  Leo ni jumatano. Angalia tena kalenda yako. Isipokuwa kama unaishi Hawaii.
   
 4. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #4
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Hizo red nimezipenda sana.
   
 5. sulphadoxine

  sulphadoxine JF-Expert Member

  #5
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,264
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kuendelea kutumia polisi kuzima kauli,hakuwezi kubadili mwelekeo wa wananchi au hata wa polisi wenyewe;ule wakutaka mabadiliko
   
 6. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #6
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Hapo penye highlight: ni kwqeli siku hizi hatusikii kabisa hiyo kauli mbiu. Nasikiavyo aliibuni yule Mihungo Rweyemamu, mwandishi aliyefukuzwa Mwananchi kwa kukosa maadili na kukimbilia kulamba viatu vya RA.

  Kauli mbiu hiyo inawasuta CCM kwelikweli
   
 7. Indume Yene

  Indume Yene JF-Expert Member

  #7
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 2,932
  Likes Received: 42
  Trophy Points: 145
  Jasusi wee kichaa kweli, nimeangalia hii line nimecheka sana kwa sababu ni joke iliyo na ukweli ndani yake. Richukuwe hiro ri-THANKS.
   
 8. WISDOM SEEDS

  WISDOM SEEDS JF-Expert Member

  #8
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 1, 2011
  Messages: 782
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Hivi wewe upo dunia gani, hujui hata tarehe?
   
 9. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #9
  Jun 8, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Sidhan wenzangu waliopiga kura ccm na hali hii ya maisha wanajisikiajeeeee
   
 10. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #10
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0

  Kwani wangapi waliipigia CCM? Nzoiwa & Co ndo waliomnyonga Dr wetu wa ukweli na kumpa yule wa magamba!
   
 11. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #11
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kudos Ndimara! Kweli umeonyesha CCM ni finito -- inapumulia mashine, kama vile vile alivyotamka Tendwa hivi karibuni kuhusu hali ilivyokuwa wakati wa uchaguzi. Madudu yote haya wanayofanya CCM kwa kutrumia mapolisi wake ni kutapatapa. Na kama vile mtu anayetaka kuzama majini, huwa ni hatari sana anaweza kufanya lolote kujiokoa.

  Please CCM -- tokomea peke yako uwaache Watz kwa salama.
   
 12. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #12
  Jun 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Duh! Ari zaidi, Nguvu zaidi, Kasi zaidi = ANGUKA! Sina mbavu!
   
 13. A

  ADAMSON Senior Member

  #13
  Jun 8, 2011
  Joined: May 23, 2011
  Messages: 126
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Buriani chama cha mapinduzi
   
 14. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #14
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  hahahah, hichi kipande kweli kabisa bwana..ccm hawana jipya,sio kisera wala utendaji

  "Wamewekwa uchi; wao na chama chao. Wamebakia kuanza na kumaliza mikutano yao kwa kusema "sasa tunajivua gamba." Ndizo hotuba. Ndizo ahadi. Ndizo kinga za aibu."
   
 15. K

  KERENG'ENDE JF-Expert Member

  #15
  Jun 8, 2011
  Joined: Nov 14, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35

  Hivi CCM kuna mtu mwenye akili timamu wa kusoma alama za nyakati zilizopo na kutoa tafsiri sahii kwa chama chao? hakika hayupo kwa maana hiyo lazima wa kabiliwe na mauti.......................
   
 16. sblandes

  sblandes JF-Expert Member

  #16
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 25, 2010
  Messages: 2,467
  Likes Received: 790
  Trophy Points: 280
  Safari bado ni ndefu ya kulisogeza taifa hili karibu na mataifa yaliojijengea heshima kwa wananchi wake, kwa mtaji huu wa CCM hatufiki.tumedumaa.
   
 17. N

  Nkomoji JF-Expert Member

  #17
  Jun 8, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 235
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndimara kashusha mistari ya ukweli.
   
 18. pascaldaudi

  pascaldaudi JF-Expert Member

  #18
  Jun 8, 2011
  Joined: Mar 25, 2009
  Messages: 534
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Katika yoote; ANGUKA=Ari zaidi NGuvu zaidi KAsi zaidi
   
 19. fredmlay

  fredmlay JF-Expert Member

  #19
  Jun 8, 2011
  Joined: Apr 30, 2008
  Messages: 1,855
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 135
  Kufaidi zaidi ni kulipata mwanahalisi lote la leo kama lilivyo na sio vipande
   
 20. k

  kusisimba Member

  #20
  Jun 8, 2011
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 37
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hongera ndimara kwa makala yenye ukweli halisi, meseji imefika. Hopeful wataelewa.
   
Loading...