MwanaHALISI: Makala ya leo ya Ndimara ni 'must read'

Kumbe ndo sababu walianguka,wanamtafuta mchawi aliyewaloga wakaanguka, wakati kauli mbiu yao inasema ''anguka'' sasa utaepuka vipi anguko. Mh! kazi ipo. Watz tusifurahie sana hayo cha msingi tumwombe Mungu sana ili hata kama ni mageuzi yatatokea isewe kama misri,tunisia n.k. Waombaji wa taifa waongeze msuli wa maombi
 
MS uko wapi comment basi, au umekuwa mbuni kuficha ichwa mat.ko yapo nje?
 
[

Na Ndimara Tegambwage

Njia bora ya kuharakisha mabadiliko ya kisiasa na a kiuchumi nchini Tanzania ni kubughudhi viongozi wa upinzani kila kukicha.

Kamata. Bambika mashitaka. Weka rumande. Peleka mahakamani… Achia kwa dhamana. Kamata. Weka rumande. Fungulia mashitaka…kama jana, kama leo, kama kesho, kila siku.

Wasimamizi wa mradi huu – wakipenyeza amri kwa watekelezaji – wanafikiri kwa njia hii, watafaulu kudhoofisha na hata kuua upinzani dhidi ya serikali chovu ya Chama cha Mapinduzi (CCM).

Polisi hawafurahii kukamata. Polisi wanafurahia kubaki na ajira yao. Kubaki na vimishahara vyao. Ni ya magwanda yao yanayoelekeza urefu wa kamba yao katika kujikimu.

Polisi wakamataji hawana masilahi katika kukamata viongozi wa upinzani. Wanatii amri ya wakubwa zao. Wakubwa wenye uswahiba na wakubwa siasani.

Wanaotumiwa kukamata hawana masilahi katika kufyatua risasi. Katika kulipua mabomu ya machozi. Katika kumimina maji-pilipili machono mwa wananchi. Hawana!

Ndani ya polisi nako kumejaa “Kabwela hana kitanda” – yule wa kwetu wanaita ndala omwa fulano – mtegemea fadhila!

Watawala wanatoa amri. Polisi wao wanatii amri. Watawala wanatoa amri kujilinda leo. Leo hii. Kufika au kutofika kesho sio hoja kwao. Wanataka leo naya leoleo.

Kwa hiyo kamata! Bambikia mashitaka. Weka rumande. Peleka mahakamani. Achia kwa dhamana. Kamata. Weka ruymande. Fungulia mashitaka… kama jana, kama leo, kama kesho, kila siku.

Chukua mfano wa Mbowe. Freeman wa Chadema. Kijana mdogo tu mwenye mdomo mpana uliojaa ushawishi.

Mbowe, kama Dk Willibrod Slaa na viongozi wengine wa Chadema, akilia wananchi wanaomsikiliza wanalia naye. Akicheka wanacheka naye. Akinuna wananuna naye. Watawala wanaamuru: kamata. Bambika mashitaka.

Chuykua mfano wa Chadema. Chama ambacho kimejidhihirishia kuwa na uwezo mkubwa wa kuwafikia wananchi, kuwaibua kutoka lindi la woga na ujinga.

Chukua mfano wa Chadema. Chama ambacho kimefuta umaarufu wa bandia wa CCM, kukinyang’anya wafuasi, kukibakizia wanafunzi wanao swagwa na walimu wanaolinda ajira zao kama polisi.

Chukua mfano wa Chadema. Chama ambacho wengi wanasema mgombea wake wa urais alishinda na CCM inakiri nguvu yake ndani ya vikao na kwenye hadhara.

Chukua mfano wa umati wa wananchi unaojitokeza kwenye mikutano ya Chadema; maswali yanayoulizwa na wananchi na ahadi wanazotoa ili kuing’oa CCM

Fuatilia kashifa lukuki zilizoizonga CCM na serikali yake; kushindwa kwa chama hicho kujibu hoja kuhusu wizi ndani ya benki kuu, kuhusu matumizi hewa; kuhusu mikataba ya kihuni nay a kinyonyaji.

Kazi ya kisiasa iliyofanywa na upinzani, hasa Chadema, CUF na NCCR-Mageuzi, imewezesha wananchi kuelewa kuwa CCM siyo chama cha siasa, ni chama cha ukwapuaji.

Kukua na hata kuimarika kwa vyama vbya upinzani, hasa Chadema hakutokani na ubora na umakini wa viongozi wake peke yake. Kunatokana pia na mazingira ya kutota kwa waliotawala kwa miaka 50.

Chadema wamepata fursa ya kuzunguka nchi na kueleza kuwa mataifa huadhimisha miaka 50 ya uhuru wake kwa kuonyesha utawala bora – kisiasa na kiuchumi.

Lakini katika Tanzania, hasa tunapokaribia kuadhimisha miaka 50, watawala ndio huionyesha walivyo na makucha marefu ya kupora fedha na rasilimali za taifa.

