Ndugu jf kwa masikitiiko makubwa mwanafunzi wa chuo kikuu aliyepigwa risasi usiku wa leo na majambazi amefariki dunia asubuhi mapema leo..
R.I.P Alex
Inaskitisha sana, poleni sana Mungu awatie nguvu.
Wanafunzi Wa chuo kikuu udsm waliokuwa wakijisomea kwa maandalizi ya mitihani ya mwisho wamevamiwa na kuporwa vitu vyote zikiwemo laptop 3 na mmoja wao kupigwa risasi na kukimbizwa hospitali.
Mgogoro mkubwa Ni kwa polisi Wa chuo(auxiliary) ambao hawakuonyesha ushirikiano katika kuwasaka wezi..
Matukio haya yamekuwa yakijitokea Mara kwa Mara chuoni hapa.
...(get wel soon our brother..)
Polisi wapunguze nguvu kupambana na chadema na kuongeza nguvu ya kupambana na uhalifu..Hivi hawa policcm kazi yao ni nini. Hii siyo mara ya kwanza kwa wanafunzi kuvamiwa, kuibiwa mali zao, kujeruhiwa, kufanyiwa kitu mbaya-IFM. Ni hivi karibuni matukio ya kutisha yametokea katika taasisi za elimu nchini mfano Chuo cha Uuguzi DOM, AIA,IFM na sasa UDSM. Cha kushangaza wanaofanya mambo haya hawakamatwi. Je; hawa policcm ni mpaka Kamanda wao avamiwe ndio usikie kuna watu wamekamatwa?