mwalimu mpole1
Member
- Aug 2, 2012
- 9
- 15
tatizo la siku hizi unachanganya waalimu competent, wa upe,na wa voda faster,wa corruption sasa hapo ndipo umoja unapokosekana.very sad.zaman teacher alikuwa anaheshimika sana siku izi naona walimu mmeshindwa kuwa wamoja na kuwa na sauti moja
Oh poor teacher. I am sorry too. Lakini miaka miwili na nusu sio mbali, msijisahau.
umeichonga wewe? Nenda kwa banda huko.Hadithi nzima niya kuchonga kwa kuangalia uhalisia wa mazingira ya mwalimu na mwanafunzi wawapo shuleni hasa mwalimu anapokuwa anaingia darasani . Japo ukweli ni kwamba walimu hawalipwi vizuri.
haitho yako nzuri
Wengi mnafahamu SHULE ZIMEFUNGWA ILA DARASA LA SABA NA LA NNE BADO WANAENDELEA NA MASOMO WAKIJIANDAA NA MITHANI YA TAIFA. L eo nilipoingia darasa la saba kufundisha nimekuta watoto wanamjadala mkubwa. kwakuwa kelele zilikua nyingi nikalazimika kujua kuna nini. Watoto wote walicheka kisha ikawa hivi:
Mimi: Mbona mnapiga kelele hamna kazi ya kufanya?
Wanafunzi: kicheko
Mtoto: Hamis si useme tu?
Zaituni: msiposema nawasema
Mimi: Zaitini niambie mama yangu!
Mtoto mwingine: Eti ni kweli mshahara wenu ni mdogo sana kuliko hata......(anataja kazi)
Mimi: Nitawaambia siku zijazo. Tuendelee na somo la leo. (NAPOTEZEA). Kisha naandika ubaoni mada dogo ya leo. METHALI NA NAHAU. (nikaligeukia darasa na ona watoto bado wanacheka). Haya Hamis tumbie methali yoyote uliyoweza kupata kwenye habari tuliyosoma jana.
Hamis: Fimbo ya wanyonge ni umoja wao
Mimi: Vizuri! Sasa nani anaweza kuifafanua methali hii.
Hamis: Mfano mwalimu ninyi si mnalipwa kidogo mkiwa na umoja mtalipwa nyingi na nyinyi kama wengine.
Watoto: kicheko
Mimi: Naanzisha wimbo na watoto wanaitikia huku wakicheka (napotezea ila naumia naamua kuandika maswali ubaoni ) fanyeni maswali haya kisha monitor utaniletea kwenye dawati langu.
Kilichoniuma si ukweli kuwa tunaloipwa kidogo ni ile hali ya kuona hata watoto tunaowafundisha nao wanaidharau kazi hii kiasi hiki!
Mbona umetoa maswali(zoezi) wakati umefundisha methali moja tu?