Mwanafunzi wa darasa la kwanza anastahili hivi ?????.....

nnunu

JF-Expert Member
Mar 4, 2011
654
230
Habari ndugu wadau wa elimu,
samahani naomba ufafanuzi katika hili,
mtoto wa darasa la kwanza kweli anatakiwa kufundishwa haya yote kwa umri wa miaka 6-7 alionao?

1-kiswahili
2-english
3-mathematics
4-science
5-reading
6-v/skills
7-pds
8-spelling

je katika umri huo ataelewa vizuri masomo yote hayo? Ubongo wake upo tayari kupokea yote hayo?...masomo yote hayo yana class work na home work kila siku, mtoto ni lazima abebe daftari zote kila siku anapoenda na kurudi shule,anabeba daftari 16 na diary ya 17 kila siku . Je hii imekaa sawa??. Nilipowauliza waalimu wakasema wao wanafuata tu walivyoambiwa kufanya na uongozi wa shule husika.
Tafadhari ndugu wadau wa elimu naomba ufafanuzi katika hili kwa mtoto wa darasa la kwanza je linamjenga kitaaluma??, linaendana na capacity ya ubongo wake??.
Naheshimu michango yenu yote, pia naamini ntapata ushirikiano toka kwenu, asanteni.
 
Mmmmmh masomo nane!!! Hapana aisee nadhani ni mzigo mzito kwa mtoto kama hiyo. Nakumbuka enzi zetu ni masomo matatu HESABU, KUANDIKA na LUGHA.
 
ni kwa english medium skul ndo wana hayo mambo.! Huku kwetu (st kayumba) ni masomo ma3 tu: mwandiko, hesabu na uraia @ std 1.
 
ni kweli ni english medium,,,LD na Puupuu nimewaelewa asanteni. Naendelea kusubiri michango ya wadau mbalimbali, ili walitoe ufafanuzi zaidi katika hili.
 
Back
Top Bottom