Mwanafunzi mbaroni kwa kubaka mwenzie | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mwanafunzi mbaroni kwa kubaka mwenzie

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Rutashubanyuma, Jan 3, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Mwanafunzi mbaroni kwa kubaka mwenzie


  Na Suleiman Abeid, Shinyanga

  JESHI la Polisi mkoani Shinyanga linamshikilia mwanafunzi wa kidato cha kwanza katika Shule ya Sekondari Kishimba wilayani Kahama kwa kosa la kumbaka mwanafunzi wa shule ya msingi wa darasa la sita mwenye umri wa miaka 11.Kamanda wa
  Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Diwani Athumani alimtaja mwanafunzi kuwa ni Frank Stephano (16) mkazi wa mjini Kahama na kwamba tukio hilo lilitokea juzi saa 1.30 usiku.

  Kamanda Athumani alisema mtuhumiwa huyo alifanya unyama huo baada ya kumvamia mwanafunzi huyo wa kike (Jina na shule vimehifadhiwa) aliyekuwa katika matembezi ya kusherehekea mwaka mpya huko katika kitongoji cha Nyasubi mjini Kahama ambapo
  alianza kumbaka kwa nguvu.

  Hata hivyo alisema mwanafunzi huyo alipiga kelele za kuomba msaada kutoka kwa wapita njia ambao walifika na kufanikiwa kumkamata mtuhumiwa ambapo walimpeleka katika kituo cha polisi cha mjini Kahama.

  Tunamshikilia mtuhumiwa huyo na baada ya kukamilika kwa uchunguzi wa tukio hilo tutamfikisha mahakamani kujibu shtaka la ubakaji, tunawashukuru wananchi waliowezeshwa kukamatwa kwake na kumfikisha mikononi mwa vyombo vya dola pasipo kujichukulia sheria mkononi,alieleza Bw. Athumani.

  Katika tukio lingine, polisi wilayani Bukombe inamshikilia mkazi wa Wilaya ya Chato mkoani Kagera kwa kosa la kupatikana na pikipiki inayohisiwa aliipata kwa njia za wizi.

  Kamanda Athumani alimtaja mtuhumiwa anayeshikiliwa kuwa ni Bw. Elius Joseph (25) mkazi wa Chato ambaye alikamatwa mwishoni mwa wiki iliyopita saa saba usiku akiwa na pikipiki aina ya SANLG yenye namba za usajili T. 896 BCM.

  Alisema polisi waliokuwa doria huko katika Kijiji cha Runzewe walimkamata mtuhumiwa huyo ambapo alipotakiwa kutoa maelezo juu ya uhalali wa kumiliki pikipiki hiyo alishindwa kufanya hivyo na hivyo kukamatwa na anatarajiwa kufikishwa mahakamani baada ya kukamilika kwa uchunguzi.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Jan 3, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,305
  Likes Received: 417,643
  Trophy Points: 280
  Wanafunzi wanapoyatelekeza majukumu yao yaliyowapeleka shule ujue hiyo jamii....is finished......................
   
 3. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #3
  Jan 3, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Watoto wa siku hizi tabu tupu.
   
 4. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #4
  Jan 4, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Yani mdogo hivyo tayari kafikia kubaka??Kweli kazi ipo!!Sasa na yeye atapigwa miaka 30 jela au anaachwa kwasababu ni minor?
   
Loading...