Ikula
Member
- Feb 4, 2017
- 87
- 138
Wanajamvi,naomba kuliweka wazi hili mwaka Jana 2016 mwezi August katika shule ya sekondari Kidodi kuna mwanafunzi alisimamishwa masomo kwa tuhuma kuwa ana ujauzito baada ya kwenda kupima zahahati ya Kidodi wilaya ya kilosa binti hakukutwa na ujauzito lakini bodi ikaidhinisha kufukuzwa kwake na akalazimishwa kusaini kukubaliana na maamuzi ya bodi,lakini binti huyu cha ajabu aliitwa kufanya mtihani wa Taifa wa kidato cha pili mwaka jana na amefaulu vzuri lakini bado shule imekataa kumpokea hata kutoa uhamisho wamegoma wanalazimisha mtoto tumpeleke private na wazazi hawana uwezo nimekuja kwenu kuomba ushauri