MwanaHalisi lamshinda Rostam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

MwanaHalisi lamshinda Rostam

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Halisi, Jun 19, 2009.

 1. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #1
  Jun 19, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Habari zilizotufikia hivi punde zinaeleza kwamba wamiliki wa gazeti la MwanaHalisi, Hali Halisi Publishers Limited, wamefanikiwa kumzuia Rostam Aziz kutekeleza hukumu iliyowataka wamlipe mfanyabiashara huyo mabilioni ya fedha.


  Mafanikio hayo yamepatikana kufuatia hukumu iliyotolewa jana na Jaji Eusebio Munuo wa Mahakama ya Rufani, aliyezingatia kwamba MwanaHALISI na wenzake wakilazimishwa kumlipa Rostam bilioni 3/- wataathirika lakini Rostam hawezi kuathirika kwa kutolipwa.


  stay tuned
   
 2. Exaud J. Makyao

  Exaud J. Makyao JF-Expert Member

  #2
  Jun 19, 2009
  Joined: Nov 30, 2008
  Messages: 1,523
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Imekuwa kama NGONJERA sasa.
  Haya, yetu macho.
   
 3. Kibunango

  Kibunango JF-Expert Member

  #3
  Jun 19, 2009
  Joined: Aug 29, 2006
  Messages: 7,639
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  Hukumu zingine....... mMMhm!
   
 4. MawazoMatatu

  MawazoMatatu JF-Expert Member

  #4
  Jun 19, 2009
  Joined: Sep 6, 2008
  Messages: 505
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hongera Mwanahalisi!
   
 5. M

  Mkandara Verified User

  #5
  Jun 19, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Sasa Rostam na Wizara watawalipa mwanahalisi gharama za kufunga gazeti hilo kwa muda wote ikiwa ushindi ni wa mwanahalisi?
   
 6. Ochu

  Ochu JF-Expert Member

  #6
  Jun 19, 2009
  Joined: May 13, 2008
  Messages: 972
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  hii habari imekaa tenge...this is called in law stay of execution ambayo haimaanishi kubadilisha unamuzi wa awali wa mahakama bali zuio la kutekeleza hukumu wakati rufaa inaendelea...mko hapo?
   
 7. Kikojozi

  Kikojozi JF-Expert Member

  #7
  Jun 19, 2009
  Joined: Mar 24, 2009
  Messages: 331
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Naona kama hiyo hukumu imekaa kisiasa zaidi. RA hawezi shinda kesi yoyote ya kuchafuliwa jina hapa Tanzania. Hebu tungoje hizi za Mengi.
   
 8. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #8
  Jun 19, 2009
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Sijaelewa ina maana kumbe kuna kifungu cha namna hiyo! Hongera Kubenea
   
 9. Halisi

  Halisi JF-Expert Member

  #9
  Jun 19, 2009
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 2,810
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  uko sahihi, kwani si kwamba wamefuta hukumu, ila wamezuia utekelezaji wa hukumu, lakini pia muelekeo wa kesi ya msingi kuamuliwa irudiwe ni mkubwa kwani haikufuata taratibu za kesi.


  Hoja ya mawakili wa MwanaHalisi ilijikita katika Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai (The Civil Procedure Act, 1966 [Toleo la Marejeo 2002]) ambapo waliomba Rostam azuiwe kutekeleza hukumu ya Jaji Makaramba kwa sababu itakiuka misingi ya sheria.
  Pia waliieleza Mahakama kwamba wakati Jaji Makaramba alifikia hatua ya kutoa uamuzi wa upande mmoja wa bila kusikiliza ushahidi wa upande wa pili na kuamuru MwanaHALISI wamlipe Rostam bilioni 3/-, alikiuka Sheria ya Mwenendo wa Kesi za Madai, ambayo inatamka wazi katika fungu la VIII kanuni ya 14 (Order VIII, Rule 14) kuwa uamuzi wowote utakaotoa fidia inayozidi 1,000/- hauwezi kutolewa bila kusikilizwa upande wa pili.
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Jun 19, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,536
  Trophy Points: 280
  Kesi zote za defamation na libel ziko very tricky na ni kesi sumbufu ambapo mahakama kuu inadescretion ya kuamua vyovyote.
  Msingi mkuu wa kesi hizi ni kuchafuliwa jina infront of the right thinking members of the society.
  Hoja ambayo Mwanahalisi angeweza kuishiklia ni kuwa RA hajachafuliwa na kuvunjiwa heshima yake kwa sababu tayari ni mchafu na hiyo heshima anayodai anayo, hana.
  Assets zote na liabilities za Hali Halisi haziwezi tosha kutekeleza hukumu husika.
  Wakati rufani inasubiriwa, ni vyema Kubenea akajiweka salama kwa kukaa mkao wa utayari kuifilisi Mwanahalisi na kuanzisha Mwana Halisia.

  Ukishadeclare umefilisika, hukumu inakuwa haitekelezeki kesi inakuwa imekwisha. Tunaendelea na Mwana Halisia.
   
 11. Kaa la Moto

  Kaa la Moto JF-Expert Member

  #11
  Jun 19, 2009
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 7,666
  Likes Received: 166
  Trophy Points: 160
  Hivi wan jf naomba nieleweshwe mbona kesi zote za kuchafuliwa jina ni za RA v/s .......?
  Kwa nini hajiulizi kwa nini wadanganyika wananituhumu sana kutokuwa msafi? anadhani kwa kufanya hivyo kutamsafisha? Namuonea huruma!
   
 12. Dilunga

  Dilunga JF-Expert Member

  #12
  Jun 19, 2009
  Joined: Apr 8, 2009
  Messages: 679
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mwanzoni hukujua hii ni interlocutory decision ambayo hai affect kesi ya msingi au uliamua tu kupotosha?

  Eti MwanaHalisi lamshinda Rostam. Kina Halisi hawa ndio wapashaji habari wa jamvi. Wapotoshaji ile mbaya.
   
 13. Kilasara

  Kilasara JF-Expert Member

  #13
  Jun 19, 2009
  Joined: Dec 21, 2008
  Messages: 578
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Hongera sana Saeed Kubenea. Hata hivyo ushauri wa Pasco hapo juu ni vizuri ukauzingatia, ili hata kama Hukumu rasmi ya Mahakama ya Rufaa ikiwa unfavourable to Mwana Halisi Publishers, uwe umeshajihami.
  Tunakupenda na kukuthamini sana sisi wana harakati. Uzi ni huo huo.
   
 14. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #14
  Jun 19, 2009
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Tutajie hizo kesi zote unazodai ili tujadili kesi baada ya kesi, otherwise tutakuelewesha vipi. Eleweka ili ueleweshwe.
   
 15. N

  Njimba Nsalilwe JF-Expert Member

  #15
  Jun 19, 2009
  Joined: Mar 23, 2008
  Messages: 251
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kwa mfano hii hapa nyingine, hebu tueleweshe kwa nini ni yeye tu?

  Rostam files 28bn/- libel case against Mengi

  DAILY NEWS Reporter, 19th June 2009 @ 02:49, Total Comments: 0, Hits: 277

  A prominent businessman, Mr Rostam Aziz, has sued the IPP Chairman, Reginald Mengi, listing several demands, including 28bn/- compensation as general damages for defamation.

  In the suit filed by his advocate, Mr Kennedy Fungamtama on June 5, this year, at the High Court in Dar es Salaam, Mr Aziz is demanding the amount as general damages for libel, hashed up falsehoods and malicious misrepresentation of facts uttered and published by the plaintiff to the general public.

  Mr Aziz wants an unconditional apology and retraction of defamatory statements made by Mengi at a press conference on April 23, this year, in Dar es Salaam, in which the latter labelled former as a “shark” of corruption.

  On the same day, Mengi is alleged to broadcast or aired on ITV a special programme called ‘Kipindi Maalum’ in which he uttered defamatory words about Mr Aziz. The special programme was repeated on April 27, this year, according to the charges.

