Mwanafunzi chuo kikuu UDSM apigwa risasi- Afariki

Mwanafunzi chuo kikuu UDSM apigwa risasi- Afariki

Status
Not open for further replies.

Simply

Senior Member
Joined
Oct 13, 2012
Posts
130
Reaction score
30
Wanafunzi Wa chuo kikuu udsm waliokuwa wakijisomea kwa maandalizi ya mitihani ya mwisho wamevamiwa na kuporwa vitu vyote zikiwemo laptop 3 na mmoja wao kupigwa risasi na kukimbizwa hospitali.

Mgogoro mkubwa Ni kwa polisi Wa chuo(auxiliary) ambao hawakuonyesha ushirikiano katika kuwasaka wezi..
Matukio haya yamekuwa yakijitokea Mara kwa Mara chuoni hapa.

(get wel soon our brother..)

======= Updates =========

Ndugu jf kwa masikitiiko makubwa mwanafunzi wa chuo kikuu aliyepigwa risasi usiku wa leo na majambazi amefariki dunia asubuhi mapema leo..
R.I.P Alex
 
....kwa habari iliyonifikia hivi punde, wanafunzi wakiwa darasani maeneo ya Yombo-UDSM ghafla wamevamiwa na majambazi waliofanikiwa kuwapora laptop zao na kumjeruhi mwanachuo mmoja wa mwaka wa Nne-Sheria kwa risasi ambaye inasemekana yuko mahututi....japo amekimbizwa Hospitalini. Ni taaruki tupo sasa Chuoni hapo, na Walinzi wa Chuo haonekani hata mmoja.

Kwa habari kamili tutaendelea kujuzana, kwa kadri nitakavyo kuwa nazipata
 
Wanafunzi Wa chuo kikuu udsm waliokuwa wakijisomea kwa maandalizi ya mitihani ya mwisho wamevamiwa na kuporwa vitu vyote zikiwemo laptop 3 na mmoja wao kupigwa risasi na kukimbizwa hospitali.
Mgogoro mkubwa Ni kwa polisi Wa chuo(auxiliary) ambao hawakuonyesha ushirikiano katika kuwasaka wezi..
Matukio haya yamekuwa yakijitokea Mara kwa Mara chuoni hapa.
...(get wel soon our brother..)

Hivi hawa policcm kazi yao ni nini. Hii siyo mara ya kwanza kwa wanafunzi kuvamiwa, kuibiwa mali zao, kujeruhiwa, kufanyiwa kitu mbaya-IFM. Ni hivi karibuni matukio ya kutisha yametokea katika taasisi za elimu nchini mfano Chuo cha Uuguzi DOM, AIA,IFM na sasa UDSM. Cha kushangaza wanaofanya mambo haya hawakamatwi. Je; hawa policcm ni mpaka Kamanda wao avamiwe ndio usikie kuna watu wamekamatwa?
 
Hivi hawa policcm kazi yao ni nini. Hii siyo mara ya kwanza kwa wanafunzi kuvamiwa, kuibiwa mali zao, kujeruhiwa, kufanyiwa kitu mbaya-IFM. Ni hivi karibuni matukio ya kutisha yametokea katika taasisi za elimu nchini mfano Chuo cha Uuguzi DOM, AIA,IFM na sasa UDSM. Cha kushangaza wanaofanya mambo haya hawakamatwi. Je; hawa policcm ni mpaka Kamanda wao avamiwe ndio usikie kuna watu wamekamatwa?
Polisi wapunguze nguvu kupambana na chadema na kuongeza nguvu ya kupambana na uhalifu..
Inauma sana...Kama wasomi tunatendwa hivi masikini hohehae watakuwa wapi..?
 
..maandamano yameanza kuelekea polisi.##
 
Tetesi zilizonifikia hivi punde ni kuwa kuna mwanafunzi wa mwaka wa IV wa Chuo Kikuu Dar es Salaam amepigwa risasi na wezi waliokuwa katika jaribio la kumwibia kompyuta wakati akiwa anajisomea kwenye ukumbi wa Yombo 1.
Endelea kuwa nami kwa taarifa zaidi kadiri zitakavyonifikia...
 
Ni mambo yasiyo na msingi wowote kwa sasa,nchi imekosa maadili na kila kitu kimejaa siasa zisizo na msingi.na ni swala rahisi tu,mara nyingi baba wa nyumba alivyo ndiyo atatoa hata taswira ya familia yake ilivyo.nchi haina usimamizi madhubuti kuanzia ngazi ya juu kabisa na sasa sumu hiyo ya siasa,uzembe,kutokuwajibika,utani na mzaha kwenye maswala ya msingi imefika hadi kwenye uvungu wa taasisi ndogondogo kabisa.
Hawa auxiliary police hapa udsm wanashutumiwa kwa kushiriki maswala ya wizi kwa muda mrefu mno na wanafunzi wanavamiwa na kuibiwa lakini hata siku moja hawa polisi hawajawahi kukamata mtu.tunawajua wanavuta tu bangi wengi wao na kuvizia first years waliosimama kicouples usiku sana ili kuwachachafya na kuwadai pesa.
Swala la wizi hapa udsm ni kama issue ya kawaida kabisa sasa na sasa linakuwa hadi kufikia hatua ya watu kuvamiwa na kupigwa risasi kwa mali ndogo tu kama laptop na simu.
Silaha zimezagaa tu mitaani siku hizi mtu hata akikwaruzana na mwenzie kwenye foleni barabarani kila mtu anashuka na bastola yake na kuanza kumtishia mwenzie. Intelijensia ya nchi ii wapi??hao wanaoitwa usalama wa taifa wako wapi..(tunawakuta kwenye mabaa kila siku wakijisifia kuwa wao ni usalama wa taifa na hakuna wa kuwagusa)
Kwa kifupi tanzania kwa sasa hali si shwari kabisa,usalama haupo wa uhakika na kuna mambo mengi viongozi wetu wanayafanya huko ikulu,kwenye maofisi ya serikali na kwenye ziara zao za nje kwa manufaa yao na vizazi vyao na kusahau kabisa watanzania na mustakabali wa taifa hili.
Tuombe MUNGU atusaidie kweney kipindi hiki cha mpito lakini pia na mwenzetu ambaye tulikuwa tumalize naye mitihani leo hii MUNGU amponye.
Bado Naipenda Tanzania.
 
Duh poleni saana!! hii ni nouma aise!! Eneo ya chuo, majambazi wa Laptop duh kweli hali ni mbaya huko nyumbani.
 
Inasikitisha sana, poleni sana lakini pia hii inazidi kuonyesha taswira kuwa nchi imewashinda hawa watawala wetu.
 
by JOHN BUKUKU on JUNE 21, 2013



Taarifa zilizotufikia katika chumba cha habari zinaeleza kuwa wanafunzi wanne wa chuo kikuu cha Dar es salaam maarufu kwa jina la Chuo cha Mlimani wamevamiwa na majambazi usiku wa kuamkia leo maeneo ya Yombo chuoni hapo.


Wanafunzi hao wanaosemekana kuwa ni wa mwaka wa nne na wa mwisho wa masomo walikuwa wanajisomea na kuandaa "Disertation" zao na kujikuta wakivamiwa na watu wanne na kuamuriwa watoe komputa zao na pochi za fedha.


Kwa mujibu wa chanzo cha habari hii kutoka chuoni hapo, wanafunzi hao walikubali kuwapa komputa hizo na pochi za fedha, na majambazi kuanza safari yao.


Baadaye wanafunzi hao wakawaomba wapate hata nakala (Soft Copy) ya vitu vyao, na ndipo mmoja wao akaamua kuwafuata na kukumbana na risasi tumboni.


Mwanafunzi huyo baada ya kupigwa risasi alianguka chini na kugaagaa chini huku akikosa msaada wa kupelekwa Hospitalini.


Chanzo kimeendelea kusema kuwa wanafunzi wa Chuo hicho waliwasiliana na uongozi ili kupata gari ili wamkimbize mwenzao Hospitalini, lakini ilipita takribani nusu saa hakuna majibu na ndipo walipoamua kujikusanya na kuamua kuwafuata viongozi.


Kwa sasa mwanafunzi huyo amekimbizwa Hospitalini kupata matibabu zaidi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyotoka, ingawa FULLSHANGWE inajitahidi kufuatilia suala hilo ili kupta taarifa zaidi na picha za tukio hilo.


Tukio hilo limelaaniwa vikali na UMMA wa chuo kikuu cha Dar es salaam na kuitaka serikali kufuatiliwa na kudhibiti vitendo hivyo vya kikatili chuoni hapo.


Endelea kufuatilia katika mtandao huu amboa umefunga safari ya kuelekea Chuo kikuu cha Mlimani kuangalia nini kinaendelea.


Mbali na tukio hilo, pia kumekuwepo na wizi wa hadharani katika shule za Chuo hicho ambapo hivi karibuni wanafunzi wamekuwa wakiporwa komputa zao mchana kweupe maeneo ya Mikocheni wakitoke shule kuu ya uandishi wa Habari na Mawasilinao ya Umma (SJMC).


Suala hizi limepoteza amani kwa wanafunzi na kuwafanya washindwe kusoma kwa amani.



 
Mwanafunzi wa mwaka wa nne kitivo cha sheria kwa jina la ALEX, amepigwa risasi tumbon na majambazi. Tukio hlo limetokea saa nane na nusu usiku, ktk ukumbi wa yombo 1 ambapo alikuwa na wenzake watatu wakijisomea kwa ajili ya mtihani wa kesho. Majambaz hayo yamepora laptop 3, simu na pesa. Ulinz hapa chuo ni mdogo sana,na kuna maaskari lakini hawakuwapo na walijifisha. Tukio hlo limesababisha wanafunz kuandamana usiku mzima, wakitaka kujua haki zao za kulindwa na hao mapolsi ambao wamekuwa hawawajibiki. Toka saa nane mlio wa risasi ulilia na waliusikia lakini hawakutokea na wakati wapo mita kama 200 kutokea sehemu ya tukio. Majeruh alifikishwa hospitali ya chuo na wanafunz wenyewe, sasa amepelekwa moi, na mungu atamsaidia. Baba professor mkandala tunaomba usikie kilio chetu na muimarishe ulinzi. Sijui kama mwanafunz huyo angekuwa foreina Udsm ingekuaje. TUMEWACHOKA MApolisi. Inasikitisha sana
 
Hii pia ni sababu ya RuHUSA ya WAZIRI MKUU BUNGENI Jana? Sababu Polisi hawana WOGA wowote... Hakuna Mashitaka Lakini Hao Mawaziri na Wabunge wanao hawasomi NCHINI na Pia Hawafanyi kazi NCHINI
 
Pole sana Mwanafunzi Mwenyezi amponye ampe afya ,Kwa kauli ya PINDA(Pm) sijui jamaa alikuwa mbishi hakutii amri" akapigwa tu"na wakaidi wapigwe tu-lakini na hao vibaka wameshindwa kwenda kuvunja benk wanakuja kwa wachumia njaa wenzao?si kuna kituo cha polisi pale chuo utawala hawakufika?

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom