MwanaHalisi lamshinda Rostam

Hapa hapa hapa.
Na mtaji wa hilo lijalo atapewa na nani? Pasco, utakuja kutueleza siku si nyingi ulijuaje??
Kwani mtaji wa Mwanahalisi alipata wapi?. Kisima kile kile alichochota, kitatema tena. Hapa nimetoa angalizo tuu kwa Kubenea, mwenye nguvu mpishe. 'mtu nazo pesa' RA ana pesa, hahitaji hizo bilioni 3 kwa Kubenea bali anataka kumkomoa tuu ili mfadhili wake aingie vitani wakati anadai Shilingi moja 1/= tuu kwa mfadhili Mangi ili kuonyesha dharau kuwa lengo lake sio kutafuta fedha.
 
Huyu jaji munuo ni jaji mbarikiwa sana sijawahi kusikia mashauri yake lakini uwamuzi huu ni wa haki iliyotukuka na nirahisi mno. Baraka na laana ni vitu rahisi na vya bure ushauri wa gharama kwa yeyote ' chunga sana kiburi chako hasa cha mali bahati mbaya mali uliyoipata isivyo halali. Mali hizi za ujanja ujanja zina laana tosha ya kudumu , halafu ukiongezea ongezea chembe chembe za viburi nikama kumwaga mafuta nishati kwenye kijinga cha moto.
 
Katika uhasibu kuna suala moja gumu sana kulithamanisha. Nalo ni "GOODWILL" Wakati baadhi ya wahasibu uionyesha "Goodwill" kama asset ya kampuni katika Balance Sheet wengine huiacha kabisa maana ni very subjective. Ugumu huo huo unajitokeza katika taaluma ya sheria kuamua juu ya hoja hapo juu. Wanasheria naomba msaada wenu hapa maamuzi yanafikiwaje kuthibitisha mtu hadhi yake imechafuliwa na kuvunjiwa heshima au kinyume chake?




Watu wa JF binafsi nawaheshimu sana. Mara nyingi wakitoa angalizo au pendekezo, utalikuta liko katika hatua za utekelezaji baada ya muda mchache. Sintochangaa kukuta Mwana Halisia already booked at BRELA.

Hapa mkuu lazima uangalie previous cases zimeamuaje jambo hili. Hapo ndio wanasheria wanafanya kazi na kutumia muda mwingi. Unacheki kesi zilizopita, unalinganisha na ya kwako, alafu unaweza ku-argue zinafanana au hazifanani. Pana utamu kweli hapo. Kumbuka, sheria ni kesi, ndio maana tuna common law. Mimi binafsi sina uhakika na sheria ya bongo na hasa kesi wanazotumia kuweza kusema kwa uhakika kuwa kuvunjwa kwa heshima au kuchafuliwa hadhi ni nini.
(Lakini kama unanilipa, naweza kukutafutia...hahaha). Natania tu hapo mkuu...
 
RA na wana siasa na maisadi against wazalendo wasio na kitu ila wenye moyo wa uzalendo wa nchio yao..........mwisho itakuwaje??yangu macho hasa kuelekeo 2010
 
Mimi nilidhani mahakama ya rufani imetengua hukumu ya mahakama ya chini, kumbe utekelezaji tu? sasa ushindi uko wapi hapo!!! au tunaendeleza ushabiki kwa mbele.
 
Naona kama hiyo hukumu imekaa kisiasa zaidi. RA hawezi shinda kesi yoyote ya kuchafuliwa jina hapa Tanzania. Hebu tungoje hizi za Mengi.
wewe unaleta ndoto hapa kwa kuwa hata hii thread iliotumwa hapa tayari ameshawashinda mwanahalisi,na mwanahalisi wanmekata rufaa kwa hio kinachongojewa ni hukumu yao ya rufaa isikilizwe kwanza kabla ya kutekelezwa adhabu waliopewa ya kumtukana Mh R.A.Aziz
 
Ndio maana nikaita kesi hizi ni kesi sumbufu. Thamani ya mtu katika jamii ni jinsi anavyojithaminisha yeye mwenyewe ndio maana RA huyo huyo kadai bilioni 3 kwa Kubenea halafu amedai Shilingi 1/= tuu kwa Mangi.
Mahakama imepewa full discretion kuamua kiasi gani ndio kilipwe.
Mawakili wanaopenda litigation ndio wanaentartain kesi hizi. Mawakili waangalia mbele hawawezi kukubali hivi vikesi vya usumbufu, time consuming at the end of the day, you end up with nothing.
Lengo la RA ni kumkomoa Mangi kwaakuifilisi Mwanahalisi kwa sababu Kubenea is funded na Mangi. Kwa wenye akili timamu, wanamuona Akama insane fulani kutaka bilioni 3 kwa Kubenea who has nothing halafu anadai shilingi 1 kwa Mangi whos has everything.
Hapa hatuna nafasi kwa watu wanaolopoka lopoka bila kwa na taarifa ni kama vile mnakurupuka au kusikia habari za mitaani then mnakuja nazo hapa.hakuna mahali Mengi amedaiwa na Rostam shs moja
 
