Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza UDOM adaiwa kutaka kujiua kisa wivu wa mapenzi

Mwanafunzi wa Mwaka wa Kwanza anayesoma Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM) ambaye jina lake halijawekwa wazi inadaiwa ametaka kufanya jaribio la kujiua akiwa chuoni hapo chanzo kikitajwa ni masuala ya mapenzi.

Inaelezwa kuwa tukio hilo limetokea jana Aprili 25, 2024 wakati alipokuwa katika moja ya majengo ya chuo hicho (Block H, Collage of Education).

Taarifa za awali zimeeleza kuwa alipokorofishana na mpenzi wake litaka kujirusha kutoka Ghorofa ya Nne.

Inadaiwa amelazwa Hospitali ya Benjamin Mkapa kwa ajili ya matibabu baada ya kuonekana hayupo sawa.

Taarifa zaidi zitafuata.


MAELEZO YA UDOM
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Masoko wa UDOM, Rose Mdami alipoulizwa amesema haya:

Taarifa za Tukio hilo ni za kweli, huyo kijana ameumia kiasi na amelazwa katika Hospitali ya Benjamin Mkapa akipatiwa huduma, inadaiwa alifanya jaribio la kutaja kujiua na taarifa za awali zinaonesha kuwa chanzo ni masuala ya mapenzi.

Unajua huwa kuna changamoto ya tabia hasa kwa baadhi ya vijana hasa wa Mwaka wa Kwanza, lakini sisi kama Chuo tumeshirikisha mamlaka za kiutawala na kiusalama zinazohusika ili ziweze kufanya kazi yao.

Baada ya hapo kijana huyo akipata hali nzuri kiafya tutaingia kwenye masuala mengine yanayofuata ikiwemo ushauri wa Kisaikolojia.
UDOM napo utake kujiua hatar Sana baada wawaze ukame unaowakabiri pale nusu jangwa😂😂😂
 
Back
Top Bottom