VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,140
- 18,004
Si kitu cha ajabu kwa gazeti la michezo kuta habari nyingine, na si kinyume cha sheria. Mara nyingi magazeti ya akina Shigongo huwa yanaandika habari za siasa, utadhani Uhuru.
isitoshe mwaka 1995 wakati akina Jenerali Ulimwengu walipoanzisha Dimba (la michezo) gazeti hilo lilikuwa linaandika habari za siasa, zakampeni za uchaguzi, hadi pale walipoanzisha Mtanzania, na baadaye RAI.
Lakini ninachohofia hapa ni kwamba katika serikali hizi za kihovyo hovyo inaweza pia kulifungia gazeti hilo kutimiza uchu wake wa kuwaziba wananchi wasijue jinsi serikali yao inavyofanya unyama kwa wananchi wake.
Halafu kitu zaidi kinachonishangaza ni kwamba serikali ilishindwa kabisa kuelezea kivipi Mwanahalisi kilisema uongo katika matoleo yake iliyotaja kukiuka maadili kuhusu sakata la Ulimboka.
Mimi nadhani imefika wakati sasa serikali iwaambie wananchi kuwa sakata la kutekwa ulimboka halikuwapo kabisa na kwamba daktari huyo huenda alipigwa na mke wake nyumbani.
Sijaona serikali kama hii. Lile gazeti la Rupert Murdoch la NEWS OF THE WORLD lilikowa linaandika habari za uongo za kupotosha umma na wahariri wake kudukuu simu za watu wengine hazlikufungwa na serikali ya huko Uingereza, mmiliki wake mwenyewe ndiyo aaliamua kulifunga kuondoa malalmiko.
kwani anaeruhusu kuanzishwa magazeti mengine ni nani?au mtu yeyote anaweza amka asubuhi na kuanzisha gazeti?Serikali ikiua adui mmoja inazalisha wengine 100, kufungwa kwa mwanahalisi ni kufungua midomo ya magazeti mengine...
Ni kweli Mkuu...Serikali ikiua adui mmoja inazalisha wengine 100, kufungwa kwa mwanahalisi ni kufungua midomo ya magazeti mengine...
hizi gumzo zinanikumbusha enzi ya magazeti kama motomoto,wakati ni huu,etc .Uwezi kuziba uhuru wa habari kwakufungia vyombo vya habari.....huu ni udikiteta nijinsi gani washahuri wa habari wasivyokuwa makini wakidhani ukifungia chombo cha habari utakuwa umejiosha kwa umma wa watanzania!!Kumbe ndo kwanza unawafumbua akili wakitaka kujua nini kimefanyika mpaka gazeti linafungiwa!!
kwani anaeruhusu kuanzishwa magazeti mengine ni nani?au mtu yeyote anaweza amka asubuhi na kuanzisha gazeti?
Ngoja nikalitafute...Katika kile kinachoonekana ni kufuata ushauri wa JF katika kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kupata habari zenye mshiko,leo Gazeti dada la MwanaHALISI la Mseto limebeba makala ya kisiasa tofauti na kawaida ya gazeti hilo kusheheni michezo.
Ukurasa wa mbele kabisa wa Mseto la leo kuna makala iliyoandikwa na Mhariri wa MwanaHALISI Comredi Jabir Idrissa yenye kichwa cha maneno 'Kilicholiponza MwanaHALISI ni hiki'.Katika makala hiyo,Idrissa anachambua kwakina makala zinazosemekana kuwa siliiudhi Serikali na kupelekea kufungiwa gazeti pendwa la MwanaHALISI.
Wakati huohuo,Gazeti la RaiaMwema linaloongozwa na Gwiji wa Uandishi, Jenerali Ulimwengu aka Mzee wa G55, nalo limejitokeza katika toleo la leo kupinga ubabe wa Serikali kufungiafungia magazeti ya kiuchunguzi. Aluta Continua...
Naona kama Wanatapa tapa vile mbona kilichoandikwa kwenye Mseto ni copy & Paste ya kilichoandikiwa kwenye Mwanahalisi Jumatano iliyopita.Katika kile kinachoonekana ni kufuata ushauri wa JF katika kuhakikisha kuwa wananchi wanaendelea kupata habari zenye mshiko,leo Gazeti dada la MwanaHALISI la Mseto limebeba makala ya kisiasa tofauti na kawaida ya gazeti hilo kusheheni michezo.
Ukurasa wa mbele kabisa wa Mseto la leo kuna makala iliyoandikwa na Mhariri wa MwanaHALISI Comredi Jabir Idrissa yenye kichwa cha maneno 'Kilicholiponza MwanaHALISI ni hiki'.Katika makala hiyo,Idrissa anachambua kwakina makala zinazosemekana kuwa siliiudhi Serikali na kupelekea kufungiwa gazeti pendwa la MwanaHALISI.
Wakati huohuo,Gazeti la RaiaMwema linaloongozwa na Gwiji wa Uandishi, Jenerali Ulimwengu aka Mzee wa G55, nalo limejitokeza katika toleo la leo kupinga ubabe wa Serikali kufungiafungia magazeti ya kiuchunguzi. Aluta Continua...