Hapa hatuna nafasi kwa watu wanaolopoka lopoka bila kwa na taarifa ni kama vile mnakurupuka au kusikia habari za mitaani then mnakuja nazo hapa.hakuna mahali Mengi amedaiwa na Rostam shs moja

Na wewe nawe! akisemwa RA tu hapo ndipo wewe utokea. Kwenye issue zingine unakuwaga wapi???????????????? Kwa Rostam??????????
 
Hongera Kubenea na Mwana Halisi kwa kumgaragaza fisadi papa,nawatakia mafanikio zaidi kumteketeza fisadi huyo papa wa rasilimali za nchi yetu.
 
Sijaelewa ina maana kumbe kuna kifungu cha namna hiyo! Hongera Kubenea

Hapo sioni sababu ya kumpa Hongera Kubenea, kwa uelewa wangu kutokana na sentgansi hii ni kuwa RA anastahili kulipwa fidia lakini point ya kulipa au kutolipa fidia inajieleza hapo juu.
 
sina utaalamu wa sheria sana, lakini tasfiri rahisi ya habari hii ni kwamba Mwanahalisi wamefannikiwa tu kuzuia utekeleza wa kesi aliyoshinda RA, sijajua haswa je imependekezwa utekelezaji upi? na je Mwanahalisi ni kweli wameshindwa hii kesi na wamekubali walimkosea RA?
lazima wajue kwamba RA anaposhinda hizi kesi anapata nguvu na anawapa nafasi wengine kuhofia madai yanayotolewa dhidi yake kwamba huenda yakawa ni yakuzusha...mwanahalisi lazima ujue unaiweka jamii katika nafasi gani katika hoja zako zote usije ukawa na ajenda ikawagawa wananchi....

KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI LAZIMA TUWE MAKINI ZAIDI...MAFISADI WAKO MAKINI PIA....
 
sina utaalamu wa sheria sana, lakini tasfiri rahisi ya habari hii ni kwamba Mwanahalisi wamefannikiwa tu kuzuia utekeleza wa kesi aliyoshinda RA, sijajua haswa je imependekezwa utekelezaji upi? na je Mwanahalisi ni kweli wameshindwa hii kesi na wamekubali walimkosea RA?
lazima wajue kwamba RA anaposhinda hizi kesi anapata nguvu na anawapa nafasi wengine kuhofia madai yanayotolewa dhidi yake kwamba huenda yakawa ni yakuzusha...mwanahalisi lazima ujue unaiweka jamii katika nafasi gani katika hoja zako zote usije ukawa na ajenda ikawagawa wananchi....

KWENYE MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI LAZIMA TUWE MAKINI ZAIDI...MAFISADI WAKO MAKINI PIA....
hapo umesema kweli mkuuu mimi mwenyewe naunga mkono vita dhidi ya mafisadi lakini kwenye issue hiiii naona mwanahalisi wamejisahau sana na kuanza kuleta unazi kueindeleza vita ya RA na Mengi, nawaelewa kwasababu ni mfadhili wenu lakini hata hivyo mngeweza kuipresent hiyo issue kwenye angle yenu wenyewe kama mwanahalisi bila kuonekana kwamba mnajaribu kujiegemeza kwa Mengi, na hilo linaweza kuwasabibishia kupoteza imani kwa wananchi kama sisi coz we all know Mengi na Wahindi wana perdsonal issues na anatumia issue hii ya ufisadi km revenge kwao, but kama wananchi sisi hatutaki tuone personal business war between Mengi na RA , sisi tunataka tuone mwanahalisi anaendelea kutuelimisha na kufichua maovu ya hawa mafisadi bila kuonekana ni mshabiki wa fulani
 
Endeleza libeneke Mwanahalisi, huyu Rostam anajiona yupo juu ya sheria! kwa ufupi ni kwamba watanzania tumemchoka!
 
Last edited:
Inviolata
user_online.gif


DUH!huu ni uzao halisi wa invisible!
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom