Mwanafunzi wa Feza ashangaa wanaofeli mtihani wa NECTA

Mwanafunzi wa Feza ashangaa wanaofeli mtihani wa NECTA

Sihitaji kupeleka mtoto shule alafu aanze kusahau Kiswahili na kujirembua (kuongea kwa ishara) namna hii. ukileta mtoto wa kizungu hapo utakuta anaongea straight tu, ila wa kibongo lazima alete mbwembwe. au angeletwa hata wa international school of TAnganyika tu. hata hivyo, nampongeza mzazi na mtoto kwa hatua hiyo.
 
Bado ni mtoto anazungumza anachokiaona machoni mwake, siku akiwa na utambuzi atajua ni kwa nini wanaofanya hizo NECTA wanaona ngumu.

Ni sawa sawa na mtoto anayemuona Baba yake ndio tajiri pekee duniani.
Akikua lini wakati ameshakuambia ni rahisi kwake? Tafuta hela umpeleke mwanao mwanamvua hizo shule za international
 
Watu wamekasirika wakati dogo kaongea ukweli tupu.
Kwa sasa mwanafunzi hapaswi feli wakati notisi zimejaa kila mahali.

Wazazi hawafatilii maendeleo ya watoto wao hivyo mtoto aende au asiende shule haiwahusu.

Watawala na watawaliwa huandaliwa na wazazi
 
Watu wamekasirika wakati dogo kaongea ukweli tupu.
Kwa sasa mwanafunzi hapaswi feli wakati notisi zimejaa kila mahali.

Wazazi hawafatilii maendeleo ya watoto wao hivyo mtoto aende au asiende shule haiwahusu.

Watawala na watawaliwa huandaliwa na wazazi
FB_IMG_1577871864627.jpg
 
Kuna tofauti ndogo sana baina ya kiburi na kujiamini.

Japo dogo anahisi kaongea kwa kujiamini, kihalisia kinachosikika hapo ni kiburi, majigambo na dharau.

By the way, bwana mdogo kesha left group. Uzungu mwingi una madhara yake nao. Nina hakika hapo alipo anaji identify kama 'they/them'.
Sawa ana akili nyingi, je marinda yapo?
 
Utofauti uliopo kati ya Shule za serikali na Shule za Kulipia ni Mkubwa mno kuanzia Hata kwny Mindset tu ya Mwalimu na Mwanafunzi husika,

Mfano Halisi anzia tu Hata Mtaani kwenu angalia watoto wanaosoma Internationa schools na Hizi za Serikali yani Utaona kabsa Maji na Mafuta vilee vinajitenga.

Watt wa Shule za serikali wakilud nyumbani kazi Kuangalia Singeli na Nyimbo za Amelowa hku wakisindikizwa Na migogoro ya Baba na mama ndani ya Nyumba hivi unafkiri hyo mtoto Saikolojia yake itakuw sawa kweli ?

Mambo ni mengi sana nataman hat nianzishe Thread yangu kabsa nielezee hili kiundani ila Kiufupi Ufaulu wa Mtoto unaanzia Na Misingi ya Wanafamilia/kifamilia.
 
Back
Top Bottom