vantz
JF-Expert Member
- Apr 22, 2016
- 1,107
- 570
Alitupwa dirishani kutoka ghorofa ya 3 ingia YouTube global tv online utaona video dah inasikitisha mnooooWakati Akwilina akiuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye daladala maeneo ya mkwajuni kinondoni jijini Dar, Feb 16 mwaka huu, mwanafunzi Shija Daudi Kasuku (20) wa chuo kikuu cha Elimu ya Biashara (CBE), Tawi la Dar, alidaiwa kuuawa kwa kusukumwa kutoka ghorofa ya tatu hadi chini.
Shija aliyekuwa akisomea Diploma ya Biashara akiwa yupo mwaka wa pili chuoni hapo, alidaiwa kuuawa na mwanafunzi mwenzake kwa kile kilichosemekana kwamba ni wivu wa kimapenzi.![]()