Viongozi wa Chadema wamewafafanulia haya wananchi; na wananchi wameelewa kuwa viongozi wengi wa sasa wanashindana kuiba dhahabu, alimasi, tanzanite, mbao na rasilimali nyingine.

Wamewafafanulia wananchi jinsi viongozi walivyoshiriki ufisadi wa kila aina; wakitoa mifano kadha wa kadha na kuoanisha nay ale wanayoona na kufahamu.

Uongo na kutosema ukweli; kutotekeleza ahadi kubwa na nzito kama kununua meli kwa matumizi katika Ziwa Victoria; kutokamata watuhumiwa wakuu wa ufisadi na tabia ya ndumila kuwili; vyote vimeelezwa kwa wananchi.

Katika mazingira ya kawaida, viongozi wa CCM wanahitaji ujasiri wa mwendawazimu kusimama mbele ya umati kueleza mafanikio, matarajio na kuomba umma kuunga mkono.

Wamewekwa uchi; wao na chama chao. Wamebakia kuanza na kumaliza mikutano yao kwa kusema “sasa tunajivua gamba.” Ndizo hotuba. Ndizo ahadi. Ndizo kinga za aibu.

Huwezi kusikia tena viongozi wa CCM wakitamba na “Ari zaidi, Nguvu zaidi na Kasi zaidi.” Wamezimika. Watani zao hutafsiri ashirio hilo kuwa ni kifupi cha “ANGUKA” na huko ndiko Chadema inahubiri kuwa wanaelekea.

Na ndani ya CCM kwenyewe mifarakano imeota ndevu. Ni piga nikupige. Kila anayefaulu kuchomoa kizinga anamchoma mwenzake.

Katika mazingira haya ndimo tunakuta: kamata mbowe, kamata Slaa. Kamata Zitto. Bambika masitaka. Weka rumande. Peleka mahakamani… Fungulia mashitaka… kama jana, kama leo, kama kesho, kila siku.

Mazingira haya yanaibua chuki. Yanaibua hasira. Yanachochea ujasiri wa kiwango cha juu wa kusema, “Hapana. Hatukubali tena kunyanyaswa.”……………..
………………………

……Habari zaidi katika MwanaHALISi ya leo uk 3.






Jamani ni maombi yangu hii thread istoke kurasa ya kwanza. Yaliosemwa humu hayawezi kabisa kuisha utamu mpaka baada ya 2015. Hongera Ndimara umesema yote.
 
.."Huwezi kusikia tena viongozi wa CCM wakitamba na “Ari zaidi, Nguvu zaidi na Kasi zaidi.” Wamezimika. Watani zao hutafsiri ashirio hilo kuwa ni kifupi cha “ANGUKA” na huko ndiko Chadema inahubiri kuwa wanaelekea."

Kumbe unaweza kujitabiria kifo chako bila wewe mwenyewe kujua! Nimeipenda hii!
 
Nakumbuka mechi ya hivi majuzi kati ya Barca na ManU, Man walipoteana sana na wakachapwa na ndo yanayowakuta ccm on political ground! RIP ccm.
 
Mbona siwaoni vijana wa Nape kwenye hii thread wandugu? Nadhani wanaukubali huu ukweli hopeless as they are
 
Mzee Ndimara ni mwandishi makini sana na yuko straight. Hana muda wa kulazimisha storiibalance kama kina majid mjengwa...
!big up mzee ndimara!
 
Jamani msisahau kufa kwa nyoka mpaka umugonge kichwani.

Chadema kama kweli wanataka kumalizia wasiishie kwenye nyimbo tamutamu tu wasonge mbele pamoja na kamata kamata.

Wakati wengine wanakamatwa watakao bahatika basi wafike kunakotakiwa.

Kwa sasa CHADEMA na CCM ni sawa sawa na kuwa na timu bora yenye kiwango cha kucheza ulaya (CHADEMA) kukutana na timu yenye majeruhi watupu (CCM) halafu kiwango chake ni daraja la pili nchini.
 
Mbona neno "ZAIDI" kwenye kifupisho cha hii kauli mbiu limesahaulika? ZAIDI limerudiwa mara tatu kukazia umuhimu wake. Kwa vile tumeambiwa chama kilikuwa na "Umaarufu wa Bandia" ina maana tayari kilikuwa kimeshaanza ku- ANGUKA. Sasa utabiri ulioletwa na kauli mbiu ulimaanisha ANGUKA Zaidi.
 
Mzee Ndimara amesema kile ambacho kilitegemewa kwamba ni wazi. Ndugu zangu wanachama na viongozi wa CCM ukweli haufichiki Chukueni hatua acheni kutoa shukurani za kinafiki kwa kikwete mwambieni tena na tena anachemka na kicheko chake kimegeuka kuwa "kero" ya kitaifa.
 
Back
Top Bottom