  Mr Aziz claims that the libellous statements complained of, apart from injuring his reputation and credit, stir irksome elements in public and incited or perpetuated hatred against him, thereby endangered his life and that of his family members.

  The defendant, therefore, prays for an injunction against the plaintiff as well as his agents and associates, restraining them from repeating the libellous/defamatory in any form.

  Mr Aziz also seeks an order compelling Mr Mengi to air on ITV and publish, at his expense, the approved apology and retraction in three consecutive issues of all mainstream newspapers, namely: the Daily News, ThisDay, Kulikoni, Nipashe, The Guardian, The Citizen, Mtanzania, The African, Uhuru, HabariLeo, Majira, Tanzania Daima and Business Times.

  Mr Aziz, who is also a Member of Parliament for Igunga (CCM), seeks an order against the plaintiff to pay the defendant costs of and incidental to the suit and any other relief the High Court deems just and fit.

  Early last month, through Ngalo & Company Advocates, Mengi equally filed a suit at the High Court against Aziz, seeking several demands, including 10bn/- compensation as general damages for libel. In his suit, Mengi claimed that he was defamed by Aziz at a press conference on May 1, this year, in Dar es Salaam, whereby the latter called him a ‘whale’ of corruption.
   
 16. R

  Rwabugiri JF-Expert Member

  #16
  Jun 19, 2009
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 2,777
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 135
  Huu sasa ni mchezo wa kuigiza. Wacha tusubili hitimisho lake.

  Ila kwa Kubenea, hongera walau kwa hatua hii ya awali.
   
 17. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #17
  Jun 19, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Katika uhasibu kuna suala moja gumu sana kulithamanisha. Nalo ni "GOODWILL" Wakati baadhi ya wahasibu uionyesha "Goodwill" kama asset ya kampuni katika Balance Sheet wengine huiacha kabisa maana ni very subjective. Ugumu huo huo unajitokeza katika taaluma ya sheria kuamua juu ya hoja hapo juu. Wanasheria naomba msaada wenu hapa maamuzi yanafikiwaje kuthibitisha mtu hadhi yake imechafuliwa na kuvunjiwa heshima au kinyume chake?


  Watu wa JF binafsi nawaheshimu sana. Mara nyingi wakitoa angalizo au pendekezo, utalikuta liko katika hatua za utekelezaji baada ya muda mchache. Sintochangaa kukuta Mwana Halisia already booked at BRELA.
   
 18. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #18
  Jun 20, 2009
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 24,569
  Likes Received: 18,536
  Trophy Points: 280
  Ndio maana nikaita kesi hizi ni kesi sumbufu. Thamani ya mtu katika jamii ni jinsi anavyojithaminisha yeye mwenyewe ndio maana RA huyo huyo kadai bilioni 3 kwa Kubenea halafu amedai Shilingi 1/= tuu kwa Mangi.
  Mahakama imepewa full discretion kuamua kiasi gani ndio kilipwe.
  Mawakili wanaopenda litigation ndio wanaentartain kesi hizi. Mawakili waangalia mbele hawawezi kukubali hivi vikesi vya usumbufu, time consuming at the end of the day, you end up with nothing.
  Lengo la RA ni kumkomoa Mangi kwaakuifilisi Mwanahalisi kwa sababu Kubenea is funded na Mangi. Kwa wenye akili timamu, wanamuona Akama insane fulani kutaka bilioni 3 kwa Kubenea who has nothing halafu anadai shilingi 1 kwa Mangi whos has everything.
   
 19. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #19
  Jun 20, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
   
 20. Omutwale

  Omutwale JF-Expert Member

  #20
  Jun 20, 2009
  Joined: Feb 4, 2008
  Messages: 1,429
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Hapa hapa hapa.
  Na mtaji wa hilo lijalo atapewa na nani? Pasco, utakuja kutueleza siku si nyingi ulijuaje??
   
Loading...