Ushauri wangu kwa watu wote wanaenda kama kundi/group kwenye beach,wawe makini sana kama hujui kuogelea sio dhambi kaa pembeni angalia wenzako,usipende sifa za kijinga kujitupa kwenye maji huku hujui kuogelea kwa kupenda sifa mbele ya mademu au marafiki.
Wote tutakufa,lakini tusikibipu kifo.
Najiuliza msimu huu ni wa mvua nyingi sana kwa maeneo yote ya mkoa wa Tanga hususani Pangani,pili ilikuwaje aogelee eneo la Sea side hostel ambalo lipo jirani na makutano ya bahari na mto Pangani??
Kasi ya maji eneo hilo ni kubwa sana,pia kuna mawimbi makali halikadhalika maji ni machafu sana kwa wakati huu wa mvua,hasa yale yanayotoka mto Pangani.
Inatia simanzi sana kwa familia!
Mungu asaidie apatikane akiwa hai!!